Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi huo .
Furaha ya kuanza kazi Nakumatt Mlimani
Mkurugenzi
Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi
huo
KAMPUNI
ya Nakumatt Holdings, imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi
yake matatu makubwa nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni
ya Shoprite ya Afrika ya Kusini.
Ikiwa
ni mpango wake mpya wa kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings,
imezindua tawi hilo kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma
zake katika eneo la biashara la Mlimani City litakaloitwa Nakumatt
Mlimani.
Tawi
hilo la 48 la Nakumatt limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za
Nakumatt na kwa ubunifu wa hali ya juu. Pamoja na Nakumatt Mlimani,
kampuni hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa litakalojulikana
kama ‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa
makao yake makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo.
Kwa
kufungua matawi yake matatu moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa
imefikisha matawi 50 katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na
hivyo kutekeleza mkakati wake wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka
2011.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi
matatu mapya yaliogharimu takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu
ya mpango wa upanuzi wa huduma za uuzaji bidhaa katika kanda ya Afrika.
Kutokana na uzinduzi wa Tawi la Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa
Nakumatt sasa ina maduka mawili makubwa yanayofanya kazi nchini
Tanzania.
Nakumatt
Mlimani inaungana na duka jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa
mwaka 2011 katika mji huo ambako kuna Mlima Kilimajaro.
”Uzinduzi
wa Nakumatt Mlimani ni ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli
ambapo tumekuwa tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es
salaam na maeneo mengine nchini Tanzania,” alisema Shah na kuongeza:
“Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri itakayopelekea uzinduzi mwingine wa
duka letu la 50 katikati ya Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia
malengo yetu tuliyojiwekea kuyafikia Februari mwakani.” Maduka matatu ya
Shoprite yalifungwa mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha
zaidi sambamba kwa kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt.
Pia Nakumatt inatarajia kufungua matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka huu. Pia
kampuni hiyo itakuwa na duka kubwa katika eneo kubwa la kifahari la
Green Square mjini Kericho nchini Kenya. Shah alisema Nakumatt ina
mkakati wa kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi uwepo wa
vitega uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka
ya supermaketi. Shah aliongeza kwa kusema:
“
Kwa sasa tunaendesha shughuli zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na
wamiliki wa maeneo ya biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma
za kujenga maeneo ya maduka makubwa katika maeneo ya Machakos, Nyeri,
Kajiado, Garissa, Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.”
Ili
kutimiza masharti ya Nakumatt, Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo
ya biashara na Mameneja wa Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt
kuhusu namna ya kuboresha uchoraji wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa
wateja katika maduka ya kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment