Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira jana imekamilisha ziara yake
kwa kukagua mgodi wa Buzwagi na kuridhishwa na utekelezaji wa maagizo
yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na usimimamizi wa Mazingira
(NEMC) kwa mgodi huo.Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele
ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Wa kwanza kulia ni
Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana
wajumbe wa Kamati katika ziara ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji
katika mgodi wa Buzwagi.
Pichani
ni ujenzi wa awamu ya pili wa Kituo cha Afya cha Mwendakulima
kinachojengwa na Mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kuwasogezea wananchi
huduma bora za afya.
No comments:
Post a Comment