Yanga wameamua, Maximo hataki kubahatisha
Wachezaji wa timu ya Yanga wakiwa mazoezini. Picha na Michael Matemanga |
Katika makabrasha ya Mbrazili huyo kila siku
anaingiza jina au kulifuta jingine katika nafasi za uwanjani na anafanya
hivyo kutokana na viwango vya
YANGA kweli wameamua. Kocha Marcio Maximo ‘The
Chosen One’ hataki kubahatisha na kuanzia sasa kila nafasi katika kikosi
chake itakuwa ina watu wa uhakika wasiopungua watatu.
Katika makabrasha ya Mbrazili huyo kila siku
anaingiza jina au kulifuta jingine katika nafasi za uwanjani na anafanya
hivyo kutokana na viwango vya
wachezaji wake mazoezini. Anayepungua anafutwa
katika orodha na ambaye kiwango kinapanda anaingizwa jina. Kocha huyo
anayafanya hayo kuhakikisha anakuwa na kikosi imara chenye ushindani
uwanjani.
Mwanaspoti lina uhakika na mpango huo wa Maximo
ambao utamwezesha kuwa na kikosi imara cha ushindani ambacho kitaweza
kupigania pointi tatu katika kila mechi watakayocheza pale pazia la Ligi
Kuu Bara litakapofunguliwa.
Tangu alipoanza kuifundisha Yanga Julai Mosi,
kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, amekuwa akiwatazama
kwa makini wachezaji wote na kuandika majina yao kitabuni pia
akifuatilia taarifa za wachezaji wake walio katika timu za taifa; Taifa
Stars, Rwanda na Uganda.
Akianzia golini, Maximo katika kabrasha lake amepanga namba moja ni Deo
Munishi ‘Dida’, anafuata Juma Kaseja halafu Ally Mustapha ‘Barthez’ na kinda Said Ally wa kikosi B amewekwa namba nne.
Nafasi nyingine yenye idadi ya wachezaji wanne
huku anayetakiwa kucheza akiwa mmoja ni ile ya ushambuliaji ambayo wapo
Genilson Santana ‘Jaja’,
Jerry Tegete, Said Bahanuzi na Hussein Javu. Jaja ndiye wa kwanza hapo.
Katika beki ya kulia, Maximo anao Juma Abdul na
Salum Telela huku anayeanza akiwa Abdul. Katikati wapo Kelvin Yondani,
Pato Ngonyani na Issa
Ngao kutoka Yanga B kama mabeki wa mwisho huku
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Rajab Zahir wakiwa mabeki wa kati wakabaji.
Hapo wanaoanza ni Yondani na Cannavaro.
Beki ya kushoto ndipo kuna dosari kidogo kwani Maximo anaye Oscar Joshua na kinda Amos Abel anayetoka kikosi B.
No comments:
Post a Comment