TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, October 27, 2014

HABARI ZILIZOTAWALA SIKU YA JANA JUMAPILI KATIKA VYOMBO VYA HA HABARI HIZI HAPA

Serikali yapiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake

unnamedWaziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonwa waliofuata huduma katikazahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru ,juzi  alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu tozo ya ushuru wa magari na wagionjwa wanaopita katik Hifadhi ya Taifa ta Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed1Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtaarifu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu juu ya adha wanayopata wananchi wa jimbo klake wakati wakiiingia katika Zahanati ya tiba za Asili cha Ngarenanyuki mkoani Arusha juzi , kutokana  na tozo la pesa kupitia hifadhi ya Taifa ya Arusha. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed2Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na Mbunge wa Siha ambaye ni Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri wakikagua kitalu cha miti katika shamba la mitiulioko wilayani humo juzi. Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme n akuondoa mgogoro uliozuia mradi huo kwa muda mrefu.
unnamed3Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri akiwa na wataalamu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakikagua msitu wa Siha mkoani Kilimanjaoro alipotembelea juzi . Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme.
……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani Siha juzi ,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema
Nyalandu alisema kasi ya ukataji miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.

“Kwa kaddri siku zinavyozidi kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.

Aliwaagiza wakuu wa wilaya za Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa  hadidu za rejea kwa ajili ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha mfuko huo.

Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.

Alisema kwamba kwa msitu wa asili kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho alishauri  umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.

Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni kama nishati na kulinda misitu.

“Umemem ni nishati mbadala badala ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala” alisema.
===================================================================

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUOMBA MKOPO POLAND

PG4A6900
*Ni wa kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia chakula
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kupata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland utakaoliongezea Taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.
Alisema uzalishaji mwaka huu umetoa ziada ya tani milioni 1.5 za nafaka na tani 800,000 za mpunga ikilinganishwa na ziada ya tani 300,000 iliyokuwepo mwaka jana. “Serikali inakabiliwa na changamoto ya kupata soko la uhakika kwa mazao ya wakulima kwa sababu tulizoea kumtumia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kama mnununzi mkuu na uwezo wezo wake ni tani 240,000 tu kwa mwaka,” alisema.
Akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya MLYNPOL ambayo inanunua mazao kwa wakulima na kusindika nafaka jana mchana (Ijumaa, Oktoba 24, 2014) Waziri Mkuu alisema teknolojia ya ujenzi wa maghala makubwa ya kuhifadhia chakula katika muda mfupi ndiyo suluhisho pekee kwa wakulima wa Tanzania katika kipindi tulichonacho.
“Wenzetu wana teknolojia ya kisasa ya ujenzi wa SILOS (maghala makubwa ya kuhifadhia chakula) pamoja na namna bora ya kuhifadhi chakula, na sisi tuna changamoto ya kuwasadia wakulima kuuza mazao kutokana na uzalishaji mkubwa wa nafaka ambao umetokea mwaka huu,” alisema.
Alisema ni mapema mno kujua kiasi cha fedha ambacho Serikali inatarajia kukopa lakini alithibitisha kwamba atatuma timu ya wataalamu kutoka sekta husika ili wafanye mazungumzo rasmi na Serikali ya Poland na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa mkopo huo.
Waziri Mkuu ambaye alisafiri km. 500 kwenda mji wa CHOJNOW kilipo kiwanda cha kutengeneza maghala (SILOS) na kusindika nafaka aliguswa na teknolojia inayotumika kwenye kiwanda hicho cha MLYNPOL ambapo kwa siku moja kina uwezo wa kusindika tani 360,000.
Mji wa CHOJNOW upo kusini Mashariki mwa Poland na pia hauko mbali na mipaka ya nchi za Ujerumani, Czeck na Austria. Kwa gari dogo ni kati ya saa 3 hadi 4 hadi kufika miji mkuu ya nchi hizo ambayo ni Berlin, Prague na Vienna.
Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, mmiliki wa kiwanda hicho kikubwa nchini Poland, Bw. WITOLD KARCZEWSKI alisema kiwanda hicho kinaposindika ngano kina uwezo wa kutoa unga laini wa mikate (refined flour), unga wa lishe (grain/brown flour), unga wa kutengeneza pasta na tambi na wa mwisho hutolewa kwa ajili ya chakula cha mifugo.
“Nafaka zikifika, zinasafishwa, zinakaushwa, zinapimwa unyevunyevu uliopo na kuanza kusindikwa kulingana na aina ya nafaka inayoletwa. Tunakusanya mazao haya kutoka kwa wakulima kwenye majimbo 16 ya nchi hii,” alisema.
Akifafanua kuhusu matumiai ya umeme kwenye kiwanda hicho, Bw. ALEKSANDR ZINGMAN ambaye pia ni mshauri na mbia wa Bw. KARCZEWSKI, alisema kiwanda hicho kinatumia megawati moja ya umeme kwa saa moja lakini matumizi yanaweza kupungua kuligana na ukubwa ama udogo wa kiwanda.
“Kama Serikali inahitaji kiwanda kidogo zaidi ya hapa, tunaweza kuwajengea na matumizi ya umeme lazima yatapungua,” alisema.
Kampuni ya MLYNPOL ina wafanyakazi 250 ambao kato yao, 200 wanafanya kazi kiwandani kwa shifti tatu za saa nane nane kila moja.
Waziri Mkuu anamalizia ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.
===============================================================

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA TREKTA POLAND

PG4A6832
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda atatuma wataalamu wa sekta ya kilimo ili waje kufuatilia suala la mahitaji ya trekta ili kuziba pengo la mahitaji yake nchini Tanzania.
Alisema lengo la Serikali la kuanzisha sera ya Kilimo Kwanza lilikuwa ni kuwasaidia wakulima kupata ruzuku ya pembejeo, mbegu bora, na dawa za mifugo ili waweze kuongeza ushalishaji.
“Kutokana na mkopo wa Serikali ya India, tulipata matrekta 1,846 ambayo hayakuchukua muda kuisha. Sasa hivi tunatafuta wabia wengine wa kutupatia zana za kisasa za kilimo kwa sababu matunda yake mazuri tumeyaona, tunataka kilimo cha Mtanzania,” alisema.
Jana asubuhi (Ijumaa, Oktoba 24, 2014), Waziri Mkuu alitembelea kampuni ya Farmers inayotengeneza vipuri pamoja na matrekta ya kulimia na kuvuna yenye ukubwa wa Horse Power 80 na 72 ambayo alielezwa kwamba yanavumilia hali ya udongo mgumu wa Afrika.
Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Farmer, Bw. ZDZISLAW ZUKIEWICZ alisema vifaa vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vina waranti ya miaka saba na vinaweza kuhimili udongo wa miamba na mawe wa ardhi ya Tanzania.
Kampuni hiyo inatengeneza matrekta, mashine za kuvuna mazao shambani (combined harvester), mashine za kukata nyasi za malisho ya mifugo pamoja na vipuri vyake. Alisema bei ya trekta ni wastani wa Euro 22,000 na wako tayari kuleta vifaa hivyo Tanzania kama watapewa oda.
Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.
==================================================================

POLAND WATAKA KITUO CHA BIASHARA

 PG4A6747
WAFANYABIASHARA wa Poland wameiomba Serikali ya Tanzania kuangalia uwezekano wa kufunguakituo cha biashara katika bara la Ulaya.
Wametoa ombi hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kikao kilichowashirikisha wafanyabiashara wakubwa 30 na wamiliki wa makampuni 20 wa hapa Poland kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Poland (Polish Chamber of Commerce) jijini Warsaw.
Walisema kuwepo kwa kituo hicho barani Ulaya kutawasadia wao kupata taarifa kuhusu Tanzania kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo hivi sasa ambao wanalazimika kwenda London, Uingereza.
Akijibu maombi yao, Waziri Mkuu alisema ombi lao ni la msingi na atawasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe kuona ni nchi gani kituo hicho kinaweza kuwekwa.
Kwa upande wake, Kaimu wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Bw. Christopher Mvula ambaye alimwakilisha Balozi Philip Marmo, alisema ili kituo hicho kiweze kuanza kazi, ni lazima pawe na jengo la ofisi za ubalozi, ofisi za kituo cha biashara na watumishi mahsusi. Balozi wa Ujerumani ndiye anayeiwakilisha Tanzania nchini Poland.
“Lazima kuwe na watumishi wa kituo lakini vilevile kuwe na Afisa Biashara, Afisa Utalii na Afisa Uhamiaji ili kuharakisha baadhi ya mambo. Siyo kila afisa wa ubalozi anaweza kuendesha kituo cha biashara,” alisema.
Alisema zitahitajika pia fedha za kulipia matangazo kwenye vyombo vya habari vya nchi husika pamoja na vipeperushi na taarifa nyingine za kuitangaza nchi kupitia kituo hicho.
Waziri Mkuu alimaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kukutana na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.
===================================================================

WAZALISHAJI MATREKTA WACHANGAMKIA FURSA TANZANIA

 PG4A6897
KAMPUNI ya URSUS ya kutengeneza matrekta ya kutoka Poland imeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania na iko tayari kushirikiana na kampuni ya SUMA JKT kutengeneza matrekta hayo.
Hayo yamesemwa na Rais wa Bodi ya URSUS, Bw. KAROL ZARAJCZYK wakati akitoa maelezo ya kampuni yake mwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokutana na wafanyabiashara wenye nia ya kuwekeza Tanzania jana asubuhi (Jumapili, Oktoba 26, 2014) kwenye hoteli ya Sheraton jijini Warsaw, Poland.
Bw. ZARAJCZYK alisema wanataka kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania kwa kutambua nafasi ya kijiografia ya mahali nchi ilipo kuwa ni fursa ya kufungua milango kwa nchi jirani za Afrika Mashariki na Kati.
“Barani Afrika tulianza kupeleka matrekta Ethiopia, Ghana na Guinea. Sasa hivi tumeamua kuja Tanzania na Zambia. Nia yetu siyo kujenga tu kiwanda bali pia kutoa huduma kwa wakulima juu ya uendeshaji na utunzaji wa hayo matrekta,” alisema.
Alisema wako tayari kutoa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania kama vile chuo fulani ili waweze kuunganisha matrekta hayo hapa nchini na waweze kuyafanyia ukaranati na kutengeneza vipuri vyake pindi ukitokea ulazima wa kufanya hivyo “Tunapenda kujenga kiwanda mahali ambapo itakuwa rahisi kupata vijana wa kuajiriwa au vijana wa kutoka chuoni ili iwe rahisi kuwafundisha pia teknolojia tunayoitumia kutengeneza matreka hayo,” aliongeza.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema atawasilisha maelezo yao kwa Waziri anayehusika na sekta hiyo ili mawasiliano rasmi yafanyike.
===================================================================

WAZIRI CHIKAWE ATANGAZA KUTETEA JIMBO LAKE

PIX 1
Na Felix Mwagara, Nachingwea WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe ametangaza rasmi kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake. Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa CCM wa Wilaya na Kata ya Mtua, wilayani Nachingwea katika sherehe ya kuwapokea viongozi na wanachama wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliojiunga na CCM wilayani humo. Waziri Chikawe alisema wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi kuacha kugombea nafasi hiyo kwani wazee na wananchi mbalimbali katika Kata zote alizokuwa akipita kufanya mazungumzo nao wanamuomba agombee tena nafasi hiyo. “Wakati nikiingia ubunge mwaka 2005 katika jimbo hili kulikuwa hakuna lami na barabara nyingi za kwenda vijijini zilikuwa hazipitiki na pia maji yalikuwa shida lakini sasa barabara za lami mjini Nachingwea zimejengwa, maji yanapatikana tena yasio na chumvi, barabara vijijini zinapitika kwa kuwa zimechongwa vizuri kwa kuwawezesha wakulima kupitisha mazao yao,” alisema Chikawe huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika katika sherehe hiyo. Picha/Story na Felix Mwagara.
=================================================================

WATOKA NJE YA KIKAO BAADA YA  KUKASHIFIWA

DV6A0360
Na Kibada Ernest –Nkasi.
Madiwani wanne  wa Halmashauri ya Nkasi Mkoani Rukwa kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA watatu na mmoja wa chama cha  Tanzania Labour Part waliamua kuchafua hali ya hewa pale walipotoka nje ya kikao cha Baraza la Madiwani kwa madai kuwa madiwani wa Chama cha Mapinduzi wanawatuhumu kuwa wanawachochea wananchi wagome kushiriki katika shughuli za Maendeleo.
Kikao hicho   cha siku mbili za cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi  kilichofanyika mwishoni mwa wiki kiliingia dosari baada ya madiwani wanne kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA- na mmoja kwa tiketi ya Tanzania Labour Party-TLP- pamoja na viongozi wao kutoka nje ya kikao kwa madai ya kukashifiwa na madiwani wa kata za Nkandasi na Kipande kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi –CCM kuwa viongozi  wa wIlaya wa vyama hivyo wanahamasisha  kupitia mikutano ya hadhara wanachama wao wasichangie  SHUGHULI ZA maende;eo hasa ujenzi wa vyumba vya maabara, Madiwani hao  walioamua kutoka nje wanatoka katika Kata za  Ninde,Kabwe, Kilando,Wapembe na Chala
 Akizungumza katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kila kata taarifa zilizokuwa zinasomwa na Wenyeviti wa Mabaraza ya maendeleo ya kata –WDC- ambayo wenyeviti wao ni madiwani wa kila kata husika Mwenyekiti wa Umoja wa Madiwani wa vyama vya upinzani Wilayani humo Diwani wa Kata ya Kirando kwa tiketi ya CHADEMA Kessy Sood alisema hakuna ushahidi wa kuthibitisha ukweli wa tuhuma hizo
Alisema tuhuma zilizotolewa na Madiwani wenzao Leonard Nakutaile wa kata ya Nkandasi na Peter Chele wa kata ya Kipande kuwa kulikuwa na maandamano ya wanachama wa CHADEMA kupinga utaratibu wa kukusanya michango kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kabla ya Nov. 15 mwaka huu kama ilivyoagizwa na Rais ni uchochezi unaoweza kuchangia kuleta mivutano ya kimasirahi ya kisiasa inayoweza kuathiri azma ya kusimamaia Maendeleo ya wananchi wa halmashauri kwa ujumla.
Ameeleza kuwa wao kama viongozi katika ngazi za Kata na Wilaya hawana maagizo yoyote kutoka ngazi za juu za vyama vyao yanayowaagiza kuwaeleza wanachama wao kususia ujenzi wa vyumba hivyo vya Maabara wala shughuli zozozte zile za maendeleo hivyo tuhuma hizo zinakipaka matope chama hicho na kuleta sura mbaya isiyo na uzalendo katika jamii
Continue reading →
==================================================================

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani yafanyika jijini Dar es salaam.

1Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) majukumu wanayotekeleza katika kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la Mgongo wazi na Vichwa vikubwa ikiwamo kutoa elimu bora kwa madaktari wanaosomea somo hilo, kwenda mikoani kutoa tiba kwa watoto wenye matatizo hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani  Jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi(ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
3Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimkabidhi Mama Dorcas Membe kitabu cha Mpango shirikishi wa Mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo Wazi jana na kumuomba kuwa Mlezi wa chama cha Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) ambapo ameahidi kushirikiana na chama hicho katika harakati za kukabiliana na Tatizo la Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi. kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Abdulhakim Bayakub.
4Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma cheti shukrani kwa mchango wanaoendelea kuutoa cha chama hicho ikiwamo kutoa matibabu kwa Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
6Baadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) = Jijini Dar es Salaam. 6BBaadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) jana Jijini Dar es Salaam. 7Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bi. Germana Gasper akitoa maaelezo kwa wananchi waliojitokeza katika banda wakati wa sherehe na kuwaasa wazazi hasa wakike waliokatika umri wa kubeba mimba kutumia vyakula vyenye vitamin ya Foliki kama maembe, Mchicha, Mihogo,machungwa, maharage, mahindi,mayai, ndizi, parachichi, papai, maini na kabichi, ili kukabiliana na tatizo la Kichwa kikubwa na Mgongo wazi kwa watoto wanaozaliwa
10Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
11Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam.
12Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani jana Jijini Dar es salaam
13Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
14Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
15 16

=================================================================

MBWEMBWE ZA STAND UNITED

Stand United wakiingia uwanjani na katapila tayari kucheza na Yanga, mwenye shati la kitenge hapo mlagoni ni Mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini amekuwa bega kwa bega na timu ya Stand United.
==================================================================

CHUO CHA TAALUMA ZA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA 21 AMBAPO WAHITIMU 280 WATUNUKIWA STASHAHADA.

01 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar Dkt. Abdalla Ismail Kanduru akitoa tamko la kuwatunuku stashahada wahitimu wa Chuo hicho katika Mahafali ya 21 yalifanyika Mbweni. 02Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Afya  Zanzibar wakila kiapo cha utiifu mbele ya mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi katika mahafali ya 21 yaliyofanyika chuoni Mbweni. 03Wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo hicho wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) baada ya kuwatunuku stashahada katika mahafali ya 21. 04  Wageni waalikwa walioshiriki mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar wakifuatilia maadhimisho  hayo yaliyofanyika Chuoni, Mbweni.06Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar katika Mahafali ya 21 yaliyofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na wa kwanza (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Dkt. Abdalla Ismail Kanduru. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment