Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.
Dkt. Pindi Chana (Mb.), leo tarehe 28 Oktoba, 2014 amefanya ziara katika Chuo
cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu –
Ilala, Dar es salaam, kwa lengo la kukagua maendeleo ya utoaji wa mafunzo kwa
wananchi.
Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi Arnautoglu hutoa mafunzo ya muda mrefu, muda mfupi na mafunzo nje ya
chuo, ambayo yote yamelenga katika kutoa stadi na maarifa mbalimbali
yanayowawezesha washiriki kupata ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe au
kuajiriwa katika Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuzalisha mali na hivyo kujiongezea
kipato na kupunguza umaskini.
Kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu asilimia kubwa ya
Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki ni watu wenye ulemavu, wengi wao wakiwa na
ulemavu wa akili.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na
watumishi na uongozi wa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Ilala – Dar
es salaam , wakati alipofanya ziara Chuoni hapo leo Oktoba 28, 2014.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.
Dkt. Pindi Chana(Mb.) akiongea na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi
Arnautoglu ( hawapo pichani), wakati alipofanya ziara Chuoni hapo,
leo Oktoba 28, 2014. Kushoto ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto na Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi
Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.
Dkt. Pindi Chana(Mb.) akikagua mazingira ya utoaji wa mafunzo katika madarasa
ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, ikiwa ni pamoja na kuhojiana na
washiriki wa mafunzo (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014. Kulia
ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi
Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.
Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakitolewa kwa
washiriki wa darasa la Uashi, katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu -
Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria
Ndamugoba akitoa ufafanuzi kuhusu eneo la chuo kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) wakati alipofanya ziara
katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo
Oktoba 28, 2014.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe.
Dkt. Pindi Chana (Mb.) akisisitiza jambo, wakati wa alipokuwa akikagua maeneo
ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba
28, 2014.
No comments:
Post a Comment