Hoteli ya Singita Grumeti Reserves.
HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania,
Matokeo
hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha
matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo
linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure.
Tangu
kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi,
matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari,
vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa
mujibu wa US Travel + Leisure, sababu ya kuipa Singita hadhi ya kuwa
hoteli namba moja duniani, inatokana na muundo wake, huduma
zinazotolewa, kuwa ndani ya mbuga kubwa kabisa ya wanyama duniani
(Serengeti), vilevile wageni mashuhuri inaopokea.
Inaelezwa
kwamba Singita Grumeti ndiyo hoteli inayoongoza kwa sasa duniani kwa
kupokea wageni wenye hadhi ya daraja la kwanza, wakiwemo marais,
matajiri, wanamichezo, wasanii, viongozi mbalimbali maarufu ulimwenguni
na kadhalika.
HAWA WANATAJWA KUJIVINJARI SINGITA
Marais wa
42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa nyakati
tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa zake
zinazotikisa duniani.
Bilionea
wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich,
alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye
hoteli hiyo.
Bilionea
wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani,
alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Wakati
alipowasili nchini, Mekesh alikuwa tajiri namba nne duniani. Ripoti ya
mwaka 2011, ilimtaja kuwa tajiri namba tisa na sasa anashika nafasi ya
19.
Mke wa
zamani wa mwanasoka anayechezea Chelsea ya England, Ashley Cole, Cheryl,
alipofika nchini miaka miwili iliyopita, inaelezwa pia kwamba alifikia
kwenye hoteli hiyo.
Mwanamitindo
aliye pia mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Marekani, Angelina Jolie
na mumewe Brad Pitt, waliripotiwa kufika nchini na moja kwa moja makazi
yao yakawa Singita Grumeti.
Wengine
ambao wanatajwa kuwahi kupumzika kwenye hoteli hiyo ni mwanamuziki wa
Marekani, Sean Carter ‘Jay Z’, mwanasoka Thierry Henry, Rais Jakaya
Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Hata
hivyo, inaelezwa kuwa orodha ya wageni wanaofikia Singita ni kubwa mno,
tatizo hufanywa siri kwa sababu watu wengi mashuhuri ulimwenguni huwa
hawapendi ijulikane kama wamefikia kwenye hoteli hiyo kwa sababu za
kiusalama.
SIFA ZA HOTELI HIYO
Ni hoteli yenye eneo kubwa, kutoka ‘loji’ moja hadi nyingine, inabidi utumie usafiri maalum.
Imegawanywa kwenye ‘loji’ mbili, moja inaitwa Ebony na nyingine ni Boulder.
Hoteli
hiyo, pia inaundwa na ‘loji’ nyingine inayoitwa Castleton Camp ambayo
inaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Bei ya chini kabisa kwa mtu kulala kwenye hoteli hiyo ni shilingi 2,000,000 na bei hiyo hutegemea na msimu.
Bei
zimetofautiana kati ya ‘loji’ moja hadi nyingine na mtu kulala kwenye
Castleton Camp, inaweza kugharimu mpaka shilingi milioni 23 kwa siku
moja.
Singita Grumeti ni moja kati ya hoteli za Singita za nchini Afrika Kusini
No comments:
Post a Comment