Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stela
Manyanya akikagua bidhaa za wajasiliamali na waoneshashi kwenye viwanja
vya maonesho ya SIDO yaliyojumuisha mikoa mitano ya Njombe,Mbeya,Rukwa
,Katavi na Kigoma sanjali na kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya ukanda
wa ziwa Tanganyika ambayo,Katavi Rukwa na Kigoma yanayoendelea kwenye
uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa
……………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Rukwa.
Halmashauri za Wilaya zimeshauriwa kutenga maeneo ya uzalishaji
na kuendeleza maeneo maalum kwenye baadhi ya mipaka ili kuweza kupata
sehemu bora za kuuzia bidhaa za wananchi zinazozalishwa katika maeneo hayo.
Ushauri huo ulitolewa na waziri wa Viwanda na Biashara
Dkt Abdalah Kigoda katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stela Manyanya wakati wa ufunguzi wa maonesho
ya kumi na mbili ya Kanda ya Nyanda za Juu kusini ya wajasiliamali
wadogo na kati Mjini Sumbawanga.
Dkt Kigoda ameeleza kuwa bidhaa kwenye maeneo maalum na ya pamoja hususani ya mipakani kunasaidia katika kuleta ushindani na uboreshaji wa bidhaa.
Akasema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kulitumia
soko la AGOA na masoko mengine ambayo Serikali imeridhia ambayo ni Afrika Mashariki AECna lile la kusini mwa Afrika SADC.
Akashauri kufanya biashara halali na nchi jirani na kutunza kumbukumbu sahihi ya biashara zinazofanyika nchi za jirani na nchi ya Tanzaznia ili kuweza kuandaa sera mahususi za kuwasaidia.
Waziri Kigoda Katika Hotuba yake akasisitiza kwa Halmashauri
zote nchini kushiriki moja kwa moja katika Program ya SIDO ya ’Wilaya
moja Bidhaa moja’ ambayo inasisitiza kuwa kila wilaya iwe inatambulika
kwa uzalishaji wa bidhaa moja itakayotiliwa mkazo zaidi kuliko nyingine
zilizopo kwenye wilaya husika.
Hii ikiwa na maana kutoa kipaumbele kwenye upande wa kuendeleza
bidhaa kwa kuipa huduma zaidi kwenye upande wa kupata mafunzo
teknolojia,masoko na mikopo,lengo ikiwa ni kuongeza mapato na ajira kwa
vijana katika maeneo husika.
Pia Wafanya biashara, wajasiliamali na wasindikaji wa bidhaa wa
Mikoa ya Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na ule wa kanda ya ziwa
Tanganyika wametakiwa kuwa wabunifu katika kubaini nini kinahitajika na
mahali gani na lini wakati wa kuzalisha kadiri ya mahitaji ya soko.
Mikoa mitano ya Kanda ya nyanda za juu na ukanda wa ziwa
Tanganyika imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi na hali ya hewa nzuri
inayovutia na kufaa katika kuzalishaa bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ambapo bidhaa zinazotokana na maliasili,mifugo,na mazao ya
kilimo ambayo mikoa yote mitano ya kandahii imejaliwa ambayo ni Njombe
Mbeya, Rukwa Katavi na Kigoma ambapo Serikali inajitahidi kuweka
miundombinu ili kuwezesha huduma na bidhaa kusafiri kwa urahisi kutoka
mikoa hiyo kwenda kwenye mikoa mingine na nchi jirani za Zambia,Jamhuri
ya Kidemkrasi ya Kongo DRC,Burundi, Malawi na Rwanda, kwa kutumia
barabara na majini Maziwa Tanganyika,Rukwa na Nyasa, Ambapo ili kutumia
fursa hiyo wanatakiwa kuwa wabunifu katika kubaini mahitaji.
No comments:
Post a Comment