Makocha 35 wameteuliwa kushiriki
kozi ya ukocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
itakayofanyika mjini Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi
wa CAF, Sunday Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo
washiriki wote wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya
Kati (Intermediate) pamoja na vyeti vya kitaaluma vya elimu ya
sekondari (academic).
Washiriki wa kozi hiyo ni
Abdulmaliki Nemes (Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented Youth
Sports Centre), Ally Jangalu (Moro Kids), Amri Saidi (Mwadui FC),
Athuman Kambi (Morogoro), Charles Mwakambaya (Burkina Faso FC), Damian
Mussa (Alliance One) na Daudi Sichinga (Kasulu United).
Denis Maneva (Shule ya Msingi
Logo), Edgar Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi
Mtimbwilimbwili), Henry Ngondo (Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi
Kilimanjaro), Jumanne Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi
Alliance), Martin Saanya (Magereza Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine
University Academy).
Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage
Kabange (Kagera Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon
(Kishoto FC), Nyamtimba Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo
(Makongo), Rashid Abdallah (Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino
Rangers), Safari Nyerere (Elimu Sports Academy) na Said Lyakuka (Kizuka
Stars).
Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20),
Simon Shija (Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting), Swalehe Allawi
Abdul (Alliance Academy), Yasin Bashiri (Kick Off Sports Academy) na
Zuberi Katwila (Mtibwa Sugar).
Wakati huo huo, kutakuwa na kozi
ya wiki mbili ya ukocha ya ngazi ya Kati (Intermediate) itakayofanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 29 mwaka huu.
Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).
No comments:
Post a Comment