By KHATIMU NAHEKA
-====================================
Kwa kushirikiana na Makamu wake, Clement Sanga,
Manji ameunda kamati hiyo kwa mamlaka aliyonayo kupitia azimio la
Mkutano Mkuu uliofanyika Januari 20 ambao ulimpa madaraka ya kufanya
mabadiliko ya kamati ya utendaji atakavyojisikia.
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amevunja
Kamati ya Utendaji na mara moja ameitangaza kamati mpya ambayo haina
jina la Abdallah Bin Kleb.
Kwa kushirikiana na Makamu wake, Clement Sanga,
Manji ameunda kamati hiyo kwa mamlaka aliyonayo kupitia azimio la
Mkutano Mkuu uliofanyika Januari 20 ambao ulimpa madaraka ya kufanya
mabadiliko ya kamati ya utendaji atakavyojisikia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Manji iliyosomwa na
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, kamati mpya itaanza kazi Agosti Mosi
ambapo kila mjumbe aliyeteuliwa amepewa kazi maalumu za kusimamia. Ni
tofauti na ilivyokuwa katika kamati aliyoivunja.
Wajumbe wa kamati mpya ni Abubakar Rajabu ambaye
amepewa kazi ya kusimamia mradi wa ujenzi wa Jangwani City, Salum
Mapande (Sheria na Utawala Bora),George Fumbuka (Uundwaji wa shirika) na
Abbas Tarimba (Mipango ya Uratibu).
Wengine ni Isaac Chanji na Seif Ahmed ‘Seif
Magari’ (Uendelezaji wa Michezo), Musa Katabaro (Mauzo na Biashara),
Mohamed Bhinda (Ustawishaji matawi), David Sekione ‘Seki’ (Uongezaji
Wanachama) na Mohamed Nyenge (Utangazaji wa Habari, Taarifa na
Matangazo).
Wakati huohuo, kamati mpya iliyotangazwa haina
jina la Bin Kleb ambaye awali alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili,
lakini mwenyewe amesema aliomba kutojumuishwa kwenye kamati mpya.
Mmoja wa mabosi wa Yanga, alisema Bin Kleb ameomba kupumzika ili aweze kushughulikia mambo yake binafsi.
“Si kwamba Mwenyekiti ana tatizo na Bin Kleb,
walizungumza kwa muda mrefu na kukubaliana apumzike. Bin Kleb ndiye
aliyeomba apumzike,” alisema bosi huyo.
No comments:
Post a Comment