Kuna taarifa katika vyombo vya
habarii liyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA ,kwamba
serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari kuu ya dawa
na kusababishia ukosefu dawa katika baadhi ya hospitali.
Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia dawa
, lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa kama
inavyoelezwa. Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na serikali imekua
ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari ya
dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza dawa.
Katika kukabiliana na hali hii hospitali zote kupitia waganga
wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia 50 ya mapato
yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.
Kuhusu ukosefu wa matibabu katika Taasisi ya Saratani ocean
road, ni kweli kwa sasa baadhi ya mashine hazifanyi kazi na zinazofanya
kazi ni chache hivyo kuzidiwa wakati fulani.Hatahivyo wizara imekwisha
agiza vifaa hivyo ambavyo ni ghali sana toka Canada na vinategemewa
kufika wakati wowote kuanzia sasa na pia ikumbukwe kuwa matibabu
yanatotolewa bila malipo na gharama zote ni za serikali.
Wizara kwa sasa imeagizwa katika mpango wa matokeo makubwa sasa
(BRN)ambapo wataalam wanamalizia kazi za utekelezaji wa mpango huo.
Ambapo pia umezingatia namna ya kukabiliana na jinsi ya kuhakikisha
dawa zinapatikana kwa wakati katika vituo vya matibabu na kuiboresha zaidi bohari ya dawa.
Baada ya kuanza utekelezaji huo suala la ukosefu wa dawa na vifaa tiba utapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Pamoja na wizara kupeleka bohari tyadawa pesa kwa ajili ya
ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hospitali zihakikishe zinapeleka asilimia
50 ya mapato kama zilivyoagizwa na kutokufanya hivyo kiongozi husika
atawajibishwa.
Mwisho wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba dawa na
vifaa tiba muhimu vinapelekwa katika vituo vyote , pia inaendelea
kufanya kazi na taasisi zote zisizo za kiserikali kwa karibu kwa faida
ya wananchi wote.
Imetolewa na :-
Dkt. Seif S. rashidi (Mb)
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII
27/10/2014
No comments:
Post a Comment