BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Arusha limemtaka wakala wa
usambazaji wa umeme vijijini (REA)kuhakikisha kuwa vijiji vyote
vilivyoko kwenye mpango wa kupatiwa umeme vinapata kwa wakati kwani
kwa sasa mashimo yalichimbwa yanahatarisha maisha ya wananchi.
Mbali na baraza hilo kuwataka REA kufikisha umeme kwa wakati vijijini
lakini pia wanatakiwa kuifanya jamii iweze kuwakubali tofauti na sasa ambapo wamechimba mashimo ya kusimamamishia nguzo na wameyaaacha.
Akiongea na katika baraza hilo la madiwani lililofanyika
jana mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saimon Saningo alisema kuwa
ni muda mrefu sasa umepita toka wakala hao wachimbe mashimo na
kuyaacha kama yalivyo jambo ambalo limewafanya wananchi kubaki na
malalamiko.
Amedai kuwa,mashimo hayo yanahatarisha sana maisha ya wananchi lakini pia hata mifugo ambayo ipo vijijini humo na kwa hali hiyo wananchi wamebaki wakiwa na manunguniko makubwa.
Ameongeza kuwa endapo kama muda wa kufikisha umeme vijijini haujafika basi REA wanatakiwa kwenda kufukia mashimo hayo na pindi watakapokuwa tayari basi watayafukua na kisha kusimamisha nguzo kwa ajili ya umeme.
Hataivyo ameitaka REA kuhakikisha kuwa wanashirikiana na madiwani
waliopo kwenye kata husika kwani takwimu za halmashauri hiyo
zinaonesha kuwa bado asilimia kubwa ya madiwani hawajui mradi huo
Amesema kuwa wakati mwingine wananchi wanashindwa kupenda na
kuthamini mradi huo kwa kuwa hawana hamasa kutoka kwa madiwani hao
hali ambayo wakati mwingine inasababisha fujo zisizo za lazima hasa
maeneo ambayo mradi huo umepita.
No comments:
Post a Comment