TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, October 29, 2014

PATA HABARI KUBWA ZILIZOTOKEA SIKU YA JANA JUMANNE TAREHE 28/10/2014 NA KUANDIKWA NA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI

BENKI YA NMB YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA PROMOSHENI YA WEKA NA USHINDE

 Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB, Salie Mray (kulia), akimkabidhi Florence Kasenene cheti cha ushiriki katika  promosheni ya Weka na Ushinde katika hafla iliyofanyika viwanja vya benki hiyo Tawi la Sinza Mori Dar esaSalaam leo asubuhi. Kasenene alijishia bajaj.
 Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NMB, Salie Mray (kulia), akimkabidhi Florence Kasenene, akimkabidhi funguo wa bajaj, Florence Kasenene katika hafla hiyo.
 Ofisa Habari wa benki hiyo, Doris (kushoto), akizungumza kwenye sherehe hiyo.
 Mshindi wa pikipiki, Mariam Mburinyingi  akifurahi kushinda pikipiki hiyo na mmoja wa maofisa wa benki hiyo.
 Mshindi wa baiskeli, akiijaribu  kuiendesha baada 
ya kukabidhiwa.
 Washindi wa baiskeli wakiwa na baiskeli zao pamoja 
na maofisa wa benki hiyo.
 Baiskeli walizokabidhiwa washindi.
 Pikipiki walizokabidhiwa washindi hao.
Bajaj na pikipiki zilizokabidhiwa kwa washindi.
 
Dotto Mwaibale
 
BENKI ya NMB imetoa zawadi za pikipiki, bajaj na baiskeli kwa washindi wa promosheni ya Weka na Ushinde inayoendeshwa na benki hiyo.
Salie Mray alisema washindi waliopata zawadi kwa mwezi wa kwanza wa promosheni hiyo ni wa Kanda ya Dar es Salaam.
“Kwa Kanda ya Dar es Salaam tuna washindi 30 ambao zawadi zao tunawakabidhi leo ‘jana’ na wale wa Kanda zingine watapewa zawadi zao kwenye kanda zao” alisema Mray.
Aliwataja washindi walioshinda bajaj ni watano, washindi watatu wameshinda pikipiki za magurudumu mawili na washindi 22 wamejishindia baiskeli aina ya Phoenix.
Alisema katika promosheni hiyo kuna zawadi nyingi za kushindania zenye thamani ya sh.milioni 500 hivyo watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani droo zingine zitaendelea kuchezeshwa kila Jumatatu.
Alisema zawadi zilizotolewa jana zinatokana na droo ya nne iliyofanyika kwa nchi nzima ambapo tayari wamepatikana washindi wa 17 wa bajaj, 16 pikipiki na 132 baiskeli aina ya Phoenix.
Mray alisema hiyo ni fursa kwa wateja wao kwani kila mtu anaweza kushinda ili mradi tu afuate taratibu za kushiriki ambazo ni kuweka fedha kwenye akaunti yake mara nyingi awezavyo ili kujiongezea naafasi zaidi kushinda. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
=====================================================================

Rais Kikwete Mgeni Rasmi maadhimisho ya miaka 10 ya Utumishi wa Umma.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10   ya Tume hiyo tangu kuanzishwa kwake ambapo Kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, KatibuMkuu Kiongozi na Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea,Taasisi na Mashirika ya Umma. Kulia ni Naibu katibu wa Tume hiyo Bi NeemaTawale. unnamedKatibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10   ya Tume hiyo tangu kuanzishwa  kwake ambalo litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere tarehe 30 Oktoba, 2014 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kushoto ni Naibu Katibu wa Tume hiyo Bi Rose Elipenda na kulia ni Naibu Katibu  Bi Neema Tawale akifuatiwa na Naibu Katibu Bi Rose Mboya.
(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO)
 
……………………………………………………………………………
 
Frank  Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kongamano la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume  ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika jijini Dar es salam Oktoba 30 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Julius  K. Nyerere.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ulio lenga kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo.
Akifafanua kuhusu siku hiyo Mpangala amesema Kongamano hilo la siku moja litaanza saa 2:00 asubuhi hadi 11:00 jioni ambapo pamoja na mambo mengine kongamano hilo litahusisha historia ya Utumishi wa Umma kabla na baada ya Uhuru.
“Kauli mbiu katika  maadhimisho hayo ni Imarisha Uzalendo,Uadilifu na Uwajibikaji katika Kusimamia Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma ili kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini” alisemaMpangala.
Akizungumzia wageni watakaoshiriki Mpangala amesema kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Idara  zinazojitegemea, Taasisi na Mashirika ya Umma, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu.
Pia Mpangala alitoa wito kwa waalikwa wote kuhudhuria  kongamano hilo kwa lengo la kuonaTume ilipotoka, ilipo na inapoelekea kwa kuyatazama mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 na mwelekeo wa Tume katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Tume ya Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) cha sharia ya Utumishi wa Umma NA. 8 ya mwaka 2002 ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 9 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa kwa sharia Na 18 ya mwaka 2007.
=================================================================

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii yafanya ziara katika Miradi mitatu ya NSSF jijini Dar

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo ‘Dege Eco Village’,iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo ‘Dege Eco Village’,iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mbunge jimbo la Lindi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Salum Barhan akifatilia kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni iliyokuwa ikitolewa na Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (hayupo pichani)
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akielekeza jambo wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo ‘Dege Eco Village’,iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyovu Mkoani Kigoma,Mh. Albert Obama akiuliza swali kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo kuhusiana na mradi huo wa Daraja la Kigamboni.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mhandisi Karim Mattaka (katikati) akiwaeleza Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii namna wanavyopanga nondo ili kuweka uhimara wa daraja la Kigamboni ambalo linatarajiwa kumalizika mapema mwakani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa nne kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo wakitembelea Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakiangalia namna maji yanavyotolewa chini kwa ajili ya kuweka nguzo za Daraja la Kigamboni.
Waheshimiwa wakijadiliana wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo ‘Dege Eco Village’,iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
 Ubao wa Maelezo ya Mrad wa Kijiji
Baadhi ya Nyumba za Mradi wa Kijichi.
Mh. Obama akiangalia Mandhali tulivu ya Kijichi.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo.
Majengo yanayoendelea kujengwa katika eneo la Mradi wa Kijichi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. 
Mh. Maua Daftari
Mh. Sugu.
Baadhi la Majengo ya Mradi wa Kisasa wa Dege eco Village yakiendele kujengwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda akizungumza na wanahabari walioambatana nao kwenye ziara hiyo.
Picha ya pamoja ya Wabunge Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) mara baada ya kumalizika kwa ziara.
=======================================================

RAIS KIKWETE AONDOKA VIETNAM BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI NCHINI HUMO

unnamedRais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza (wa pili kushoto),
Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mussa Azzan Zungu (kulia), Mbunge
wa Tumbe Mhe Rashid Ally Abdallah (kushoto) na Balozi wa Tanzania
nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo muda mfupi
kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara
yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28,
2014
unnamed1 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji
wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi
tayari  kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara
yake ya siku sita nchini China na Vietnam  leo Oktoba 28, 2014
unnamed2 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji
wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi
tayari  kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara
yake ya siku sita nchini China na Vietnam  leo Oktoba 28, 2014
unnamed4 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na  Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza na Balozi wa Tanzania
nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari  kuanza safari ya
kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini
China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014
unnamed5Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa  na wenyeji wake katika

uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari  kuanza
safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku
sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014
====================================================================

Wanawake wameaswa kutumia fursa iliyopo katika sekta ya bahari.

unnamedMkurugenzi wa Usalama wa Mazingira Majini Bw. Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka akiongea na wajumbe wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaofanyika jijini Dar es salaam.
unnamed1
Mjumbe wa sekretarieti ya Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) Bi. Veronica Maina akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
unnamed2
Mwenyekiti wa WOMESA kutoka Mauritius Bi. Meenaksi Bhirugnath-Bhookun akitoa mada wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika  uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
unnamed3
Dkt. Faustina Ncheye kutoka WOMESA Tanzania akimpima afya Bi Tumaini Namoya mjumbe wa mkutano huo kutoka Kenya.
unnamed4
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa mwaka wa WOMESA mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
(Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO)
…………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Wanawake wameaswa kutumia fursa iliyopo katika sekta ya bahari kwa kupata elimu na mafunzo ya sekta hiyo ambayo ni msingi wao katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ukuaji sayansi na teknolojia inayoongezeka kwa kasi duniani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Mazingira Majini Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) unaofanyika leo jijini Dar es salaam.
Akisoma hotuba kwa niqaba ya Katibu Mkuu huyo, Mwaijande amewataka wajumbe wa mkutano huo (WOMESA), wawe tayari kujadili masuala yanayojenga na kukuza ushiriki wa wanawake katika sekta ya bahari katika nchi zao.
Katika mkutano huo wa siku nne ambao umeanza leo oktoba 28 na unatarajiwa kumalizika Oktoba 31 mwaka huu, mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mpango mkakati wa WOMESA kuhusu ushiriki wa wanawake katika masuala ya sekta ya bahari katika nchi wanachama. 
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey amesema kuwa WOMESA imekuwa msatari wa mbele katika kumwendeleza mwanamke kwenye sekta ya bahari.
Pamela amesisitiza kuwa wajumbe wa mkutano huo ni vema waelewe na kusimamia dira ya WOMESA ambayo lengo lake ni kuwawezesha wanawake kupata ajira katika sekta ya masuala ya bahari kwa njia ya kupta elimu na mafunzo katika kuendeleza taaluma yao juu ya masuala ya bahari.
Mkutano huo wa WOMESA unajumuisha wajumbe 52 kutoka nchi mbalimbali wanachama zikiwamo Ethiopia, Namibia, Komoro, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Mauritius na Kenya.
Nchi nyingine ni Angola, Sudani, Lesotho, Uganda, Somalia, Eritrea, Botswana, Rwanda, Madagaska, Afrika Kusini, Msumbiji, Burundi, Malawi, Djibout, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
Mkatano huo wa siku nne unafanyika nchini chini ya ufadhili wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Taasisi ya Masuala ya Bahari Tanzania (DMI),   shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) kwa kushirikiana na  Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP).
==================================================================

Taasisi ya Viwango Zanzibar wakuatana na Dk.Shein

==================================================================

TATIZO LA UPUNGUFU WA UMEME KUPATIWA UFUMBUZI MWAKANI.

index NA MAGRETH  KINABO. MAELEZO
TATIZO la la kutokuwepo umeme katika jijini Dares Salaam hususan maeneo ya katikati ya Jiji na nje kidogo ya Jiji na mkoa wa  Arusha, ikiwemo mikoa ya  Mwanza na Shinyanga linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi ifikapo mwaka Juni mwaka 2015.
Hayo yalisemwa leo na  Mhandisi Mkuu wa masuala ya Umeme kutoka Benki ya Maendeleao ya Afrika(ADB), Dkt.  Babu  RAM  wakati akizungumza na waandishi wa habari leo(jana) mara baada ya  Waziri wa Fedha wa Marekani , Jack  Lew  ambaye aliwasili nchini usiku wa kuamkia leo(jana) na alitembelea nchini, jijini Dares Salaam kwa ziara ya siku moja ili kujionea shughuli mbalimbali  ukiwemo mradi wa ‘Electricity  V ‘ unaoendelea kwenye  Kituo kidogo cha kusambazia umeme kilijulikanacho kwa jina la Sokoine.
“ Mradi huu ni mojawapo ya agenda  ya  Serikali ya Tanzania ya matokeo makubwa sasa(BRN). Unahusisha ujenzi na uboreshaji wa vituo vidogo vya umeme vilivyoko katika jiji la Dar es Salaam na  mkoa wa Arusha, pia unahusisha upanuzi wa miundombinu ya usambazaji wa umeme katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Unaratajia kukamilika katikati ya mwaka 2015,” alisema  RAM.
 Alisema mradi huo  katika kituo hicho , ambacho kinahusisha jiji la  Dares Salaam na mkoa wa Arusha kinatarajia kunufaisha mara mbili ya idadi ya sasa ambao ni  wateja 3000 na wafanyabiashara  wakubwa 400. Pia  wateja usambazaji wa umeme katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga utanufaisha wateja wapya 9000.
“Mradi wote huu utanufaisha wateja wanakadriwa kufikia 12,000 na utagharimu Dola za Marekani milioni 50,” alisisitiza.
Alisema mradi huo utahusisha usambazaji wa umeme katika kituo kidogo cha  umeme  cha Ilala na mkoa wa Arusha kwenye eneo la Njiro.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa masuala ya umeme (nishati) kutoka  Wizara ya Nishati na Madini,  Mhandisi Innocent  Luoga alisema  mradi huo ni maojwapo wa Dira ya Maendeleo ya nchi ili ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe ni nchi ya kipato cha kati.
Aliongeza kwamba mradi huo, utaongeza upatikanaji wa umeme kwenye maeneo ya katikati ya jiji la Dares Salaam, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Ocean Road na Ikulu kwa sasa mahitaji ni makubwa kutokana na kuongezeka kwa majengo na jiji hilo kupanuka.
“Lengo kubwa la mradi huu ni mkakati wa Serikali wa kuongeza upatikanaji wa umeme katika jiji la Dares Salaam, Arusha,Mwanza,Shinyanga na maeneo ya vijijini,” alisema Luoga.
Luoga alisema  katika mradi huo, itawekwa transforma  yenye uwezo mkubwa  wa kufikia 30MVA  badala ya 15MVA zilizokuwepo hapo awali.
Alisema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambayo inapata fedha kutoka Marekani kupitia mpango wa Rais wa Marekani, Barrack Obama wa miradi ya umeme (Power Africa Initiative),
 Aliitaja miradi mingine, kuwa ni City Center unaofadhiliwa na Finland, Gongolamboto, Kurasini, Mkuranga, Mbagala, Kurasini, Kigamboni, Masaki, Mbezi, Ilala na Ubungo , ambapo itahusu upanuzi wa vituo na kuongeza transforma  kubwa.
Katika ziara ya Waziri wa Fedha wa Marekani, Lew pia  alitemblea Wizara ya Fedha ,ambapo alifanya mazungumzo na   Waziri wa Fedha, Saada  Salum Mkuya, maeneo ya Bandari . kituo cha mafuta cha Kurasini na kufanya mazungumzo na viongozi husika.
Waziri huyo amefanya ziara hiyo katika nchi za Afrika ,ambazo ni Misri, Tanzania na Afrika ya Kusini , ambapo anatarajia kuwasili nchini humo baada ya kuondoka nchi leo usiku.
Lengo la ziara hiyo ni kuhimarisha uhusiano na nchi za Afrika kupitia baada ya ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama  aliyoifanya mwaka jana katika nchi za Afrika  na kuzindua mpango huo.
 Waziri huyo atarejea nchini kwake baada ya ziara ya Afrika Kusini.
 Mradi huo katika awamu ya kwanza  umehusisha nchi zingine ambazo ni  Kenya, Ethiopia,Ghana,Liberia  na Nigeria, ikiwemo Tanzania na una lengo la kunufaisha wateja zaidi ya milioni 60.
====================================================================

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 WAANZA KAMBI

imagesWarembo wa Miss Universe Tanzania 2014 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Golden Tulip Hotel. Hii ni kwa ajili ya kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania 2014 itakayofanyika tarehe 02 mwezi Octoba.
Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema usaili wa mwaka huu umefanyika katika mikoa mitano ya Tanzania na warembo zaidi ya 70 walisajiliwa kwa mashindano haya.
Kambi ya Miss Universe Tanzania 2014 imekamilishwa na warembo 12 kutoka mikoa mitano ya Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam, pamoja na mrembo mmoja kutoka Zanzibar.
“Tumechagua warembo ambao wameonyesha uwezo wa kujitambua na kuelewa umuhimu wa kushiriki katika mashindano makubwa kama haya. Tuna wanafunzi wa vyuo wanaosomea udaktari, uhandisi,uhasibu na pia tuna akina dada wajasiriamali . Tunafurahi kuona kila mwaka warembo wetu wanazidi kujitambua na kazi yetu kubwa ni kuwaendeleza” alisema Sarungi
Pamoja na zawadi ya fedha taslimu, mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 atapata fursa ya kutangaza bidhaa mbalimbali na kufanya kazi za kijamii. Pia kama ilivyo ada kwa mwaka wa 4 sasa, mshindi atapewa nafasi (scholarship) ya kusoma New York Film Academy , Marekani. Hivi sasa washindi wa mwaka 2011 na 2012, Nelly Kamwelu na Winfrida Dominique wako New York masomoni.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata James ,2010 Hellen Dausen , 2011 Nelly Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaniwa na Insignia, MeryLight , Golden Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Missie Popular blog, Seif Kabelele blog, Urban Rose Hotel, RichBoys Entertainment (TZ) Ltd na New York Film Academy.
===================================================================

HABARI KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

indexNa Maryam himid kidiko na Kijakazi Abdallah-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi zake za kuwaelimisha Wananchi ili waachane na tabia ya kujenga karibu na  maeneo ya Kambi za Kijeshi kwa lengo la kuepuka usumbufu pamoja na madhara yanayoweza kuwakumba baadae.
Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Abuod wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma katika kikao cha tano kinachoendelea cha Baraza la Wawakilishi. 
Saleh alitaka kujua kuwa lini Serikali itafikiria kuzihamisha kambi za kijeshi zilizopo karibu na Makaazi ya Raia na kuzipeleka nje ya Miji na Vijiji.
Waziri Aboud alifahamisha kuwa katika nchi yoyote ile duniani kambi za kijeshi huwekwa Kimkakati kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi husika ikiwemo Zanzibar.
Alisema Kambi zilizopo nchini sio tatizo na kwamba zimewekwa kwa kuzingatia haja ya kiulinzi, usalama na mazingira ya Zanzibar ilivyo.
Ameongeza kuwa Jeshi la Wananchi linahitaji maeneo maalum yakiwemo ya kufanyia mazoezi ili kujiweka tayari kwa adui yoyote Yule atakaeingia katika nchi kwa kufanya uadui.
Hata hivyo aliongeza kuwa kwa sasa kambi zilizopo zilijegwa kwa miaka mingi iliyopita na kwa wakati huo maeneo hayo hayakuwa karibu na makaazi ya raia.
Amesema kutokana na maeneo ya Kambi hizo kuvamiwa na Wananchi kwa lengo la kuanzisha Makaazi limekuwa tatizo na kwamba juhudi zinafanywa kuondokana na tatizo hilo ikiwemo kuwaelimisha Wananchi juu ya Madhara yanayoweza kujitokeza
====================================================================

Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi

2aBaadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
3aBaadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
4aMmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo kabla ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini Arusha.
…………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Arusha
Tanzania imeeleza mipango yake ya kuendeleza masuala yanayohusu nishati jadidifu mbele ya Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimtaifa la Jotoardhi linaloendelea jijjini Arusha.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho kwa niaba ya Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Jotoardhi Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Paul Kiwele amesema kuwa lengo la kukutana kwa kamati hiyo ni kuzungumzia hatua zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao.
Bw. Kiwele ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo ameeleza kuwa, lengo jingine la kikao hicho ni kuangalia faida zilizopatikana kupitia nishati hiyo pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na kuona namna bora ya kuzitatua.
Ameongeza kuwa, pendekezo la nchi wanachama kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza masuala ya jotoardhi katika nchi zao ikiwemo ya kifedha limepitishwa na mashirika kadhaa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhifadhi wa Mazingira ( UNEP) na Umoja wa nchi zilizo katika bonde la Ufa (ARGEO)
Aidha, Bw, Kiwele ameongeza kuwa, kikao hicho kimeamua kuipa nafasi Tanzania kusaidiwa kuendeleza masuala ya jotoardhi katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la Ngozi, Mkoani Mbeya.
Kikao hicho cha Kamati ya Watoa Maamuzi ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea katika kongamano la tano la jotoardhi ambapo linakwenda sambamba na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusu masuala ya jotoardhi ikiwemo masuala ya utafiti, uchorongaji na masuala ya fedha.
Kongamano hilo litafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal jijini Arusha na litawashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali duniani.
=============================================================

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.

1Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE). Picha na OMR 2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya GS 1, Ester Budili, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene. Picha na OMR 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya Kazymate, Mariam Mjewa, kuhusu Jarida maalum la ‘Mchakarikaji’  wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Chupa ya kinywaji cha Dodoma Wine wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 6 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Viatu (makubazi) na kusikiliza maelezo kutoka kwa Bi Hadija Rashid wa Kikundi cha Wajasiliamali cha Vumilia Corporation kutoka Pemba, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 7 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kikundi cha Wajasiliamali Walemavu cha Women Clief Mafinga, Fatina Kangessa, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR 8Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Program kuendeleza Ujasiliamali kwa Wanawake, Noreen Toroka, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR
9Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Picha na OMR
10Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali na wageni waalikwa katika maonesho hayo. Picha na OMR 11Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali na wageni waalikwa katika maonesho hayo. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment