Viungo vya Binadamu ambayo hutumika kufundishia madaktari.
Dar es Salaam.
Wakati sakata la kuokotwa kwa viungo vya
binadamu likiendelea kutikisa nchi, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kimesema kuwa hutumia maiti 25 kwa
kuwafundishia wanafunzi kila mwaka.
Pia chuo hicho
hakijawahi kuagiza maiti kutoka nje ya nchi na kwamba ni mtu mmoja tu
aliyewahi kutaka maiti ya mtoto wake itumike kufundishia.
Kauli
hiyo ya MUHAS imekuja siku chache baada ya Serikali kuamua kuifungia
Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU),
baada ya kubaini kasoro kadhaa katika utendaji wake.
Juzi,
Serikali ilifanya ukaguzi wa kushtukiza IMTU, baada ya hospitali hiyo
kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika
Bonde la Mto Mpiji, jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki iliyopita.
KWA TAARIFA ZAIDI BOFYA HAPA.
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com
No comments:
Post a Comment