TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, October 28, 2014

HABARI ZILIZOTAWALA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 27/10/2014 NI HIZI HAPA

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI

v5Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa  na mwenyeji wake Rais Mhe
Truong Tan Sang wa Vietnam  wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu
ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi  ya siku mbili
nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
v6Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa
na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam  wakati wa
mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya
ziara yake rasmi  ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
v9 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mhe Truong
Tan Sang wakikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake
wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya
kwanza ya ziara yake rasmi  ya siku mbili nchini humo leo Jumatatu
Oktoba 27, 2014
v25:Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana baada ya
kutembelea kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL Jumatatu Oktoba 27, 2014
v28Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu

Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong,
katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo
Jumatatu Oktoba 27, 2014
==============================================================

MRATIBU MKAZI WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR

IMG_3633Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyefika Ikulu ya Zanzibar leo kwa ajili ya mazungumzo.
IMG_3641Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipomtembelea kwenye Ikulu ya Zanzibar leo.
IMG_3646Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiendelea na mazungumzo Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ofisi ya Zanzibar, Anna Senga (kushoto).
=======================================================================

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANDAA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR

unnamedMratibu wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Patrick Mwesigye kutoka nchini Rwanda akitoa nasaha zake kwa Watendaji hao katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo huko Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View. unnamed3 Mgeni rasmi Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai (kati kati) waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
…………………………………………………………………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Jumuiya ya Afrika Mashariki imeandaa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar  ikiwa ni Mkakati wa kuunda Chombo maalum cha pamoja cha usimamizi na usajili wa Dawa utakaofanywa katika nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Mafunzo hayo ya siku tano yanalengo la kuweka Msimamo wa Pamoja na Viwango sawa kwa Bodi za Vyakula na Dawa ili Dawa itakaposajiliwa katika nchi moja ikubalike kimatumizi katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai amesema kuwepo kwa Chombo cha Usimamizi wa Pamoja katika Nchi hizo kutasaidia kuondokana  na Tatizo la Uingizwaji wa Dawa zisizofaa Kimatumizi katika nchi hizo.
Amesema Chombo hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo kwa vile kutakuwa na Mikakati ya kupeana taarifa za karibu kuhusu Dawa zinazosajiliwa na kusambazwa katika nchi zao.
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo Patrick Mwesigye kutoka nchini Rwanda amesema Malengo ya Jumuiya hiyo ni kuhakikisha Vitengo vyote vya Nchi Wanachama vinajengewa uwezo na Ufanisi ili viwe katika Ubora unaofanana.
Amesema kwa sasa kila nchi inatathmini na kusajili Dawa kivyake na kwamba kukamilika kwa Mafunzo hayo itakuwa ni hatua kubwa ya kufikia Makubalianao ya kuanzishwa kwa Chombo kimoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
Akizungumza pembeni ya Mkutano huo Mratibu mwenza kutoa Zanzibar  Hidaya Juma Hamad amesema kukamilika kwa Chombo hicho kutasaidia sana upatikanaji wa Dawa salama katika nchi husika.
Amesema sambamba na hilo kutasaidia kupunguza gharama na matumizi mengi ya rasilimali ambayo yangetumika katika nchi zingine.
“Dawa Moja kuisajili inaweza kuchukua miaka miwili kwa hiyo Dawa hiyo itakaposajiliwa katika nchi moja itakuwa na uhalali wa kutumika katika nchi nyingine bila kusajiliwa tena, na hapo gharama kubwa zitakuwa zimeepukwa” Alisema Hidaya.
Pamoja na Zanzibar kupewa mafunzo hayo bado inakabiliwa na Changamoto nyingi zinazokwaza ufanisi wao ikiwemo uhaba wa Fedha, Ofisi ndogo na Idadi ndogo ya Wataalamu na Watendaji wa kukagua Maduka ya Dawa, Vyakula na upekuzi bandarini.
===============================================================

Wananchi wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa sura kwa sura

indexNa Magreth Kinabo
WANANCHI   wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa  sura kwa sura na ibara kwa ibara ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno  ya watu yenye nia ya kupotosha ukweli.
Kauli hiyo ilitolewa jana  na  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha   Rose Migiro wakati  wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ya WAMA  Nakayama, iliyopo  wilayani Rufiji  mkoani Pwani.
Dkt . Migiro  ambaye  alikuwa mgeni  rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na  baadhi ya viongozi , wakiwemo  baadhi ya wake za viongozi   na wageni  wengine mbalimbali.
“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi  ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu. 
 kazi iliyombele  yenu  ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa ibara. 
“Tusikubali kusomewa  na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dkt. Migiro.
Akizungumza na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa  kupigwa wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.
Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma baada ya Bunge Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.
=======================================================================

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIZUNGUMZA NA WAWEKEZAJI WA POLAND

unnamed3Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilusha mawazo na viongozi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil baada ya kusikiliza mada yao. Wa pili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo, Bw. KRZYSZTOF SWIACKI. (Picha na Irene Bwire wa OWM).  unnamed1Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil, Bw. NICODEMO SWIACKI (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu kampuni yao ambayo inataka kuwekeza Tanzania kwenye kiwanda cha kusafisha dhahabu na ujenzi wa hoteli ya kimataifa huko Zanzibar. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba. (Picha na Irene Bwire wa OWM).

MAMA SALMA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA KOREA KASKAZINI,PAMOJA NA MAMA RACHEL RUTO.

unnamed2Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Kaskazini Bwana Kim Yong Nam. Mama Salma alikutana na kiongozi huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ulioko Nairobi tarehe 26.10.2014 akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea nchini China.
 PICHA NA JOHN  LUKUWI 
unnamedMke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Naibu Rais wa Kenya Mama Rachel Ruto kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata mjini Nairobi tarehe 26.10.2014. Mama Salma alisimama kwa muda uwanjani hapo akiwa njiani kurejea nchini akitokea Beijing nchini China kwenye safari ya kikazi.
===================================================================

Ubalozi wa Japan waisaidia shule ya WAMA Nakayama sh. milioni 800

unnamed
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha  Rose Migoro(kulia  ) akimkabidhi cheti Kaimu Balozi wa Japan  nchini, Kazuyoshi  Matsu naga   ikiwa ni ishara ya kutambua  msaada  wa nchi hiyo wa kuisaidia  Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika hatarishi ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani  Rufiji mkoani Pwani   wakati wa sherehe ya mahafali ya pili  ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
………………………………………………………………………………
 Na Magret Kinabo, MAELEZO
 UBALOZI wa Japan kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje umetoa kiasi cha fedha cha Sh. Milioni 800, ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 500,000 kwa ajili ya kusaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ya WAMA  Nakayama, iliyopo  wilayani Rufiji  mkoani Pwani.
 Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa Japan chini,  Kazuyoshi   Matsu   naga  wakati  wa sherehe za mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana  na kuhudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha   Rose Migiro ambaye  alikuwa mgeni  rasmi  baadhi ya viongozi , wakiwemo  baadhi ya wake za viongozi   na wagemi wengine mbalimbali.
“ Juzi Idara ya Mambo ya  nje  ya  Japan imekubali kutoa Dola za Marekani 500,000 kwa ajili ya mradi wa mpya wa awamu ya pili wa kusaidia  shule ya Sekondari ya WAMA   Nakayama,” alisema  Kaimu Balozi huyo.
 Matsu   naga aliongeza kwamba fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kompyuta na utawala, yakiwemo mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
“Sisi Wajapan  tunapenda kuendelea kutoa msaada  kadri inavyowezekana. Msaada wa leo utaongeza urafiki kati nchi ya Japan na Tanzania,” alisisitiza.
Kaimu Balozi huyo alimataka kila wanafunzi wa shule hiyo, kutoa mchango wake katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutumia mafunzo aliyoyapata.
 Kwa upande wake, Dkt. Migiro, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, aliwataka  wadau mbalimbali  kuendelea kumsaidia Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma  Kikwete  katika kusaidia wanafunzi hao ili kupanua fursa za watoto wa kike kielimu.
“Nimegundua kuwa mtoto  wa kike anakabiliwa na upungufu wa fursa si kitaaluma. Hivyo kuchangia shule hii   kwa mtoto  wa ni kujenga na kuihimarisha ya  fursa yake  yeye   binafsi na familia kwa ujumla.
Dkt. Migiro alifurahishwa uweleadi wa wanafunzi wa shule hiyo, yakiwemo mazingira bora, ambapo alisema shule hiyo inaviwango bora.
Naye Mke wa Rais Mama Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka  wanafunzi hao  kutumia nafasi ya kusoma  bidii  ili waweze kufaulu hatimaye  kushika nafasi mbalimbali  za  uongozi kama Dkt.
Akizungumzia kuhusu matarajio ya WAMA kutokana shule hiyo, alisema kutoa wataalamu wa nyanja zote , ikiwemo fani ya sayansi . Hivyo  aliwataka kuongeza bidii katika masomo ya sayansi.
Alisema WAMA itaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hadi watakapofikia hatua  ya mwisho.
Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu,  Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi (TAMISEMI) Hawa Ghasia aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa bidii zao ambao zimeifanya shule hiyo  kuongeza katika wilaya hiyo.
Jumla ya wanafunzi  wapatoa 89 wanatarajiwa kuhitimu  elimu ya kidato cha nne  mwaka huu katika shule hiyo.
========================================================================

Mahafali ya pili ya WAMA Nakayama yafanyika

4
Msanii Vicky Kamata akiimba wimbo wa kumpongeza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) kwa juhudi za mkomboa mtoto wa kike kielimu wakati mahafali ya pili Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika mazingira magumu ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani  Rufiji mkoani Pwani yaliyofanyika jana.
5
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha  Rose Migoro(kulia) akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari  mwanafuzi mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika mazingira magumu ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani  Rufiji mkoani Pwani   Ulizeni Ngonyani  katika mahafali ya pili yaliyofanyika jana
6
.Baadhi ya wahitimu  wa elimu ya sekondari  ya kidato cha nne kutoka  katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika mazingira magumu ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani  Rufiji mkoani Pwani   wakifurahia na jambo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe za   mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
Picha namba 8892 ni Baadhi ya wake za viongozi waliohudhuria sherehe hiyo.
.Picha na Magreth Kinabo, Maelezo
IMG_8872
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha  Rose Migiro(katikati ) akizindua zahanati kwa  ajili ya matibabu ya  wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati  mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
IMG_8881
Wahitimu  wa elimu ya sekondari  ya kidato cha nne kutoka  katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika mazingira magumu ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wakiimba wimbo  wakati wa sherehe za   mahafali ya pili yaliyofanyika jana.
=====================================================================

NECTA yafanikiwa kudhibiti udanganyifu na wizi wa mitihani ya taifa nchini.

unnamed Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Baraza hilo ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika usajili wa watahimiwa na uchakataji wa matokeo ya Mitihani ya Taifa. Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi. unnamed1Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu huo unahusisha uchunguzi wa uhalali wa mwombaji.  Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO)
…………………………………………………………………
Frank- Mvungi – MAELEZO
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.
Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za baraza la mitihani.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.
Akifafanunua Mafie amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.
Aidha Mafie aliongeza kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka 2012 na 3,303 mwaka 2011.
Akieleza zaidi kuhusu mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya Taifa.
Katika kukabiliana na tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa katika vyeti vyao.
Katika utaratibu huo vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya watu wengine.
Baraza la Mitihani la Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002 kwa ajili  ya kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani, kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.
================================================================

Jotoardhi kichocheo cha Uchumi – RC

unnamedMkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela akiongea jambo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku mbili kuhusu masuala ya jotoardhi kwa washirki kutoka nchi zilizo katika bonde la Ufa . Mafunzo hayo yanatangulia kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi litakalofunguliwa tarehe 29 Oktoba, 2014 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
unnamed2Baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo kuhusu masuala la jotoardhi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela hayupo pichani wakati akifungua rasmi mafunzo hayo.
unnamed4Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela (katikati) akiongea jambo na Kamishna Msaidizi anayeshughulia Nishati Jadidifu , Wizara ya Nishati na Madini, Edward Ishengoma (kushoto) mara baada ya kufungua mafunzo kuhusu masuala yanayohusu jotoardhi.
unnamed5Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya masuala ya jotoardhi kutoka nchi zilizo katika bonde kla ufa na nyi nyingine duniani, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela (wanne kulia).
…………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Arusha
Imeelezwa kuwa, nguvu ya nishati mchanganyiko ikiwemo jotoardhi ni kichocheo na kipimo cha maendeleo kwa nchi yoyote kutokana na umuhimu wa nishati hiyo kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za uchumi na viwanda.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela wakati akifungua mafunzo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, kuhusu masuala yanayohusu jotoardhi yaliyoanza leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).
Mafunzo hayo yanashirikisha washiriki takriban 150 kutoka nchi mbalimbali za Afrika zilizo katika bonde la ufa na nchi nyingine duniani.
Aidha, ameongeza kuwa, mafunzo hayo ni muafaka kwa Tanzania kutokana na uzoefu ambao washiriki wataupata kutoka nchi nyingine ambazo zimepiga hatua katika masuala ya jotoardhi kama Kenya na Ethiopia ambazo zimechangia katika gridi ya Taifa ya nchi zao kiasi cha megawati 500 za nishati ya umeme unaotokana na jotoardhi.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia nishati jadidifu, Wizara ya Nishati na Edward Ishengoma, ameeleza kuwa, mafunzo hayo na uwepo wa kongamano hilo kwa Tanzania kuna manufaa makubwa.
Ishengoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la tano la Kimataifa la Jotoardhi alitaja manufaa hayo kama kutangaza hazina kubwa ya jotoardhii iliyopo Tanzania, jambo ambalo litasaidia kuvutia wawekezaji na taasisi zinazofanya utafiti wa masuala ya jotoardhi.
Ameongeza kuwa, nishati ya jotoardhi ni nishati isiyokwisha hivyo uwepo na matumizi yake yatasaidia katika ukuaji wa viwanda ikiwemo kuchangia katika sekta za kilimo na manufaa yake ni makubwa kimaendeleo.
“Jotoardhi ni chazo ambacho hakiishi. Uzalishaji wake hauna mwisho na una manufaa makubwa. Tanzania tunataka kukiendeleza chanzo hiki kama wenzetu Kenya na Ethiopia”amesisitiza Ishangoma.
Aidha, mafunzo hayo ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika kongamano la tano la Kimataifa la Jotoardhi litakalofunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Washiriki wa kongamano hilo pia watapata fursa ya kutembelea katika maeneo yenye dalili za jotoardhi ikiwemo Ngorongoro na Manyara lakini pia watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

No comments:

Post a Comment