MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga,
amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema, kuwa
Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la
Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014). Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo
umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo
huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na
vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika
kuvua taji ili awe huru.
“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana
na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili
taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru
ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua
taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee
na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili
ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.
Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa
hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu
kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20
mwaka huu. “Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa
hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji,
ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa
kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo na bado tunamtambua kuwa
mrembo wetu,” alisema Lundenga.
Kwa upande wa mama wa mrembo
huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si
za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho,
badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji
hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya
ya mitandao.
No comments:
Post a Comment