Serikali
imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia
(IMTU), baada ya kuifanyia ukaguzi na kubaini kasoro kadhaa za
uendeshaji wake.
Ukaguzi
huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya
utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hospitali hiyo imefungiwa wakati Kamati ya Watu 15, iliyoundwa na Serikali ikiendelea kuchunguza kashfa hiyo.
Hata
hivyo, wakati taarifa za kufungiwa zikitolewa habari za ndani
zinaonyesha kuwa hapakuwa na mgonjwa yeyote hospitalini hapo, ikielezwa
kuwa wagonjwa wote waliondoka baada ya kuibuka kwa kashfa ya viungo IMTU
ikihusishwa.
Mganga
Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Bunini Kamba alisema kuwa wameamua
kuifungia hospitali hiyo kwa muda usiojulikana, baada ya kukuta upungufu
mbalimbali katika maeneo ya kutolea huduma, jambo linalohatarisha
usalama wa wagonjwa.
"Maabara
tumekuta dawa ambazo muda wake wa kutumika umepita na hazikuwa katika
mpangilio maalumu. Wodini hakuna usimamizi maalumu, hasa kwa wagonjwa
wenye majeraha," alisema Dk Bunini.
Aliongeza:
"Hakuna wauguzi wa kutosha na mashine ya kuchoma taka ngumu haifanyi
kazi vilivyo. Tumeona kuwa hospitali hii haistahili kuendelea kutoa
huduma kwa jamii."
Mkurugenzi
wa Hospitali hiyo, Profesa Yasin Mgonda alisema: "Tumesikia uamuzi huo
uliotolewa baada ya kufanyika ukaguzi. Tutajirekebisha na
tutakapokamilisha tutawaita kuja kutukagua tena."
Alisema
kuwa pamoja na sababu nyingine, hospitali yake imefungiwa baada ya
kubainika kuwa bomba la maabara limeharibika na halitoi maji.
Nyingine
ni kutojaza vitabu vya wagonjwa kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, pia duka lake la dawa kuwa halijasajiliwa lakini
akasema sababu hiyo imewashangaza kwani wanachojua wao duka hilo
limesajiliwa.
Kwa
upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus
Saidia aliliambia gazeti hili kwamba anaipongeza Serikali kwa uamuzi huo
akisema utanusuru maisha ya wananchi waliokuwa wakipata huduma
hospitalini hapo.
"Tunaipongeza Serikali, ila tunaiomba iwatafutie wanafunzi wa chuo hicho maeneo mengine ya kujifunzia," alisema Dk Saidia.
Juzi, Dk
Saidia alisema kuwa wote waliohusika na kashfa ya utupaji mabaki ya
viungo vya binadamu wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu
kitendo hicho kimekiuka sheria, taratibu, haki za binadamu, maadili ya
ufundishaji na taaluma ya udaktari.
"Kama ni
taasisi ya utafiti imepoteza sifa ya kufanya utafiti na kama ni ya
mafunzo basi imepoteza sifa ya kutoa mafunzo ya tiba. Kama ni hospitali
itakuwa imepoteza sifa za kutoa tiba kwa binadamu," alisema Dk Saidia.
Naye
spika wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho (IMTUSO), William Mapunga
alisema kuwa kufungiwa kwa hospitali hiyo kutawaathiri, kwani watakosa
sehemu ya kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo, akiiomba Serikali
kuliangalia suala hilo kwa mapana.
Chanzo:Mwananchi

No comments:
Post a Comment