Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba
yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa
washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo
hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii
nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.
SERIKALI
ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama
moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030
katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam
kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa
kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya
Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.
Amesema
kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika
Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda
ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
Mkurugenzi
wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini
(ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali
za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini
zinazoendelea.
Balozi
Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi
hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa
Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la
kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo. Amesema kwamba
watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma
bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini
wa kipato.
Balozi
Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia
yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia,
utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya
kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa
upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward
Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa
yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya
wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo
tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania
imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya
ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja
za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la
kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
Mhadhiri
wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano
akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu
maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza
kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya
ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni
wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt
Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa
Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha
ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye
jamii
Amesema
kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha
kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za
kutimiza malengo ya milenia.
Mdau akichangia mada yake.
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
Wadau mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment