Kiongozi
wa Mbio za Mwenge kitaifa Bi Rachel Kasanda akikabidhi mashine za
kufyatulia matofali kwa Hassan Soud Katibu wa kikundi cha Changamoto kwa
niaba ya vikundi vingine vya wilaya ya Ilala ambazo zimetolewa na
shirika la Nyumba nchini NHC jana wakati wa mpokezi ya Mwenge wa Uhuru
Ilala Boma mara baada ya Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Ilala Bw.
Jackson Maagi kumkabidhi kiongozi huyo wa mbio za mwenge ikiwa ni juhudi
za shirika hilo kusaidia kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana ili waweze
kujiajiri kwa kuyatua matofali na kuuza.
Askari wa Kikosi cha FFU wakiulinda mwenge mara baada ya kuwasili Ilala Boma mahali ambapo ndiyo kituo ulipolala mwenge huo.
Meneja
wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi wa pili kutoka
kushoto akiwa pamoja na wafanyakazi wnzake kabla ya kukabidhi mashinne
hizo jana.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo jana
=========================================
HOTUBA FUPI YA MENEJA WA NHC ILALA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA
Ndugu kiongozi wa Mbio za mwenge,
Ninayo furaha kubwa sana kusimama mbele yenu na kuongea nanyi kama mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
Ndugu
Kiongozi wa Mbio za Mwenge; Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango
mkakati wake wa miaka mitano ambao moja ya malengo yake sita makuu ni
kuboresha taswira ya Shirika.
Katika utekelezaji wa lengo hili, Shirika lina sera ya huduma kwa
jamii ambayo imejikita katika kusaidia vijana kujiajiri. Ili kuwezesha
vijana kujiajiri, Shirika limeamua kuzisaidia Halmashauri za Miji na
Wilaya kote nchini mashine za kuwezesha vikundi vya vijana kutengeneza
matofali ya kujengea nyumba. Nchi yetu ina Halmashauri 160 na kila
Halmashauri itapewa mashine 4 kwa ajili ya kusaidia vikundi vya vijana.
Katika mpango huu jumla ya mashine 640 zitatolewa na Shirika na
kugharimu shilingi 288,000,000/.
Aidha, kila Halmashauri itapatiwa shilingi laki tano (500,000/=) kama
mtaji kwa vijana kuanzia shughuli yao ya kutengeneza matofali.
Kadhalika, Shirika limegharamia shilingi 800,000/= kwa kila Halmashauri
kwa ajili ya kuwalipa wakufunzi kutoka VETA wanaotoa maelekezo kwa
vijana namna ya kutumia mashine hizo.
Ndugu
Kiongozi wa Mbio za Mwenge,katika kutekeleza mradi huu jumla ya
shilingi milioni mia saba (700,000,000/=) zitatumika. Aidha, tunatarajia
kuwa ajira zaidi ya 8,000 za moja kwa moja na ajira nyingine zaidi ya
200,000 zisizo za moja kwa moja zitapatikana.
Katika mpango huu kila Wilaya inatakiwa kuwa na vijana 40 watakaokuwa
katika vikundi vya watu 10 kila kimoja. Msaada huu ni mkubwa lakini
kutokana na ukubwa wa tatizo la ajira jitihada zaidi kutoka kwa wadau
mbalimbali zinatakiwa.
Ni matarajio yetu kuwa taasisi nyingine ama mtu mmoja mmoja atashiriki kukwamua vijana hawa.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, kupitia maadhimisho haya, Shirika
linatoa mashine nne (4) kwa vikundi 4 vya vijana vilivyoundwa katika
wilaya ya Ilala ambapo kila kikundi kina jumla ya vijana10 watakaotumia
mashine moja. Hivyo jumla ya vijana 40 katika Wilaya hii watapata ajira
kutokana na mashine hizi.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, mwisho Shirika linatoa rai kwa
Taasisi za serikali, mashirika ya umma, binafsi na watu mbalimbali,
kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza tatizo la ajira kwa
vijana.
Ni
matumaini yetu kuwa tutawaunga mkono kwa kununua matofali yao ama
kusaidia upatikanaji wa mashine nyingine zaidi ili wengine ambao
hawajafikiwa na mradi huu wafikiwe na wapate kufaidika.
Kipekee tunaomba Serikali za Mitaa (kwa maana ya Halmashauri zetu za
wilaya, miji, manispaa ama jiji) wawe ni wanunuzi wakuu wa matofali
yatakayotengenezwa na vikundi hivi vya vijana ambayo ni ya gharama nafuu
ili kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi na kuwaongezea kipato chao.
Tunawaomba pia msaidie kusimamia mradi huu ili uweze kuwa endelevu.
No comments:
Post a Comment