Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa
ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibarkilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni
utekelezaji wa miradi yadharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada
ya Mvua kubwa.
Mradi huoambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Mradi huoambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto
akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa
ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa
Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande
cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi
wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya
kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa kwa kiwango cha
changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani
wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru
Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida
ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna
Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za
Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa
kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi
huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa
nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya
ujenzi wa barabara hiyo
No comments:
Post a Comment