Amenukuliwa akisema >>> ‘January
anafanya kazi nzuri ya ubunge pia ananisaidia sana kwa kazi ya wizara
niliyompa, unajua January alipogombea Ubunge alinificha nilikuwa nasikia
kwa wenzake tu pale ofisini, baadae alivyoweka mambo yake sawa ndio
akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa’
‘Nikamtakia heri… kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake
inaonyesha Ubunge aliutaka kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli,
nimesikia anafikiria mambo makubwa… hajaniambia mi nimesikia tu,
namtakia kila la heri…. haya mambo anaamua Mungu wala hayalazimishwi’

‘Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki, Mungu akiwa
hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa, mimi
nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata
hata kama utapingwa kiasi gani, kama halijafika wakati wake haliwezi
kutokea, mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake….
2005 ikawa wakati wake nikapata, na wewe usipopata sasa usiweke nongwa” –
JK
Hapa chini kuna video ya dakika 3 ikionyesha sehemu ya kazi zake Naibu waziri huyu ambae pia ni Mbunge wa Bumbuli kupitia CCM.
No comments:
Post a Comment