Na: FICHUO Tz
Shirika la kutetea haki za wanyama la Afrika Kusini limeanza uchunguzi
kuhusiana na kifo cha twiga baada ya kuumia wakati akisafirishwa kwenye
gari. Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema twiga mmoja kati ya wawili
waliokuwa kwenye lori, aligonga kichwa chake katika barabara moja mjini
Johannesburg.
Gari
hilo baadaye liliharibika na kulazimika kusubiri kwa saa kadhaa kabla ya
kutengenezwa. Wanyama wote wawili walipelekwa kwa daktari wa wanyama,
lakini shirika la kutetea haki za wanyama la NSPCA limesema twiga mmoja
alikufa.
Tukio hilo limeleta mjadala mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Meneja
wa NSCPA Rick Allen amethibitisha kuwa twiga huyo alipata majeraha ya
kichwani lakini amesema uchunguzi ni muhimu ufanyike kutafuta sababu
hasa ya kifo hicho.
No comments:
Post a Comment