Kanisa la
Waadventista la Waadventista Wa Sabato nchini Uholanzi limesema mmoja wa
viongozi wa kanisa hilo alinusurika kuhusika kwenye ajali ya ndege ya Malaysia
baada ya kubadilisha tiketi ya kusafiri
na ndege hiyo iliyodunguliwa huko Mashariki mwa Ukraine juma lililopita na kuua
watu 298 papo hapo.
Mwenyekiti
wa Unioni Konferensi ya Uholanzi Wim Altink amesema jana kuwa Frieda
Souhuwat-Tomasoa alikuwa amekata tiketi ya ndege hiyo namba 17 kutoka
Amsterdam kuelekea mji mkuu wa Malaysia
Julai 17 mwaka huu lakini alibadilisha tiketi dakika chache kabla ya kuondoka
kwa ndege hiyo na kuamua kusafiri na ndege ya shirika la ndege la Emirates.
Souhuwat-Tomasoa
ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Unioni konferensi ya Uholanzi na mzee wa
kanisa la Rotterdam Kaskazini alikuwa akisafiri kuelekea Ambon,Indonesia kwa
ajili ya kuusaidia umoja wa mataifa kwa ajili ya kushughurikia mgogoro wa
kidini uliodumu katika eneo hilo kwa muda wa miaka 10 sasa.
Souhuwat-Tomasoa kwa sasa yuko Moluccas, Indonesia na amekuwa
akisafiri kuelekea Ambon katika visiwa vya Maluku vilivyoko mashariki mwa
kisiwa cha Sulawesi akiwa ni mjumbe wa umoja wa mataifa kwenye mpango huo.
Taarifa
zinaeleza kuwa mbili ya tatu ya abiria waliopanda ndege hiyo ni raia wa
uholanzi ambako julai 21,mwaka huu viongozi wa makanisa walishiriki kwenye
maombi ya maalum ya kuwaombea waliopoteza ndugu na jamaa kwenye ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment