=================================================
Fabiano mshindi wa medali ya fedha ya mita 10,000
kwenye michezo hiyo mwaka 2006 nchini Australia alikuwa tegemeo la
Tanzania, lakini alishika nafasi ya 11 huku Mtanzania mwingine John
Leonard akiishia njiani.
NYOTA ya Tanzania katika michezo ya Jumuiya ya
Madola inayoendelea huko Glasgow, Scotland imeendelea kufifia baada ya
jana Jumapili mwanariadha tegemeo Fabiano Joseph (pichani) kushindwa
kwenye marathoni.
Fabiano mshindi wa medali ya fedha ya mita 10,000
kwenye michezo hiyo mwaka 2006 nchini Australia alikuwa tegemeo la
Tanzania, lakini alishika nafasi ya 11 huku Mtanzania mwingine John
Leonard akiishia njiani.
Kushindwa kwa Fabiano ni mwendelezo wa wanamichezo
wa Tanzania kwenye michezo hiyo kuondoshwa mapema ambapo tayari, baadhi
ya mabondia, waogeleaji na timu ya mpira wa meza wameaga michezo hiyo.
Fabiano alitumia muda wa 2:15.21 kumaliza mbio
hizo, wakati mshindi Michael Shelley wa Australia alitumia muda wa
2:11.15 na Stephen Chemlany wa Kenya alikuwa wa pili akitumia 2:11.58
huku Mganda, Abraham Kiplimo alikimbia kwa 2:12:23. Wakati huohuo, juzi
jioni, bondia Nasser Mafuru aliondoshwa kwenye michezo hiyo na kuungana
na Seleman Kidunda aliyeugua tumbo na kushindwa kupigana.
No comments:
Post a Comment