Wajumbe kutoka Serikali
ya Japan wakichukua mambo ya muhimu wakati Mkutano wa Majadiliano ulipokuwa ukiendelea.
Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada.
Wajumbe kutoka Serikali
ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo.
Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.
Baadhi ya wajumbe kutoka Tume ya Mipango, Klasta ya Biashara ya Kimataifa
na Mahusiano ya Kiuchumi ambao walioshiriki kuratibu majadiliano hayo kutoka kulia Bw.
Robert Senya na Bi. Sudah Lulandala wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano
wakimsiliza Mwenyekiti wa mjadala Dkt. Philip Mpango. Upande wa kulia
ni wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na upande wa
kushoto ni wajumbe kutoka serikali ya Japan.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa pili kulia)
akifungua mkutano wa majadiliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Japan kuhusu ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa mwaka
2014/15. Majadiliano hayo yalifanyika Julai 25, 2014 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na yaliratibiwa
na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Wajumbe wa mkutano uliohusisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakurugenzi na Wataalam wa
Sekta mbalimbali wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea.
(Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango).
No comments:
Post a Comment