TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, July 31, 2014

KAM COLLEGE YAFANA KATIKA MAHAFALI YAKE YA KWANZA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Mkuu wa  KAM COLLEGE, Dr.   K.M  -  Musika (CMLT, DMLT, MD),( WA [wa kwanza kushoto) nuda mfupi baada ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,  ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo (MOHSW) Dr. Otilia F. Gowelle, aliye muwakilisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Stephen Kebwe, wengine katika Picha ni Viongozi waliofuatana na Mgeni Rasmi.
 
 Baadhi ya Majengo ya Chuo cha Kisasa cha Udaktari, KAM COLLEGE , kilichopo Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam, baadhi yao wakiwa ni wanafunzi waliokuwa wakihitimu katika mafunzo ya Clinical officer & Medical Officer, wakijiandaa kuingia katika Sherehe za Mahafali ya Kwanza katika chuo hicho.
Mkuu wa  KAM COLLEGE, Dr.   K.M  -  Musika (CMLT, DMLT, MD) na  Mkurugenzi wa Mafunzo (MOHSW) Dr. Otilia F. Gowelle, kulia, muda mfupi baada ya kuwasili mgeni Rasmi aliyemuwakilisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Stephen Kebwe,

 Baadhi ya Wazazi wakiingia katika Mahafali hayo
 
 Mgeni Rasmi baada ya Kuingia alikwenda Moka kwa moja kufungua jiwe la msingi la Majengo ya chuo hicho.
 
 
 
 Baada ya Ukaguzi wa Majengo Mgeni Rasmi moja kwa moja kwenye Daftari la Wageni Maalumu. kwa ajili ya kuweka uthibitisho wake.
 Baada ya kusaini Daftari la Wageni, alikwenda kwanza kwenye Jukwaa la Wageni kisha kuwasabahi Wahitimu Kabla ya Kuungana nao kwa Mavazi.
 Baadhi ya Wahitimu wakiwa wamesiamama kumlaribisha Mgeni Rasmi

Baada ya kusaini Daftari la Wageni, alikwenda kwanza kwenye Jukwaa la Wageni kisha kuwasabahi Wahitimu Kabla ya Kuungana nao kwa Mavazi.
 Baadhi ya Wageni waliokuwa na Ndugu Zao wakihitimu, wakiwa kwenye Eneo Maalum kwa ajili ya Wageni.
 
 
 
 
 Mzee Musika, ambaye ni Baba wa Familia ya kina Msika, wamiliki wa Chuo cha KAM COLLEGE, pia alitunukiwa Cheti Maalum kutoka kwa Familia ya Watoto wake, kwa Kuwazaa, akionyesha Zawadi yake juu kwa Wandishi pamoja na Umri wa Mzee Msika kuwa Umesonga, lakini alifanikiwa kuinia na kupunga mkono kwa wageni waliokuwa wamejaa katika Ukumbi wa Sherehe wa Chuo hicho, na kupigiwa Vigelegele na Vifijo, ikiwa ni kutokana na Mzee Msika kufika Eneo hilo kwa Kushikiliwa na kutembea na Fimbo, kitendo kilichoitwa Ushupavu na Uvumilivu.
 Mkuu wa  KAM COLLEGE, Dr.   K.M  -  Musika  kati kati akitoa maelekezo kwa mmoja wa wahusika kwenye Chuo hicho wakati wa Kumkaribisha Mgeni Rasmi
 Baadhi ya Wageni wakiingia mfululizo ndani ya ukumbi wa KAM
 
 
 
 
 
Hakika Mahafali haya ya Kwanza katika Chuo cha Afya, KAM COLLEGE, palikuwa hapatoshi kutokana na jinsi ambavyo kwanza watu walivyoitikia kwenda kushuhudia mahafali hayo, ambayo ukiachilia mbali wazazi wa wahitimu, ndugu na jamaa zao, lakini pia mwitikio kwa watu kutaka kuingia, na hata wengi pia walitaka kuzamia kuingia, maana chuo hiki pia ni lazima nikisifie kwa Ubora wake, maana kama huyu Mzee Musika ndiye aliyewapa plani hii ya kufikia hapo, hakika wamejitahidi sana kufikia hatua ya kuwa chuo bora.
kwa mtazamo wangu hii KAM COLLEGE sasa inaweza kuwa pia Chuo Kikuu maana hadhi yake ni ya kimataifa na hata kama kuna wazazi wanapenda watoto wao lipata elimu hii ya Mafunzo ya Udaktari, Uuuguzi, na masuala yanayohusiana nayo, basi wasisite kuwapeleka Vijana wao katika chuo hiki cha KAM cOLLEGE.
Sipo hapa kusifia sana bali hakika panapotakiwa kupewa papewe napasipotakiwa pasiwepo na uraghai, kwanza mijengo ilivyojengwa tu utadhani UDSM, 

Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo, pamoja na Ratiba kuonyesha angefungua saa 4:30 haikuweza kuwa hivyo kutokana na saa zetu za Tanzania(Uswahili), hivyo ilibidi kuanza shuguli saa za saba saba kama siyo nane, Majengo Mazuri lakini Ratiba kwa upande wangu sijui ni mgeni Rasmi au ni uongozi wenyewe, maana burudani ziliendelea muda wote chini yake Supa Star, Abdalah Mwaipaya, ambaye kundi la Viajana wake muda wote walionekana kutawala jukwaa kwa Kamera huku wakituonyesha pia katika Kioo(Projector).

Baada ya Mgeni Rasmi kusikiliza Hotuba za Serikali ya Wanafunzi, ambao kilio chao kikuu ilikuwa ni kuitaka Serikali iwawezeshe na wao kupata Mkopoooooooooo na pia kuitaka Serikali, kwenye Suala la Mitihani basi Wote wao yaani wa Usajili wa NACTE kwenda sambamba na wale wengine yaani wa TCU.

LAKINI pia kuitaka Serikali, mimi naongezea..... kuitaka Serikali, iwaandalie Pia Ajira hawa Madaktari, zijengwe zahanati na Hospitali za kutosha kukidhi ajira zao, wasisome kisha kuishia kuuza dawa kwenye Phamacy tu, chanzo cha upotevu wa Madawa Mahospitalini.

Nimalize kwa kuwashukuru wote waliofanikisha Mahafali ya kwanza ya chuo cha KAM , Ongereni sana Wahitimu wote.
NIPIGIE KAMA KUNA CHA KUNENA NA MIMI@ +255-767-869133

No comments:

Post a Comment