Pichani
juu na chini ni baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja
wa Mataifa na watoto wa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa walipojumuika pamoja mwishoni mwa juma
kushiriki michezo mbalimbali kwenye UN Family Day kusheherekea maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanishwa kwake.
Watoto
wakifurahia kupakwa rangi usoni katika bonanza la UN Family Day ikiwa
ni shamra shamra ya maadhimisho ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Timu
ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (jezi za blue bahari) na timu ya
wafanyakazi wa Wizaya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakimenyana uwanjani kwenye UN Family Day iliyofanyika mwishoni mwa juma
kwenye viwanja vya michezo Gymkhana ambapo timu ya Umoja wa Mataifa
iliibuka kidedea kwa kuinyika timu ya Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa bao 3-0.
Wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa wakishangilia ushindi baada ya kuibuka kidedea
kwenye mechi ya kirafiki na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa
Kimataifa katika kwenye bonanza la UN Family Day lililofanyika mwishoni
mwa juma.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Maendeleo (UNDP) Bw. Philippe Poinsot nao walijumuika na wafanyakazi
wenzao katika UN Family Day kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt Natalia Kanem (mwenye t-shirt nyeupe) akiteta jambo na
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye
bonanza la UN Family Day wakijiandaa na zoezi la kukabidhi medali kwa
timu zilizocheza mechi ya kirafiki.
Kutoka
kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem, Mwakilishi Mkazi wa
FAO, Diana Templeman, Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani
(WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora na Mratibu Mkazi wa mashirika
ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakipata picha ya pamoja kabla
ya kukabidhi zawadi kwa timu zilizomenyana kwenye bonanza la UN Family
Day.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwavisha
medali timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
iliyonyukwa bao 3-0 .Kulia ni Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.
Kapteni
wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye
picha ya pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa mara baada ya
kukabidhiwa kikombe.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akikabidhi kikombe kwa
Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza iliyoibuka kidedea
kwenye mechi ya kirafiki bonanza la UN Family Day.
Kapteni
wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza akifurahia kikombe
walichokabidhiwa baada ya kuitandika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa bao 3-0.
Tatu
bila tatu bila…….Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO)
nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora akijumuika na timu ya Umoja wa
mataifa kushangilia ushindi huo huku wakiimba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akifurahi jambo
na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani
(WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora kwenye bonanza la UN Family Day
ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa
tangu kuanzishwa kwake.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa
UNDP, Bw. Titus Osundina.
UN
Care waliweka mabanda kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ikiwemo ya Uzazi
wa mpango, Ugonjwa Ebola, Upimaji wa VVU na ushauri nasaha, kansa ya
matiti na mengine mengi kwenye bonanza la UN Family Day lililofanyika
mwishoni mwa juma.
Watoa
huduma za afya wakifanya kipimo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa waliohudhuria bonanza la UN Family Day kusheherekea miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mtoa
ushauri nasaha na upimaji wa VVU kutoka Angaza (kushoto) akimsikiliza
na mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kabla ya kumfanyia vipimo.
Petra
Karamagi wa ofisi za Mratibu Mkazi akibadilishana mawazo na MC wa UN
Family Day, Usia Nkhoma Ledama kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar.
No comments:
Post a Comment