MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE MARA
MOJA, UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30, JINSI YA KIUME ALIUAWA KWA KUPIGWA
SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUKUTWA AKIWA AMEVUNJA
NYUMBA YA HUSSEIN HASHIM (22) TANYBOY NA KUIBA TSHS 400,000/=.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
28.10.2014 MAJIRA YA SAA 04:00 USIKU HUKO MTAA WA VIWANDANI, KATA YA
MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA MHANGA
BAADA YA KUMUONA MTUHUMIWA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA NA WANANCHI
KUJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA MAREHEMU. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA VAVA ZAKARIA, UMRI KATI YA MIAKA 50 -55
ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.439 BDV AINA YA KING LION ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE
28.10.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO MAENEO YA TAZARA, KATA YA
IYUNGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBEYA/TUDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA MARA
BAADA YA TUKIO HILO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment