Rais Kikwete afungua Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano
la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya tutmishi wa Umma lililofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam . Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano
la Maadhimisho ya miaka 10 ya Tume ya tutmishi wa Umma lililofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam . Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
Kongamano la Maadhimiso ya miaka 10 ya tume ya Umma lililofanyika jijini
Dar es Salaam.Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) pamoja na makatibu wakuu
Kiongozi wastaafu Matern Lumbanga(kulia) na Philemon
Luhanjo(kushoto)(picha na Freddy Maro)
========================================================================
Viongozi wa Msondo wamtembelea Rais Kikwete Ikulu
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa Bendi ya Msondo
ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao walimtembelea
Rais Kikwete ikulu na kufanya naye mazungumzo(picha na Freddy Maro). Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Bendi
ya Msondo ngoma ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Viongozi hao
walimtembelea Rais Kikwete ikulu na kufanya naye mazungumzo(picha na
Freddy Maro).
===================================================================
PINDA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO OMAN
Waziri
Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman
akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014. Kulia ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi
nakushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu) Baadhi
ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29,
2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) Baadhi
ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29,
2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) Baadhi
ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29,
2014.
(Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) Waziri
Mkuu, Mizengo pinda akizunguma na Watanzania waishio nchini Oman
akihitimisha ziara yake nchini humo Oktoba 29, 2014.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
===============================================================
Tigo na Facebook kutoa huduma za internet bure kupitia Internet.org
- Inatarajia kuongeza idadi ya watumiaji wa intenet nchini
- Upatikanaji wa intanet kupitia simu za ‘smartphone’ za bei nafuu kutoka Tigo
- Upatikanaji wa intanet kupitia simu za ‘smartphone’ za bei nafuu kutoka Tigo
Tigo jana imetangaza kwamba
watashirikiana na kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook kuwapatia
mamilioni ya Watanzania huduma ya intanet kwa bei nafuu kupitia
‘application’ maalum ya Internet.org.
Tigo pia inatoa fursa ya wateja
kununua na kumiliki simu za kisasa ‘smartphones’ kwa bei nafuu,
kuwapatia huduma bora ya intanet na kutoa huduma ya bure kabisa kwa
tovuti zinazohusiana na elimu, afya, habari na mitandao ya kijamii
kupitia Internet.org.
App ya Internet.org itaanza
kutumika kuanzia 29 Oktoba na itawapatia wateja wa Tigo fursa ya kutumia
tovuti na apps kama: AccuWeather; BabyCenter & MAMA; BBC News &
BBC Swahili; BrighterMonday; The Citizen; Facebook; Facts for Life; The
Girl Effect; Messenger; Mwananchi; Mwanaspoti; OLX; Shule Direct;
SuperSport; Tanzania Today and Wikipedia.
Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa
huduma hizo leo, Mkuu wa Idara ya Data na Vifaa vinavyotumia Intanet,
David Zacharia, alisema, “Kupitia ushirikiano huu na Facebook
tunadhamiria kuongeza wigo wa matumizi ya kidijitali nchini kwa
kuwahamasisha Watanzania wengi zaidi kuingia mtandaoni.”
Zacharia aliendelea kusema kwamba
ushirikiano huo kati ya Tigo na Facebook itazidi kuendeleza matumizi ya
intanet nchini lakini pia itasaidia kufungua milango mipya ya fursa za
kiuchumi na kijamii kwa walio katika sekta mbali mbali za elimu,
teknolojia, sanaa na biashara.
Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) inaeleza kwamba watumiaji wa intanet nchini Tanzania
imeongezeka kutoka milioni 7.5 mwaka 2012 mpaka milioni 9.3 mwezi wa
Juni 2014 ambayo ni sawa sawa na ongezeko la asilimia 18.
Tigo, kupitia mmiliki wake
Millicom, tayari wana ushirikiano na Facebook nchini Tanzania na
Paraguay ambayo inawapatia wateja wake matumizi ya bure kabisa katika
mtandao huo wa kijamii.
“Leo tunapanua ushirikiano wetu na
Tigo nchini Tanzania kutoka katika kutoa huduma za bure kupitia mtandao
wetu wa Facebook na kujumuisha huduma za kupata taarifa muhimu kwenye
sekta ya afya, elimu, mawasiliano, uchumi, ajira na habari za kitaifa.
Kwa kuwapatia Watanzania teknolojia na huduma hizo kwa gharama nafuu
tunaamini ya kwamba tunaweza tukaharakisha mchakato wa kuwaunganisha
kila mtu katika ulimwengu wa intanet na dijitali,” alisema Meneja Bidhaa
wa Internet.org kutoka Facebook, Andrew Bocking.
Wateja wa Tigo nchini wanaweza wakapata app ya Internet.org kupitia huduma ya Google Play Store, kwa kutembelea www.internet.org
kupitia simu zao za mkononi, kupitia ‘Tigo Portal’ na pia kupitia
‘bookmark’ iliyopo katika huduma ya kuperuzi ya Opera Mini. Huduma hii
inaweza ikatumika kupitia simu za kisasa ‘smartphones’ au simu za
kawaida pia.
Internet.org ni mpango maalum
uliobuniwa na Facebook yenye lengo la kuwapatia huduma za intanet yenye
gharama nafuu kwa theluti tatu ya watu duniani ambao bado
hawajaunganishwa na intanet ili kuweza kuwapatia fursa zile zile ambazo
theluthi ya watu duniani iliyobaki wanaendelea kupata.
App ya Internet.org inafanya
mtandao wa intanet kuwafikia watu wengi zaidi kupitia kundi la huduma za
bure ambazo zinawezesha watu kuperuzi taarifa na tovuti mbali mbali
zenye msaada kwao bila kuingia gharama yeyote.
=================================================================
KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YAENDELEA NA UKAGUZI KATIKA MIGODI
Kamati
ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira imeendelea na ukaguzi katika
Migodi ya dhahabu kufahamu utekelezaji wa Sheri a ya Mazingira. Katika
Mgodi wa Bulyanhulu Kamati iliangalia jinsi maji yenye kemikali
yanavyohifadhiwa na udhibiti wa taka za plastiki mgodini hapo. Migodi
iliyotembelewa mpaka sasa ni Mgodi wa North Mara, Geita na Bulyanhulu.
Hii leo Kamati hii itaendelea na ziara yake katika mgodi wa Buzwagi.Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kulia)
akitoa ufafanuzi wa kisheria mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira. Kamati hiyo iko katika ziara ya kikazi kukagua
utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi. Wengine katika picha
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mh. James Lembeli (wa tatu kulia), Mh.
John Mnyika na Mh. Henry Shekifu wajumbe wa Kamati hiyo. Wa kwanza
(kushoto) ni Bw. Peter Burger, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Pichani ni taka za plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa Bulyanhulu.
Wajumbe
wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha
ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika
Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
Wajumbe
wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha
ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi
katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
==================================================================
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA YASSINI HEZRON (14) MKAZI WA KIWIRA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA
YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.235 AFB AINA YA M/CANTER LILILOKUWA
LIMEBEBA MATOFALI LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE FREDY MPONDO KUSHINDWA
KUPANDA MLIMA NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUANGUSHA MATOFALI NA KUSABABISHA
KIFO KWA TINGO HUYO.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE
29.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MAENEO YA NEW LAND BAR, KATA
YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA TUKUYU/KYELA. CHANZO CHA AJALI NI GARI HILO KUSHINDWA
KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO
HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. OTHAZ ANGOLILE
(18) 2. SAMSON MWANGOMILE (46) 3. FORD SAMSON (20) NA 4. BARAKA JOSEPH
(23) WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS NA RIDDER PAKETI 108.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI
HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO NA TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA/KUUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
===========================================================
KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA BWAWA LA KUZALISHA UMEME MEROWE
Waziri
wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Prof. Peter Msolla wakiwa kwenye
kiwanda cha nyama ya kuku wakiangalia utendaji na uendeshaji wake.
Mjumbe wa Kamati, Prof. David Mwakyusa akiangalia moja ya kifaa cha kisasa katika Hospitali ya Mji wa Merowe.
Ujumbe wa Tanzania ukisikiliza taarifa ya Mji wa Merowe kutoka kwa Inj. Mohamed Elsheikh. Mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Merowe Ujumbe
wa Tanzania, viongozi wa Sudan na wataalam mbalimbali wa Bwawa la
kuzalisha umeme la Merowe wakiwa katika picha ya pamoja katika bwawa
hilo.
……………………………………………
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea
Bwawa la Kuzalisha Umeme la Merowe katika Mji wa Merowe na kujionea
namna ya wenyeji wanavyotumia maji ya Mto Nile kwa kuzalisha umeme wa
kutosha kwa ajili ya mji huo na nchi nzima ya Sudan.
Mradi wa Bwawa la Merowe ni mkubwa
katika nchi ya Sudan na mbali na kuzalisha umeme, pia unatumika kwa
shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa aslimia mia kinategemea
Mto Nile.
Aidha, mradi wa bwawa hilo pia
umechangia kuleta maendeleo makubwa kiuchumi kwa kuwezesha kujengwa kwa
uwanja bora wa ndege wa kisasa, hospitali bora ya kisasa na kiwanda
kikubwa cha nyama ya kuku katika mji wa Merowe.
Hivyo, kuonyesha jinsi gani nchi
ya Sudan inavyotumia fursa ya maji ya Mto Nile vizuri katika kuleta
maendeleo ya Sekta zote nchini mwao.
Hii ni muendelezo wa ziara ya siku
nne nchini humo kwa kamati hiyo, katika kujifunza namna ya kutumia
vizuri rasilimali ya maji ya Mto Nile katika kukuza maendeleo ya nchi.
===================================================================
Serikali yashauriwa kuwekeza katika sekta ya Filamu
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo
akiowaonyesha mabango ya filamu za Tanzania wageni kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Kenya (hawapo pichani) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo ili
kujifunza namna ya Uendeshwaji wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Silyvester
Sengerema.
Kutoka
kushoto ni Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA)
Bi. Jacquline Kinyanjui, Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
Kenya Bi. Mercy Tepla na Afisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Bw. George Charles wakisikiliza maelezo kutoka kwa uongozi wa
Bodi ya Filamu Tanzania walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini
Dar es Salaam.
Ujumbe
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya wakiwa katika kikao cha pamoja na
Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wa pili kutoka kushoto
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Kenya walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini Dar es
Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM
==========================================================
PSPF YAKABIDHI MABATI 300 KWA WILAYA ZA KILOLO NA MUFINDI
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald
Guninita akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa mwakilishi wa PSPF
kutoka makao makuu Amelia Rwemamu kwa ajili ya ujenzi wa maabara za
sayansi katika shule za sekondari wilayani humo, Makabidhiano
yalifanyika juzi katika ofisi za wilaya ya Kilolo(picha na Denis Mlowe)
……………………………………………………………………
Na Denis Mlowe,Mufindi
KATIKA kutekeleza maagizo ya
Rais Jakaya Kikwete kila shule iwe na maabara tatu ifikapo Novemba mwaka
huu Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPSF) umetoa msaada wa
mabati 300 yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni sita katika wilaya za
Kilolo na Mufindi, mkoani Iringa kufanikisha ujenzi wa maabara hizo na
hosteli kwa chuo cha Ualimu Mufindi.
Wakati wilaya ya Kilolo imepata
bati 200 zitakazotumika kusaidia kukamilisha ujenzi wa maabara
unaoendelea katika shule zake za sekondari, Chuo cha Ualimu
Mufundi(MUTCO) kilichopo mjini Mafinga wilayani Mufindi kimepata bati
100 ikiwa ni kutumiza ahadi iliyotolewa na Meneja wa Sheria wa PSPF
Abrahamu Siyovelwa aliyotoa May 27 katika mahafali ya chuo hicho.
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu
wa wilaya ya Mufindi Monica Kalalu juzi katika viwanja vya Chuo cha
Ualimu Mufindi(MUTCO) Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Iringa Baraka
Jumanne alisema lengo la msaada huo ni sehemu ya mpango wao katika
kusaidia sekta ya elimu nchini na kutekeleza maombi yaliyoombwa na
viongozi wa wilaya hizo katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete kila shule ya sekondari iwe na maabara ifikapo
Novemba mwaka huu.
“PSPF ni shirika la mfuko wa
pensheni hivyo faida lazima iifikie jamii hasa katika suala la elimu ya
za sekondari na msingi hivyo tumeamua kuwapatia mabati 100 chuo cha
Mufindi na wilaya ya Kilolo mabati 200 kutekeleza maombi yao kwa shirika
la PSPF kusaidia ujenzi wa maabara na ujenzi wa hostel kwa chuo cha
Mutco hivyo leo tunawakabidhi madawati haya mia tatu kwa lengo la
kutekeleza ahadi ya shirika.” Alisema Jumanne.
Aidha Jumanne alitoa wito kwa
viongozi kuwashawishi wafanyakazi Kilolo na wanafunzi wa chuo cha
Ualimu Mufindi kujiunga mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma wa PSPF
kwa huduma bora na mafao bora yakiwemo mafao ya
uzeeni,ulemavu,mirathi,mafao ya rambirambi za mazishi, malipo ya
wategemezi na malipo ya penshini ya kila mwezi.
Alitoa faida ya kujiunga na PSPF
kwa kuwa kuna baadhi ya mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo
yanalenga kuwawezesha watumishi kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazowakabili katika utumishi wao kabla na baada ya kustaafu
Aliongeza kuwa PSPF ina mpango
imeweka mahususi wa kuhakikisha unaboresha maisha wa wanachama wake
wakiwemo wasio wafanyakazi kwa kuweka akiba isiyo ya hiyari
itakayowawezasha kufaidika kwa faida ya maisha yao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya
ya Mufindi Monica Kalalu alilishukuru shirika la PSPF kwa msaada huo na
kutoa wito kwa wanafunzi na walimu na kuwataka wadau wengine wajitokeze
kuisaidia sekta ya elimu hususani ujenzi wa maabara ambao unaendelea
nchi nzima kwa sasa,
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo
Gerald Guninita alisema kuwa msaada huo utazisaidia shule za sekondari
za wilaya ya Kilolo katika kukamilisha ujenzi wa maabara na kuwataka
pspf wasiishie hapo katika kutoa msaada zaidi katika sekta ya elimu.
Na Amelia Rweyimamu ambaye ni
Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam, akizungumza wakati wa
kukabidhi bati hizo alisema kuwa PSPF inatambua umuhimu wa kuwepo kwa
maabara hapa nchini hivyo ofisi yake imeona vyema kushiri katika ujenzi
huo kwa kutoa bati hizo.
Rweyimamu alisema PSPF inatoa
mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao
la kifo, fao la mazishi, fao la wategemezi lisilo na kikomo, fao la
kujitoa, fao la uzee, fao la kufukuzwa kazi, na fao la ujasiriamali.
Aidha aliongeza kuwa PSPF inatoa
fao la elimu ambapo mfuko hudhamini mikopo katika bodi ya mikopo ya
wanafunzi, lengo kubwa ikiwa ni kujenga uwezo wa kuhudumia wanafunzi
wengi katika taaluma mbalimbali ikiwemo pia taaluma ya sayansi,
Teknolojia na Afya.
=================================================================
HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
TFF YAOMBA WADAU WABUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za
timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima
uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
Mshindi wa jezi ya nyumbani
atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini
atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz
au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi
za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio
na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.
SDL KUANZA KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 22
Michuano ya Ligi Daraja la Pili
(SDL) inayoshirikisha timu 24 zitakazocheza katika makundi manne ya timu
sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi
Novemba 22 mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyoketi jijini Dar es Salaam jana
(Oktoba 29 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange ilipitia
maandalizi maandalizi ya ligi hiyo ikiwemo mwongozo wake (roadmap).
Kwa mujibu wa mwongozo huo,
usajili wa wachezaji utamalizika Oktoba 31 mwaka huu. Kipindi cha
pingamizi ni kuanzia Novemba 1 hadi 7 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria
na Hadhi za Wachezaji inatarajia kukutana Novemba 11 mwaka huu kwa ajili
ya kupitisha usajili.
Pia Kamati ya Mashindano
imepitisha viwanja vya timu zote, isipokuwa uwanja wa timu ya Mpanda
United ya Katavi na ule wa Town Small Boys ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Uwanja wa Town Small Boys
haukupitishwa kwa vile hauna uzio wa kudumu ( wa chuma) wa kutenganisha
wachezaji na washabiki, na pia ufikaji wa timu Tunduru ni mgumu kutokana
na ubovu wa barabara ikizingatiwa kuwa ligi hiyo itachezwa hadi kipindi
cha Masika.
Kwa upande wa uwanja wa Mpanda
United, umekataliwa kwa vile hauna vigezo vya msingi vinavyotakiwa
ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo, kutokuwa na nyasi na uzio wa
kudumu kutenganisha wachezaji na washabiki.
===========================================================
WANAUME WATAKIWA KUSHIRIKI SAWA NA WANAWAKE KATIKA MASUALA YA AFYA YA UZAZI.
Na Magreth Kinabo_MAELEZO_Dar es salaam
Wanaume wametakiwa kushiriki
katika wa masuala ya afya ya uzazi ili waweze kusaidia katika ukoaji wa
maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinisia na watoto
Dkt. Pindi Chana wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Halmashauri
Kuu ya Chama cha Uzazi na Malezi bora Tanzania(UMATI).
Kauli mbiu ya mkutano huo ni miaka 55 ya kutoa huduma bora za uzazi wa mpango Tanzania ni tumia uzazi wa mpango , okoa maisha.
Amesema katika kusherekea maika 55 ya UMATI ni vema wadau wote washirikiane na wataalamu wa sekta ya afya katika kutekeleza kazi zinatokana na hali halisi ya mahitaji ya huduma ya afya ya uzazi kwa jamii husasani kwa wanawake, watoto na vijana ili kuokoa maisha ya wananchi.
Amesema katika kusherekea maika 55 ya UMATI ni vema wadau wote washirikiane na wataalamu wa sekta ya afya katika kutekeleza kazi zinatokana na hali halisi ya mahitaji ya huduma ya afya ya uzazi kwa jamii husasani kwa wanawake, watoto na vijana ili kuokoa maisha ya wananchi.
Dkt. Chana amesema kuwa takwimu
kwa Tanzania zinazonyesha kuwa vifo vinavyotokana na uzazi ni takribani
454 kwa kila vizazi hai 100,000 .
Ameongeza kuwa idadi hiyo inaweza kupungua iwapo huduma bora, taarifa sahihi na elimu kuhusu afya ya uzazi itawafikia Watanzania wengi ili liwe taifa lenye uelewa mkubwa kuhusu masuala ya uzazi.
Ameongeza kuwa idadi hiyo inaweza kupungua iwapo huduma bora, taarifa sahihi na elimu kuhusu afya ya uzazi itawafikia Watanzania wengi ili liwe taifa lenye uelewa mkubwa kuhusu masuala ya uzazi.
Dkt. Chana ametoa wito kutumia
njia ya makundi rika kama mabaraza ya watoto ,vilabu vya watoto na
vyama vya FEMATALK ili kufikisha ujumbe kwa ajili ya kuokoa maisha ya
mama na mtoto.
Amewataka wajumbe wa mkutano huo
kuendelea na juhudi za kuhamasisha jamii ili kuondoa vitendo vya ubaguzi
wa kijinsia kama vile ndoa za utotoni na wanaume kutoshiriki katika
masuala ya afya ya uzazi sawa na wanawake.
Dkt.Chana ametoa wito kwa UMATI kuendelea na juhudi hizo katika harakati za kumukomboa mtoto wa kike.
================================================================
RAIS MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA SATA, MEYIWA
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia
salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika
Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya
Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.
Ametuma salamu hizo kwa Rais wa
FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa
amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa
huyo wa Bafana Bafanavilivyotokea wiki hii.
Rais Malinzi amesema kuwa misiba
hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla
kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa
miguu.
Amewaomba Rais Jordan na Rais
Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia
ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.
Rais Sata (77) alifariki dunia
juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa
kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili
mjini Vosloorus.
===================================================================
Ofisi ya Taifa ya Takwimu yazindua ripoti ya mapato na matumizi ya kaya.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum jana jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua
chapisho la la utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi wa mwaka
2011/2012 ambalo linaonesha mwenendo wa hali ya uchumi nchini.
Waziri Saada amesema kuwa
utafiti unaonesha kuwa kwa kila watu 100 waliokuwa na uwezo wa kufanya
kazi mwaka 2011/2012, watu 75 walijishughulisha na kilimo na uvuvi.
“Chapisho ninalolizindua linatoa
taarifa muhimu kwa Serikali katika kutathmini na kurekebisha baadhi ya
sera na mipango ya maendeleo ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa
wananchi” alisema Waziri Saada.
Hata hivyo, Waziri Saada ameongeza kuwa matumizi ya zana duni za kilimo bado ni changamoto kubwa inayoendelea kulikabili taifa.
Utafiti unaonesha kwa asilimia
96.5 ya kaya zinazojishughulisha na kilimo bado zinatumia jembe la mkono
na asilimia 0.1 wanatumia zana za kisasa za kilimo likiwemo jembe la
plau na trekta.
Kwa upande wa washirika wa
maendeleo, mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Philippe Dongier amesema
kuwa wapo begakwa began a Serikali ya Tanzania katika kupunguza
umaskini kwa wananchi ili waweze kupata mahitaji yao ya muhimu katika
maisha ya kila siku.
Naye Balozi Finland nchini Bi.
Sinikka Antila akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washirika wengine
wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi amesema kuwa
wataendelea kushirikiana na Tanzania kutokana na mahusiano mzuri
yaliyopo baina ya washirika hao wa maendeleo.
Chapisho la Utafiti wa Mapato na
Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2011/2012 limeandaliwa naSerikali kwa
ushirikiano wa washirika mbalimbali wa maendeleo nchini wakiwemo Benki
ya Dunia, Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Uingereza
(DFID), Taasisi za Umoja wa Mataifa ikiwemo UNDP, UNFPA na UNICEF.
==============================================================
Rais Dk.Shein atembelea Benki ya Damu Salama
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Damu Salama
kiliopo Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo alipofanya ziara
fupi.[Picha na Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Meneja wa Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud
Ahmed alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho Sebleni Nyumba za Wazee
Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifutana na Meneja wa Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud Ahmed
(kulia) katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo hicho
Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akiangalia Damu Salama zilizohifadhiwa katika mashine maalum akiwa
na Aaza Humud katika chumba maalum alipotembelea katika Ofisi za Kituo
hicho Sebleni Nyumba za Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akifutana na Meneja wa Kituo cha Damu Salama Dk.Mwanaheri Mahmoud
Ahmed (kushoto) baada kutembelea chuma maalkum cha kuhifadhi Damu
Salama iliyochangiwa na wananchi Mbali mbali huko Sebleni Nyumba za
Wazee Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.] Afisa
Mhamasishaji wa Kituo cha Damu Salama Omar Said Omar (kulia) akitoa
mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na
wafanyakazi wa kituo hicho alipofanya ziara maalum ya kutembelea
kuangalia maendeleo ya utendaji kazi Sebleni Nyumba za Wazee Mjini
Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
=============================================================
SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE
Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao |
Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.
Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.
Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.
Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.
Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.
Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.
Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.
Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.
Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.
Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.
Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.
Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.
Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
Baadhi
ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania ‘SHIWATA’ wakishudia ugawaji
wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa Pwani
===========================================================
Taarifa ya Kifo Cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange anasikitika kutangaza
kifo cha Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) kilichotokea tarehe
29 Oktoba 2014 katika Hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa
akipata matibabu.
Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Mwili wa marehemu Meja Jenerali Aidan Isidore Mfuse (mstaafu) unatarajia kuwasili Tanzania tarehe 31 Oktoba 2014 saa 7:30 mchana na kuhifadhiwa katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo.
Heshima za mwisho kwa Viongozi, Wanajeshi na Watumishi wa Umma zitatolewa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo tarehe 01 Novemba 2014, kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi na mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Njombe kwa mazishi, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba, 2014 saa 8.00 mchana.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
====================================================
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja
wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere leo mara baada ya kuwasili akitokea
katika ziara yake ya Ulaya na Mashariki ya Kati Oman. Baadhi ya viongozi alioongozana nao katika ziara hiyo wakiwa katika mkutano huo.
…………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali imeanza kulifanyia kazi
tatizo la wakulima kukosa mahali pa kuhifadhia ya mazao yao, hivyo
litapatiwa ufumbuzi katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo
baada ya mpango wa kujenga maghala makubwa kuanza.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda katika mkutano wake na
waandishi wa habari alioufanya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K.Nyerere uliopo jijini Dares Salaam kufuatia ya ziara yake ya kikazi katika nchi za Uingereza, Poland na Oman. yenye lengo la kuhimarisha mahusiano.
Waziri Mkuu Pinda alisema ametembelea nchi ya Poland, ambayo ilikuwa na
lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano na kutafuta msaada wa
mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu wa kusaidia kupambana na tatizo la
uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia nafaka au chakula.
Alisema katika nchi hiyo amejionea jinsi ilivyo kuwa na mfumo maalum wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chakula.
“Unahitajika mfumo huu wa Poland wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi
chakula. Hivyo tunahitaji kiasi cha fedha cha Sh. bilioni 240 hadi
bilioni 260 kwa ajili ya kukabilian na tatizo hili, tumeandika ombi na
tumeshapeleka kwa Serikali,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Aliongeza kwamba pia wameomba mkopo wenye masharti nafuu ili kusaidia
kupambana na tatizo la uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia chakula,
hivyo kwa kuanzia wameomba mkopo wa Euro milioni 500 katika nchi ya
Poland,ambao wenye riba nafuu ya kiasi cha 0.25.
Alisema lengo ni kujenga maghala kubwa katika baadhi ya mikoa, ambayo
aliitaja kuwa ni Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Dodoma, Tanga na ghala
dogo katika Kanda ya Ziwa.
Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mahindi nchini alisema wakulima
wameweza kuzalisha tani 500,000 za mahindi, lakini changamoto iliyopo
iliyopo ni mahali pa kuhifadhia.
Aliongeza kuwa uwezo wa maghala ya Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa
Chakula(NFRA) ni tani 240,000 wakati bado kuna tani zaidi ya 200,000
zilizozalishwa mwaka jana (msimu uliopita) za mahindi na katika kipindi
cha sasa wamepanga kununua tani 3.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali imeshirkisha sekta binafsi ili iweze
kununua tani 200,000 na lakini bado chakula ni kipo cha kutosha.
Alisema kwa upande wa mpunga kuna tani zaida 800,000 kwani msimu huu
zilimezalishwa tani milioni 1.5. hali hiyo imechangiwa na matumizi ya
mbegu bora, mbolea na matumizi ya matrekta.
Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa juhudi zao za kulizalisha chukula cha kutosha.
Akizungumzia kuhusu ziara yake nchini Oman alisema ilikuwa na lengo la
kuhimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.
Alisema nchi hiyo mwikitio wa nchi hiyo wa kuwekeza ni mzuri hususan kwenye kilimo, mifugo na uvuvi.
“ Eneo walioonesha hisia ni la mifugo, hasa
“ Eneo walioonesha hisia ni la mifugo, hasa
No comments:
Post a Comment