Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (watatu kutoka kulia) akiwa kwenye
picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya afya nchini mara baada ya kufungua
Kongamano la wadau hao leo jijini Dar es salaam.Wengine kushoto ni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO_Dar es salaam.
Makamu wa Rais Dk. Mohemed Gharib Bilali akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii
Dk Seif Rashid leo Jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano la wadau
wa Sekta ya Afya lililofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wadau wa Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya wakiwa wanamsikiliza
mgeni rasmi ambaye ni makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………….
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali imesema itaendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini
kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hosipitali za Rufaa zote nchini ili
kuhakikisha wananchi wanapata matatibu bora na yanayoridhisha.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais
Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati akifungua Kongamano la wadau wa Afya
nchini.
Amesema kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati katika kuhakikisha
kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za afya ili apate muda mzuri wa
kuchangia shughuli nyingine za maendeleo akiwa mzima.
Dkt. Bilali ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa motisha kwa
watumishi wa Sekta ya afya ili waendelee kutoa huduma bora za afya kwa
wananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif
Rashid amesema Tanzania ni moja kati ya nchi nne barani Afrika
zilizoweza kufikia lengo namba 4 la malengo ya millennia katika utoaji
wa huduma bora za afya.
Amesema kuwa hatua imefikiwa baada ya Wizara hiyo kuamua
kuanzisha idara maalum itakayohusika kuangalia ubora wa huduma
zinazotolewa hapa nchini ili kuongeza tija katika Sekta ya Afya kwa
kuwapa Wananchi huduma bora zinazokidhi vigezo.
Ameongeza kuwa kwa wale wanaofanya vizuri katika kutoa huduma za Afya watatambuliwa kwa mchango wao katika kutoa huduma bora.
Dkt. Rashid ametaja vigezo vinavyotumika katika kuwapata watoa
huduma za afya kuwa ni kutoa huduma inavyotakiwa,kutumia utaalamu sahihi
katika kutoa huduma hiyo na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika
kutoa huduma za afya.
Aidha Dkt. Rashid ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa
kupitia mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma
bora za afya.
Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya limehusisha wadau zaidi ya
300 kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali
na linafanyika kwa muda wa siku mbili ambapo baadhi ya wadau
walitambuliwa kwa kutoa huduma bora za Afya ni kama vile Hosipitali ya
Rufaa Mbeya,KCMC, na Bugando.
No comments:
Post a Comment