Usiku wa kuamkia leo, muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama kwenye huduma.
Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku
kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa awali zimeshindikana, kutokana na
kushindwa kugeuka wala kuinuka - akiwa amelazwa.
Frank amesafishwa kichwa na anaendelea vema. Muujiza wake ni kwamba nguo aliyokuwa amevaa ilichanwa na vioo, lakini yeye mwenyewe hajachubuka kutokana na vioo hivyo. |
Tayari ndugu na marafiki walishafika
kutoka Dar es Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita
kuwajulia hali na kuwafariji.
Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU
(31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na
kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine
linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema
ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara
kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.
Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za
vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za
injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER
(20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam
ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote
wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao
zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar
es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU
na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la
Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
Jennifer Mgendi (kushoto) akimjulia hali rafiki yake, Bahati. |
No comments:
Post a Comment