President Kikwete meets China’s prime Minister Li Keqiang in Beijing
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meet and hold talks with Prime minister of the Peoples’ Republic of China Rt.Honorable Li Keqiang at the Great Hall of the people in Beijing this morning when the president paid a courtesy call on him.President Kikwete is on a State Visit in China at the invitation of China’s President Xi Jinping(photos by Freddy Maro)
=============================================================
MTANDAO WA WANATAALUMA TANZANIA (TPN) WATOA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA VIJANA
Mbunge wa Kigamboni, Dk.Faustine Ndugulile, akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Professional Approach Development, Lillian
Madeje, akitoa mada kwenye kongamano hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa, akihojiwa na wanahabari kuhusu ngongamano hilo. Kushoto ni Naibu
Waziri wa Maliasili na utalii Mahmoud Mgimwa ambaye alikuwa mgeni rasmi
kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal kwa ajili ya kufungua
kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa akihutubia katika kongamano hilo.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
Hapa mdau wa mtandao huo akijisali kwenye daftari la mahudhurio.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mahmoud Mgimwa (katikati),
akiwa na viongozi wa mtandao huo. Kutoka kutoka kushoto, Naibu Katibu
wa mtandao huo, Daniel Stephen, Rais wa Mtandao huo, Phares Magesa,
Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile na Mjumbe wa Mtandao huo,
Modesta Mahiga.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.
Vijana wakiwa kwenye kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali.………………………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
WATANZANIA wametakiwa kujiunga katika fursa mbalimbali za kiuchumi ili kukuza maendeleo ya nchi katika kiwango kinachostahili.
Mwito huo
umetolewa Dar es Salaam leo na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii
Mahmoud Mgimwa kwa Niaba ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Bilal wakati wa
Ufunguzi wa wa kongamano la Mtandao wa Wanataaluma Tanzania(TPN).
Alisema kuwa ni wakati muafaka kujishughulisha na fursa za kiuchumi ili kufikia malengo ya millenia.
Alisema
Serikali inaunga mkono jithada chanya zinazofanywa na sekta binafsi
ambazo zipo kwa lengo la kuendeleza jamii na nchi kwa ujumla.
Mgimwa
aliwata Watanzania wajiunge na TPN kwani una lengo la kuwahusisha katika
sekta mbalimbali ikiwemo ujasiriamali ambao mara nyingi unakuwa katika
kukuza maendeleo ya nchi.
“Watu
wengi wanaweza kujiuliza kwamba wajiunge watapata nini lakini ukweli ni
kwamba watanufaika na taaluma ambayo itakuja kuwasaidia katika maisha
yao.
“Napenda
niwapongeze kwani nimeona vijana wengi wamejiunga na mtandao huu ambao
naamini utawasaidia vijana kuondokana na tatizo la ajira,”alisema.
Naye Rais wa TPN Phares Magesa alisema kuwa watu waache kusubiri kuwezeshwa badala yake wawe na mwamko wa kujiwezesha wenyewe.
Alisema lengo la sekta hiyo ni kutumia sekta ya ujasriamali katika kusaidia jitihada za Serikali kukuza maendeleo ya nchini.
“Naamini
kwamba kila kijana ambaye amehudhuria kongamano hili akitoka hapa
anaweza kuwa mtu mzuri wa kujihusisha na ujasiriamali,”alisema.
Alisema
kuwa maadhimio ya mkutano huo yatasaidia kutatua changamoto mbalimbali
zionazpojitokeza katika jamii na kuweza kuzitatua kwa wakati.www. habari za jamii.com
==============================================================
President Kikwete receives a rousing welcome in Beijing
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete introduces former OAU/AU Secretary General Salim Ahmed Salim to China’s President Xi Jinping during the formal reception held at the Great Hall of the People in Beijing this evening.Left is the Minister for Foreign Affairs Bernard Membe and second left is CCM Secretary General Abdulrahman Kinana. President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and his host Chinese President Xi Jinping inspects a guard of honor mounted China’s People Defense force in Beijing this evening during a formal reception at the Great Hall of the people. President Kikwete is on State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping. President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his host President Xi Jinping waves to the cheering crowd during a formal reception for the President and his delegation held at the Great Hall of the People in Beijing at the climax of his State visit this evening.(photos by Freddy Maro)
=====================================
PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UN)
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,ambaye
alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Dar es Salaam leo, katika
Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 69 tangu kuundwa
kwake. Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Karimjee.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez (kushoto) akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakifuatilia matukio mbalimbali ya hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maadhimisho hao.
Waziri Tibaijuka akihojiwa na wanahabri kuhusu
maadhimisho hayo.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiwa
kwenye maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisubiri kuondoka baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Gwaride maalumu la watoto la bendera likitoa
heshima kwa mgeni rasmi.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari
wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni
wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani zikiendelea
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
PROFESA TIBAIJUKA AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 69 YA UMOJA WA MATAIFA (UNTibaijuka
alitoa wito huo leo katika sherehe za kuazimisha miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Waziri
Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maazimisho hayo
alibainisha kuwa mabadiliko ya Tabia Nchi yameendelea kuwa tishio kubwa
kwa binadamu katika siku za leo duniani kote.
Kutokana
na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliitisha mkutano wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23, mwaka huu ambapo watu, nchi,
mabara na wafanyabiashara walitoa tamko la kuungana pamoja kwa kila
mmoja kuinusuru dunia.
Prof.
Tibaijuka alisema kuwa akiwakilisha bara la Afrika, Rais wa Tanzania
Jakaya Kikwete aliwasilisha mpango unaoonyesha juhudi za pamoja
zinazofanywa na bara hilo kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Katika
mkutano huo, Tanzania imeahidi kuimarisha juhudi zake katika kutunza
misitu na matumizi ya nishati kama upepo, sola na gesi asilia,” Waziri
Tibaijuka alisema.
Hivyo
Prof. Tibaijuka alihimisa nchi wahisani kutimiza ahadi zao kwa wakati
hususani kutoa fedha kiasi cha dola za Kimarekani billion 100 kila mwaka
hadi 2020 zitakazosaidia katika juhudi za kupambana na changamotio
hizo.
Waziri
aliwaambia wageni waalikwa katika sherehe hizo pia kuwa Tanzania
inaendelea kutekeleza malengo ya changamoto za mileniamu na kuhakikisha
kuwa nchi inaendelea kuimarisha amani, utawala wa sheria na kudimisha
haki za binadamu.
President Xi Jinping Welcomes President Kikwete in Beijing
China’s
President Xi Jinping welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the
Great Hall of the People in Beijing this evening during the official
formal reception at the climax of the State visit at the invitation of
the Chinese leader. President
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for
an official photograph with their host China’s President Xi Jinping and
his wife China’s First Lady Peng Liyuan shortly after they arrived for
an official formal reception at the Great Hall of the People in Beijing
this evening(photos by Freddy Maro)
MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MKE WA RAIS WA CHINA MAMA PENG LINYUAN
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na mwenyeji wake Mke wa Rais wa
China Mama Peng Liyuan wakielekea kwenye chumba maalum kilichoko kwenye
ukumbi wa The Great Hall of China kwa ajili ya kufanya mazungumzo. Mama
Salma yupo nchini China akifuatana na Mume wake Rais Dkt. Jakaya Kikwete
kwenye ziara nchini humo. Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake
Mama Peng Linyuan, Mke wa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kwenye
jumba la mikutano la The Great Hall of China jijini Beijing tarehe
24.10.2014
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mama Peng Linyuan, Mke wa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kwenye jumba la mikutano la The Great Hall of China jijini Beijing tarehe 24.10.2014
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mama Peng Linyuan, Mke wa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping kwenye jumba la mikutano la The Great Hall of China jijini Beijing tarehe 24.10.2014
PICHA NA JOHN LUKUWI
=================================================================
Prof. Tibaijuka: Magonjwa ya Mlipuko yatekelezwe Kimataifa
Na Anita Jonas-MAELEZO
Umoja wa Mataifa umeshauri kuchukua hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya milipuko ya magonjwa hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya Kidunia kwani yanaathiri mifumo yote ya kimaendeleo.
“Mataifa yaliyoendelea yasingepuuzia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza Afrika hali isingekuwa hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai yangu kwa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua tahadhari wakati wote ”Alisema Prof. Tibaijuka.
Aidha, Prof. Tibaijuka alisema kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio miongoni mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo hawanabudi kusaidia Mataifa mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa Kijani wa Hali ya hewa.
Akizungumzia kuhusu hatua ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000 kutoka Burundi, Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha ulimwengu kuwa suala la mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa kazi na kuwafanya wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.
Naye Mratibu muwakilishi wa makazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez alisema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine, wamepanga kusaidia na kuboresha miundombinu ya kiusalama ili kuendeleza amani Duniani kwani bila amani maendeleo ni vigumu kupatikana.
Pia Bw. Rodriguez aliipongeza Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia katika sekta ya afya kwa ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya nchini vinatoa huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
Sherehe hizo zimebebwa na kauli mbiu ya “Leave no One Behind” ikiwa na mlengo wa kuleta maendeleo yenye usawa duniani.
===============================================================
Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kuanza katikati mwa Mwezi Novemba.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid
Mahamoud Hamid(kushoto) akitoa ufafanuzi baada kusoma taarifa kuhusu
kuanza kwa shughuli za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares
Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC.Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi
Julias Malaba.
…………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo,Maelezo
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)
imesema kwamba zoezi la majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura linatarajia kuanza rasmi katikati mwa mwezi Novemba
mwaka huu.
Aidha NEC imefafanu kwamba
zoezi hilo, litafanyika kwa kutumia mfumo mpya wa ‘Biometric Voter
Registration’(BVR) katika majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Kawe
katika Manispaa ya Kinondoni, Kilombero, Halimashauri ya Mji wa
Kilombero na Mlele, Halimashauri ya Mlele, ambapo vituo vya uandikishaji
vimewekwa katika kata zilizomo katika majimbo husika.
Hayo yalisemwa na Makamu
Mwenyekiti wa NEC pia na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid
Mahamoud Hamid,wakati akisoma taarifa kuhusu kuanza kwa shughuli za
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dares Salaam.
“Tume tayari imekwishapokea
baadhi ya vifaa muhimu vya uandikishaji zikiwemo fomu za unadikishaji,
hivyo kinachosubiriwa ni kupokea BVR kits 250 zinazotarajiwa kupokelewa
wakati wowote kuanzia leo. Zoezi la Uandikishaji litakapoanza, vituo
vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,
vyama vya siasa vinaruhusiwa kuweka mawakala wao katika kituo ili
kushuhudia jinsi uandikishaji utakavyokuwa unafanyika,” alisema Hamid.
Makamu Mwenyekiti huyo alisema baada ya zoezi hilo kukamilika zoezi hilo litaanza katika maeneo mengine.
“ Tunatarajia Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa wakati mmoja katika
mikoa yote nchini isipokuwa mkoa wa Dares Salaam na
Zanzibar.Uandikishaji katika mikao ya Dares Salaam na Zanzibar
utafanyika baada ya uandikishaji katika mikoa yote utakapokamilika.Muda
wa uandikishaji utakuwa ni siku saba katika kila kituo,” alisema.
Aliongeza kwamba uandikishaji
katika mikoa yote umepangwa kufanyika kuanzia mwanzoni mwa mwezi
Januari, mwaka huu hadi katikati ya Februari mwaka huu, wakati katika
mikoa ya Dares Salaam na Zanzibar utafanyika mwishoni mwa mwezi Februari
mwaka huu.
Alisema uandikishaji katika
mikoa yote utafanyika katika awamu nne kwenye kila halimashauri ili
kutoa fursa ya kuhamisha vifaa vya uandikishaji kutoka eneo moja
kwenda eneo lingine.
“Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura utahusisha wapiga kura wote wapya na wa zamani. Wapiga
kura wa zamani yaani wale ambao walikuwa wamejiandikisha katika Daftari
la Zamani, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha vilivyoko
karibu na maeneo wanayoishi ili kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za
vidole, picha na saini zao kuiongizwa katika mfumo Biometric Voter
Registration na hatimaye watapewa vitambulisho vipya.” Alisisitiza.
Alisema wapiga kura ambao
watakuwa na kadi zao za kupiga kura za zamani watatakiwa kwenda na kadi
zao katika kituo cha kujiandikisha ili kurahisisha zoezi la kuhamisha
taarifa zao za awali katika mfumo mpya wa BVR.
Aidha alifafanua kwamba kwa
wapiga kura waliopoteza kadi au wale ambao kadi zao zimeharibika
watatakiwa kwenta kituoni ili kujiandikisha na kupewa kadi mpya.
Hamid alisema kwa wapiga kura
wenye vitambulisho vya taifa Dares Salaam na Zanzibar watakuja na kadi
zao ambazo ni taarifa zao zitasomwa na vifaa maalum ili kupunguza muda
utakaotumika katika zoezi hilo, pia watapewa kadi mpya ya mpiga kura.
Alisema kwa wapiga kura
wanaoishi na ulemavu na wale ambao hawajui kusoma na kuandika
wanaruhusiwa kwenda kituoni na mtu mmoja katika familia wanayemuamini
ili kusaidia katika uandikishaji.
“Uboreshaji huu unahusisha pia
kuandikisha wapiga kura wote waliotimiza umri wa miaka 18 au zaidi na
wale ambao ifikapo siku ya upigaji kura ya maoni na uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 watakuwa wametimiza umri wa miaka 18. Pia wale wote ambao kwa
sababu mbalimbali hawakuwahi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura katika mazoezi yote uandikishaji yaliyopita,”
alisisitiza.
Hivyo jumla ya watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi wapatao milioni 23.09 wanatarajiwa kujiandikisha.
Hamid aliongeza kwamba mpiga
kura atakayejiandikisha katika daftari hilo la sasa pekee na kupewa kadi
ndiye atakayeruhusiwa kupiga kura.
“Wakati wa uandikishaji,
kipaumbele kitatolewa kwa watu wanaoishi na ulemavu, wazee, wagonjwa
wakinamama wajawazito na wenye watoto wachanga. Hivyo hawatalazimika
kusimama kwenye mstari.
Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi
kutoka NEC, Julias Malaba alisema tayari kiasi cha fedha cha Sh.
bilioni 15 zimeshatolewa kwa ajili ya zoezi hilo.Huku Makamu Mwenyekiti
wa NEC akisema bajeti halisi litafafanuliwa baadae.
Kwa upande wake, Sisti Cariah
ambaye ni Mkuu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Naibu Katibu NEC,
alisema daftari hilo litakamilika Aprili 14,mwaka huu na litawekwa
wazi kwa muda wa siku tano katika maeneo husika ili kumwezesha kila
mtu aliyejiandikisha aende kukagua na kujiridhisha kwa taarifa zake
zimeandikwa kwa usahihi.
Tume hiyo inatoa wito kwa
wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza kwa wingi katika
vituo vyote vya uandikishaji kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari
hilo.
Akizungumzia kuhusu mfumo wa BVR alisema unasaidia kupunguza ujiandikisha mara mbili na kuwa na taarifa sahihi.
==============================================================
Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala latoa tamko.
Na Beatrice Lyimo- Maelezo-Dsm.
BARAZA la Tiba Asili na Tiba
Mbadala latoa tamko kuhusu vipindi na matangazo yote ya tiba asilia na
tiba mbadala yanayoonyeshwa kwenye vyombo vya habari hapa nchini kuwa ni
batili yenye kupotosha na yasiyo na vibali.
Akizungumza na waandishi leo
jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Rogassian
Mahunnah alisema kuwa, baraza hilo linawashauri wananchi kutoamini
huduma zinazotangazwa na watu hao kuhusu tiba wanazozitoa.
Amesema kuwa, kwa mujibu wa
Sheria shughuli zote zinazohusu tiba asilia na tiba mbadala ni budi
zisajiliwe na kupewa kibali kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala.
“Kanuni za maadili, miiko na
mienendo ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala, imeweka utararibu wa
kufuatiliwa pale mganga wa tiba asili na tiba mbadala anapotangaza
shughuli zake kupitia vyombo vya habari na mabango kwa jamii” alisema
Profesa Mahunnah.
Kwa mujibu wa taarifa za
Mwenyekiti huyo zinasema kuwa, kumekuwa na uwepo wa Maafisa feki
wakijitambulisha kama Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
na kutoa vibali bandia kwa njia ya simu kuhusu urushwaji wa vipindi
katika vyombo vya habari.
Naye kaimu Msajili wa Baraza
hilo, Bi. Mboni Bakari ameongeza kuwa, kumekuwepo pia na matumizi ya
mashine ya Quantum na za kuondoa sumu mwilini kwa baadhi ya waganga
ambao hawana elimu ya kutosha juu ya kutafsiri majibu na kujua matumizi
sahihi ya vifaa hivyo.
“kutokana na kutosajiliwa kwa
mashine hizi na TFDA, ufanisi na usahihi wa mashine ya kuondoa sumu
mwilini hautambiliki na hauna uhakika” aliongeza Bi. Mboni.
Aidha, Baraza hilo
linawasisitizia waganga kuendelea kufanya usajili kwenye ofisi za
waratibu wa tiba asilia na tiba mbadala katika Wilaya na Halmashauri zao
na kutoa huduma katika sehemu walizosajiliwa.
===============================================================
NGUMI KUPIGWA KESHO OKTOBER 25 FRENDS CORNER MANZESE
Bondia
Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika
kesho oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana
na George Dimoso mpambano wa raundi nane picha na SUPER D BLOG
Bondia
Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya
kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba
25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG
……………………………………………………………………
Mwandishi Wetu
Jumamosi ya October 25 katika ukumbi wa friends Corner
Manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu
wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mhamila ‘Super D’
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa ‘Moto wa Gesi’ na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki ‘Manny Chuga’ na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa ‘Moto wa Gesi’ na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki ‘Manny Chuga’ na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
No comments:
Post a Comment