MWIMBAJI
mahiri wa muziki wa Injili, Rose Muhando amelalamika kuwa albamu yake
ya Kamata Pindo la Yesu Albamu anayotarajia kuizindua Jumapili wiki hii
imeingizwa mtaani na wezi wa kazi za wasanii, hivyo kuonya wananchi wawe
makini kwani albamu yake halisi itatoka Jumapili.
Taarifa
kwa vyombo vya habari aliyoitoa Muhando jana, ilieleza kuwa albamu yake
halisi bado haijaingia mtaani na kwamba hiyo wanayoiona wananchi sasa
ni bandia na mtu atakayewauzia wamripoti polisi.
“Albamu
ya Kamata Pindo la Yesu itaanza kuingia mtaani baada ya uzinduzi wangu
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumapili wiki hii. Albamu yangu ina
nembo ya TRA (Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini).
“Hizi
CD zinazouzwa hivi sasa si zangu, hao ni matapeli na nawaomba wananchi
tushirikiane kudhibiti wizi. Hao ni maharamia wa kazi za wasanii
wanataka kunyonyajasho langu, naomba sana wananchi mnisaidie.“Nasisitiza
albamu yangu sijaiachia sokoni bado mpaka uzinduzi ukamilike,
Watanzania wenzangu na mashabiki wangu kote duniani mnielewe na naomba
tusaidiane katika hili maana CD feki zimezagaa,” alisema Muhando na
kuongez akuwa tayari ameripoti taarifa hiyo kwa vyombo vya dola.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoratibu
uzinduzi huo, Alex msama naye katika taarifa hiyo ya pamoja alionya wote
watakaobanika kuwa CD za albamu ya Rose Muhando watakumbana na mkono wa
sheria.
“Inasikitisha
sana kuona baadhi ya watu wanataka kutumia jasho la wengine
kujinufaisha. Watanzania kuweni macho, msubiri albamu yenyewe ya Rose
Muhando Jumapili pale ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,” alisema
Msama.
Albamu
hiyo ya Muhando itakayozinduliwa Jumapili ina nyimbo za Bwana Niongoze,
Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu
na Facebook.
Hivi
sasa Rose anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu, ambapo pia amewahi
kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi),
Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo
No comments:
Post a Comment