Baadhi ya wahariri wa vyombo anuai vya habari wakiuliza maswali kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.
MTANDAO
wa Wanawake na Katiba nchini Tanzania umewakutanisha baadhi ya Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na
Katiba kujadili namna ya kushinikiza masuala ya haki za wanawake
kuingizwa katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
Semina
hiyo iliyoshirikisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na
wanahabari imeanza leo katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es
Salaam na itafanyika kwa siku mbili yaani Julai 24 na 25, 2014.
Akizungumza kukaribisha washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa
TAMWA, Valerie Msoka alisema wajumbe katika mkutano huo watajadili
umuhimu wa kuimarisha masuala ya haki za wanawake katika Katiba.
Alisema
kuwa wajumbe pia watajadili namna ya kutetea na kulinda masuala muhimu
ya haki za wanawake yaliyojitokeza katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya
ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na masuala
ya katiba yenye maslahi ya wanawake na taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary
Rusimbi ambao ni moja ya taasisi zilizoratibu mkutano huo, alisema
pamoja na mambo mengine madhumuni ya mkutano huo ni kuwawezesha wabunge
wanawake kwa wanaume katika Bunge Maalum la Katiba na wanaharakati wa
jinsia na haki za wanawake kuimarisha hoja zao.
Katika
mkutano huo wahariri wa vyombo anuai vya habari kwa nyakati tofauti
waliwataka wajumbe hao kuvitumia ipasavyo vyombo vya habari ikiwa ni
pamoja na kutoa ushirikiano ili hoja zao ziingie katika vyombo hivyo na
kuifikia jamii.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la Katiba wakizungumza
kujibu baadhi ya maswali ya wahariri wa habari walisema wamejipanga
kupaza sauti kuhakikisha hoja zao wanazozipigania zinaingizwa katika
Katiba Mpya.
Naye
Mjumbe wa Bunge Maalum, Dk. Avemaria Semakafu alivitaka vyombo vya
habari kuendelea kuwaunga mkono wanamtandao hao ili kupigania kero za
akinamama na wananchi kwa ujumla na kuhakikisha zinapata majibu katika
mchakato wa uundaji katiba mpya
Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa mkutano
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi akiwasilisha mada
katika katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na
Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.
Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Ruth Meena akiwasilisha mada.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (kulia) akiwasilisha mada
kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba.
Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo.
Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo.
Baadhi ya wahariri wa vyombo anuai vya habari wakiuliza maswali kwa
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba.
Baadhi
ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa
Wanawake na Katiba wakichangia mada katika mkutano huo Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba katika mkutano huo
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa
Mtandao wa Wanawake na Katiba wakifuatilia mada mbalimbali katika
mkutano huo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment