Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija
(kushoto) akisisitiza jambo kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la
Mavurunza, Padri Xavery Kassase kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi
milioni 15 kwa Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita kusaidia mradi wa
ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika kanisani
hapo hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase (kulia) kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita hivi karibuni
Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase(kulia) akionyesha hundi ya shilingi milioni 15 zilizotolewa na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mchango huo wa kampuni ulitolewa kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri kanisani hapo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija.

MAENDELEO ya kijamii na kiuchumi yataweza kupatikana endapo
tu kila mtu ataweza kutoa mchango wake kuwasaidia wale wanaohitaji
msaada ili kubadilisha maisha yao na kuwa wachangiaji wakubwa katika
ukuaji wa uchumi wa taifa. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Simon Bulenganija wakati wa harambee ya
kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri katika Kigango cha kanisa la
Mtakatifu Rita lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, ambapo UDA
ilichangia shilingi milioni 15.
“Watanzania wasisubiri mpaka makampuni makubwa yajitokeze
na kutusaidia kubadilisha hali zetu za kiuchumi na mfumo wetu wa maisha.
Mabadiliko yataweza kufikiwa tu endapo kila mmoja wetu ataweza
kuchangia kwa nafasi yake kikamilifu. Makampuni yote makubwa na madogo
na watu binafsi wenye uwezo wa kusaidia, wawashike mkono wale
wanaohitaji msaada ili tuweze kuendelea pamoja,” alisema. Bw. Simon Bulenganija alisema kuwa kampuni yake imekuwa
ikijihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni jitihada
madhubuti zinazolenga katika upatikanaji wa maendeleo miongoni mwa
watanzania wote.
Alisema kuwa shilingi milioni 15 zilizotolewa na UDA
zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga jeki maendeleo ya kanisa hilo
hususani katika ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na mradi
wa ujenzi wa kanisa jipya.“Japokuwa bado kampuni yetu ni kampuni changa ya
kitanzania, tumeunda programu yetu ya shughuli za kijamii katika namna
ya kwamba shughuli tunazojihusisha nazo, zitasaidia katika kutekeleza
ajenda yetu yenye kaulimbiu “ukuaji wa kampuni yetu uwe sambamba na
ukuaji wa kiuchumi wa jamii yetu”. Hii pia ni njia pekee ya kurudisha
sehemu ya pato letu kwa jamii,” alisema Bw. Bulenganija.
Naye, Bw. Frederick Msumali, Mwenyekiti wa Kigango cha
Mtakatifu Rita, aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake na ushiriki wa
Mkurugenzi wa UDA wakati wa shughuli hiyo ya harambee ambayo iliwezesha
kanisa hilo kukusanya zaidi ya shilingi milioni 60 zitakazotumika
katika mradi huo.
“Tungependa kwa kiasi kikubwa kutoa shukrani zetu kwa
mchango uliotolewa na UDA. Msaada huu kwa kiasi kikubwa utasaidia
kupiga jeki mradi wetu wa ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae
kuendelea na ujenzi wa kanisa jipya utakaofanyika karibu na kanisa hili
la sasa. “Lakini pia, tunaishukuru UDA kama kampuni na Bw.
Bulenganija mwenyewe kwa kuwa mgeni wetu rasmi. Mfano huu unahitaji
kuigwa na makampuni mengine nchini,” alisema Bw. Msumali.
No comments:
Post a Comment