Msimamizi wa Uchaguzi Bw. Alfred Kayombo (kulia) akimtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Bw. Ibrahim Ngogo.
Kwa
mara ya kwanza katika historia, chama cha demokrasia na maendeleo
(CHADEMA) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wa uongozi
mbalimbali ambapo Bw. Ibrahim Ngogo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa
chama hicho kwa ngazi ya wilaya.
Na Edwin Moshi, Makete
Akitangaza
matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Alfred Kayombo amesema Bw.
Ibrahim Ngogo amepata kura 25 akifuatiwa na Isaac Sanga aliyepata kura 6
na Shaaban Mkakanze aliyepata kura 1.
Bw.
Kayombo amesema kutokana na umuhimu wa demokrasia ndani ya chama hicho,
wameamua kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza toka chadema iingie
wilayani hapa, hivyo kuonesha kuwajali wanachama wake
Mbali
na viongozi hao wa juu wa chama pia Bw. Lazaro Chaula amechaguliwa kuwa
katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Makete kwa kupata kura 30, Bi. Rose
Mbilinyi amechaguliwa kuwa Mtunza hazina wa wilaya kwa kupata kura 26.
Aidha
Bw. Atukuzwe Mahenge amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana
(BAVICHA) wilaya na Bw. Shadraack Mwachota akichaguliwa kuwa katibu wake
na wote wamepita bila kupingwa.
Bi.
Beatrice Kyando amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa
chadema wilaya (BAWACHA), Bi Christina Timoth akichaguliwa kuwa katibu
wa BAWACHA, na Bi. Mariam Asheli akichaguliwa kuwa Katibu wa
uhamasishaji wa BAWACHA na wote wamepita bila kupingwa.
katika
uchaguzi huo pia Bw. Abiud Elia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza
la wazee kwa kura 3, Abeli Juma Sanga akipata kura 1 na kuchaguliwa kuwa
Makamu mwenyekiti, pamoja na Simon Nyasanga kuwa katibu wa baraza la
wazee wilaya.
Katika
hatua nyingine wamechaguliwa wajumbe 4 waliochaguliwa kuingia kwenye
kamati tendaji ambao ni John Sanga, Patison Pela,Orignal Sanga na Alafat
Msigwa, huku Bw.Illomo Werner Naftal akichaguliwa kuwa mwakilishi wa
wilaya kwenye mkutano mkuu taifa.
Akiahirisha
mkutano huo mwenyekiti wa Chadema wilaya Bw. Ibrahim Ngogo amewasihi
wajumbe kuondoa makundi na kutokubali kutumia kwa ajili ya kukibomoa
chama na badala yake washikamane wawe kitu kimoja kukijenga chama.
"Makamanda
uchaguuzi umeisha haitakiwi tuwe na makundi, tushikamane kukijenga
chama chetu, hilo ndilo la msingi kwa sasa, sisi viongozi mtupe
ushirikiano" amesema Ngogo
No comments:
Post a Comment