Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014
ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili
kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma.
Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali
Omar, Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania
(TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na
Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment