TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Showing posts with label Shaaban Mpalule. Show all posts
Showing posts with label Shaaban Mpalule. Show all posts

Thursday, December 29, 2011

SAFARI YA ERASMUS LUNAGA-WAKATI WA MAZIKO YAKE NA JINSI ALIVYOWAACHA WATU KATIKA MAJONZI

 Hii ni Familia yake,
 Getruda Mongela akiweka udongo wakati wa salamu za mwisho
 Kaka wa Marehemu Erasmus Lunaga akiweka Udongo
 Mke wa Marehemu, Mama Lunaga akiweka Udongo wakati wa maziko
Mke wa Marehemu, Mama Lunaga akiweka Udongo wakati wa maziko
 Mtoto wa Marehemu, Richard Lunaga(kati) na ndugu yake Rede Mkama  wakati wakiwa kanisani
 Baadhi ya watu waliofika kuaga Mwili wa Mpendwa wetu, Baba yetu Erasmus Lunaga
Mke na Watoto wa Marehemu Erasmus Lunaga wakati wa maombezi katika kanisa la Roman Mbezi

Sunday, December 18, 2011

WEMA V/S JOKETI=PILATO

KWA HADITHI ILIYOTUFIKIA MUDA MFUPI FROM NOW NIKWAMBA KUNA MANENO ZIKO CHINI YA SAKAFU ETIIII!JOKETH ANAJIPANGA KUMBURUZA WEMA SEPETU MAHAKAMANI KWAA KUMCHAFUA...
NI vurugu mechi kati ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu (pichani) na namba mbili
wake, Jokate Mwegelo, mtifuano ni mzito lakini habari mpya ni kwamba sakata hilo linahamia kwenye mkondo wa kisheria.
Wema anamtuhumu Jokate kutoka kimapenzi na aliyekuwa mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’, kitu ambacho kimesababisha wamwagane.
Kwa mujibu wa rafiki wa Jokate, Wema atasimamishwa kortini siku chache zijazo kujibu tuhuma za kumchafua mrembo huyo.
THAT KUTOKA KWA bongo codes

Mr Blue Afiwa na Mama yake Mzazi.


Mr Blue Akiwa Unguja , Dakika 30 Baada Ya Kushuka Kwenye Stage Apata Taarifa Mama Yake Mzazi Amefariki .
Nikiwa kama (mdau) nawapa pole, Mr.Blue na familia yake na wapa pole kwa kuondokewa na mama ke Mr.blue,R.I.P!Mungu watie nguvu.
Pole Sanaa Ma Friend Mr. Blue.

Friday, December 9, 2011

WATANZANIA WATAKIWA KUWA MAKINI NA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA.

Na Lydia Churi- MAELEZO
Bagamoyo –PWANI.
WATANZANIA wametakiwa kutowapa nafasi watu wanaopotosha mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali washiriki mchakato huo kwa amani na utulivu.
Akizungumza na Vijana wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Bagamoyo leo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel  Nchimbi  amesema kuwa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya  Kikwete ana nia njema ya kuhakikisha kuwa watanzania wanapata katiba mpya baada ya kutimiza miaka 50 ya uhuru wa nchi yao.
Amesema taarifa zinazotolewa na serikali juu ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya ni za dhati na serikali ina nia njema katika hili hivyo wananchi hawana budi kuwapuuza wale wanaopotosha taarifa hizo.
Waziri  Nchimbi  amesema hayo wakati wa  uzinduzi wa  Mnara wa kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa TANU kitaifa uliofanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika mwaka 1954.
 Amewaasa  vijana kuwa Mnara huo usibaki kuwa kumbukumbu tu bali  wayafanyie  kazi yote yaliyofanywa na waliowatangulia.
Amewataka vijana kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa faida ya vizazi vijavyo na kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kutathmini kazi zilizofanywa na waanzilishi ili waweze kuwarithisha watoto wao baadaye.
Naye Katibu mkuu wa UVCCM Taifa, Martin Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo amewataka  vijana wa CCM kuwa na moyo wa kujitolea ili waweze kuliletea taifa  maendeleo.

Tuesday, December 6, 2011

KILIMANJARO STARS USO KWA USO NA UGANDA YATINGA NUSU FAINALI KWA KUINYUKA MALAWI 1-0

Timu ya Soka ya Kilimanjaro Stars, muda huu imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Michuano ya Tusker Challenge Cup kwenye Uwanja wa Taifa baada ya Nurdin Bakari kuifungia timu yetu ya Tanzania goli katika dakika ya 36 ya mchezo kipindi cha kwanza kwa shuti kali , lilikwenda moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango wa Timu ya Malawi.

kwa ujumla mchezo ulikuwa mkali na wa kusisimua, zaidi niipongeze timu ya Kilimanjaro Stars kwa kuonyesha kandanda safi ambalo watanzania wengi hawakutarajia kupata ushindi kama huo, pamoja na ushindi huo pia pongezi nyingi ni kwa mlinda mlango wa Kilimanjaro Juma kaseja kutokana na kuonyesha umahiri mkubwa katika kulinda lango.

pamoja na mabadiliko ya hapa na pale lakini hadi mwisho KILIMANJARO STARS 1-0  MALAWI, ambapo sasa kwenye Nusu Fainali timu ya Rwanda itakutana na Timu ya Sudan, wakati Kilimanjaro Stars wenyeji watakutana na Timu ya Uganda.

Monday, October 10, 2011

PERUGINA INVESTMENT , SIDE WAY WAJITOKEZA KUDHAMINI MISS UTALII DODOMA

washiriki Miss Utalii Dodoma, wakigonganisha Glass na Mkurugenzi wa Side Way Lodge, Valley Marandu. Muda Mfupi baada ya Kutangaza Udhamini wake ambapo warembo watalala kwa Kipindi chote cha Kambi.
Fainal za Miss Utalii Mkoa wa Dodoma zimepangwa kufanyika kwenye ukumbi Mpya wa Kisasa wa CLUB LA AZIZI,  ikiwa ni mabadiliko ambayo yamefanywa baada ya Mkoa wa Dodoma kutaka kufanyika kwenye ukumbi kutokana na kuwa bora kwa sasa ikilinganishwa na kumbi zingine za mkoa huo.
katika onyesho hilo ambalo awali lilipangwa kufanyika ukumbi wa new Dodoma hotel,  maandalizi yanaendelea kwenye ukumbi wa New Dodoma Hotel na warembo wote wako katika hali ya ushindani ambapo baadhi ya wadhamini wanazidi kujitokeza kusaidia fainal hizo.
Baadhi ya wadhamini walijitokeza ni PERUGINA INVESTMENT CO. LTD, SIDE WAY LODGE, Warembo  wanaoendelea na mazoezi ni pamoja na Jackline Leshange,Bahati Mwinyi,Martha Simon,Elizabeth Ayoub,Magreth Kapelle, Jazila Maulid, Agnes Stephan, Lucy Charlecy, Khadija Ally, Kija Masanja, Tausi Shaaban,Kibibi Aman, Nyabitage King'ala, Joyce Mwakibinga, Axer Peter, Nelly  Fabian Angelo,Anna Gisbert, Janet John, Julieth Katunzi, Ester George, Mary Wilson, Jenifer Kayanda, Bety Magawa,  na  Jackline John , chini ya jopo la wakufunzi(Walimu), ambao ni Miss Utalii Njombe na Balozi wa Hifadhi ya Taifa  ya Kitulo 2010/2011, Neema Isdory, Miss Utalii Tabora na Balozi wa Utalii wa Ndani, Sweet Maliwa,  Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Kati, Tabia Msuta.

Washindi katika Fainal hizo wataungana na Washindi wa wenzao wa Mikoa ya Singida, Tabora, pamoja na Katavi kuunda Kanda ya Kati iliyopangwa kufanyika mwezi wa kumi na mbili kati ya Mkoa wa Dodoma na Tabora.
Katika Onyesho hilo Mgeni Rasmi anatazamiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa huo ambao ni Wageni waalikwa, Afisa Utamaduni Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mkuu wa jeshi la Polisi Dodoma, pamoja na Maraisi wa Vyuo vya Wanafunzi vilivyopo Dodoma.
Wengine  waliojitokeza kudhamini Fainal hizo  Mpaka sasa ni Pamoja na, Kifimbo FM Radio kwa Upande wa (Matangazo), CLUB LA AZIZI,  Asante Water(Maji ya kunywa Washiriki),Ngoto Feniture, Royal Village, Clouds Fm Radio, TANAPA, Ngorongoro Creater, VETA Hotel, Shabibi Bus Service.
wengine ni Tanzania Daima & Sayari News Paper, Image Masters, Papaa Msofe, Zoizzuu Fashion, Dar City College, Kumekucha Action Mart, Viovena & Co LTD, Haji  Mapoda cosmetics pamoja na waheshimiwa Wabunge wa Dodoma.

Fainal za Miss Utalii Tanzania 2011/2012 Maanadalizi yake yanaendelea katika mikoa yote ya Tanzania ambapo Fainal za Taifa zimepangwa kufanyika pia Katika Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya washiriki Miss utalii Dodoma 2011,wakiwa katika Pozi kwenye kambi yao SIDE WAY LODGE.

Monday, September 26, 2011

Waliosoma Kusini waaswa kuchangia elimu

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Lindi Mjini, Salum Baruany amewashauri watu waliowahi kusoma katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania kushirikiana katika kufanikisha tamasha la kuchangia maendeleo ya elimu kwa ajili ya mikoa hiyo.
Baruany aliyasema hayo juzi katika kikao cha maandalizi ya tamasha la kuchangia maendeleo ya elimu kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kilichofanyika Ukumbi wa Imasco, Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiwa mmoja wa waalikwa wa vikao hivyo vya kila wiki, Baruany alielezea kukunwa kwake na ubunifu wa baadhi ya wanafunzi walioamua kuwahamasisha wenzao kukumbuka walikotoka kielimu, kwa lengo la kuwainua wengine.
“Nawapongeza sana. Ni wachache wanaoweza kukumbuka walikotoka, hasa kielimu. Hapa mmelenga, mikoa ya kusini iko nyuma kielimu, naamini wa kusaidia kupandisha hadhi ni ninyi wenyewe mliosoma kule na wadau wengine wanaoguswa na suala hili.
“Msikate tamaa, mtafanikiwa. Cha msingi ni kuwashirikisha na kuwashawishi wengine waliosoma ana kuwa karibu na mazingira ya kielimu ya mikoa hii. Nchi hujengwa na wananchi wenye moyo, nanyi kwa kuguswa kwenu, naamini elimu ya kusini itainuka kwa sababu ni vigumu mtu mmoja mmoja kuchangia na bado maendeleo ya kweli yakaonekana, bali kupitia mshikamano kama wenu,” alisema mbunge huyo.
Naye Mratibu wa tamasha hilo, Asanterabbi Mtaki, licha ya kumshukuru mbunge huyo kwa nasaha zake, aliwataka wadau wa elimu nchini kuungana na waliosoma mikoa ya kusini ili kufanikisha azma ya kuiinua kusini kielimu.
“Tangu awali tumeelezea hali ya elimu ya mikoa ya Kusini, kwa kweli si nzuri na inahitajika nguvu ya ziada, ndiyo maana tumeungana kuhakikisha tunafanikisha kitu kwa ajili ya shule za kusini na wanafunzi wake, hasa yatima, walemavu na wasiojiweza ili wapate haki ya kupata elimu bora,” alisema Mtaki.
Alisisitiza kuwa, kasi ya maandalizi ya tamasha hilo inaridhisha na kuongeza kuwa, nafasi ya waliosoma kusini kuchangia mawazo bado ipo, hasa kupitia vikao vya kila mwisho wa wiki vinavyofanyika ukumbi wa Imasco.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Mohamed Mpinga (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo baada ya kupatiwa na TBL msaada wa fulana na kofia vyenye thamani ya sh. mil. 10 kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yatakayofanyika mkoani Kagera kuanzia Oktoba 3-8, mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam juzi.
 

Na Gladness Mushi, Arusha Taasisi ya maendeleo ya jamii hapa nchini (CDTF) imefanikiwa kutoa msaada wa kimaendeleo, ambapo imechangia zaidi ya milioni 43 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu wa shule ya walemavu iliopo katika eneo la Ilboru Mjini hapa Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi vyumba hivyo vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu ambayo itatumika kwa watoto hao ambao ni walemavu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw Hendry Mgingi alisema kuwa watoto ambao ni walemavu kwa kuwa nao wana nafasi kubwa sana ndani ya jamii ya watanzania aidha aliendelea kusema kuwa wao kama taasisi ya maendeleo wamefikia uamuzi huo mara baada ya kuona kuwa watoto ambao ni walemavu wana nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidika hata kama wanaulemavu wa aina mbalimbali. aliongeza kuwa kama jamii ya watanzania itaweza kuwasaidia watoto hao ambao ni walemavu basi wataweza kufanya hata idadi ya wanafunzi ambao wana ujuzi mbalimbali kuongezeka kwa hali ya juu sana hapa nchini. "unajua endapo kama baadhi ya taasisi zitaweza kuona mchango ambao wanao hawa watoto walemavu basi hawa watoto wataweza kukua kwa kiwango cha hali ya juu sana na hata kama hawataweza kufanya kazi ngumu basi wanaweza kufanya kazi ambao ni raisi na hivvyo kusaidia jamii katika kutatua tatizo la ajira"aliongeza Bw Hendry hataivyo alisema kuwa walemavu wanaweza kuibua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuweza kutengeneza ajira ambazo zimo kwenye jamii kwa kuwa mpaka sasa baadhi ya walemavu wameonekana kuwa wabunifu wa hali ya juu sana. alisisitiza kuwa ubunifu huo ambao wanao baadhi ya walemavu utaenda sanjari na upokeaji wa vipaji kutoka kwa walemavu hao ambapo kama jamii ya leo itaweza kuwasaidia ni wazi kuwa kazi mbalimbali za walemavu zitakubalika na jamii ya watanzania. 'leo kuna baadhi ya walemavu ambao wapo tu lakini cha ajabu ni kwamba bado hawajaweza kusaidika lakini huu ndio wakati muafaka wa kila mwananchi kuweza kuwasaidia hawa walemavu kwa kuwa kwa kutowasaidia basi asilimia kubwa ya walemavu hao wanashindwa kutimiza ndoto za kuondokana na umaskini"alisema Bw Hendry. Alimalizia kwa kusema kuwa walemavu hao wanatakiwa kuhakikisha kuwa elimu ambayo wanapata wanaitumia vema katika kazi zao na masomo kwa kuwa ili napo waweze kufanikiwa ni lazima kwanza kuwepo na mipango mikakati ya elimu bora.

Maandali ya kuujenga Mkoa mpya wa Njombe

Mabweni ya wanafunzi
Jamii maskini kwa kawaida huwa na vipaumbele vingi. Matokeo yake ni kushindwa kuvitekeleza. Wananchi wa mkoa mpya wa Njombe ambao ni wachapa kazi kweli kweli wameikataa falsafa hiyo na wamejiwekea vipaumbele vichache na vya uhakika ili kuujenga mkoa wao. Vipaumbe vya wananjombe ni:
1. Elimu- Kwa kujitolea wananchi wa vijiji na kata za Katulila, Madobole, Miva, Lusitu, Mtila, Mbega, Matola, Luponde, Itulike, Ramadhani, Kihesa, Utalingolo, Ihalula, Nolle, Mamongoro, Makowo, Ng’elamo, Yakobi, Igominyi, Idunda, Idihani, Lugenge na Kiyaula wameamua kujikita katika suala zima la elimu kwa shule za awali, msingi na sekondari. Majenfo mzuri ya ya kisasa yako katika hatua mbali mbali. Ombi lao ni waalimu wa kutosha.
2. Afya: Ili kuimarisha afya wananchi hao wako katika mpango wa kuwa na zahanati katika kila kata. Tayari kwa kujitolea wameanza ujenzi wa zahanati hizo. Ombi lao ni kupatiwa wauguzi wa kutosha.
3. Kilimo: kutokana na hali ya hewa nzuri ya nyanda za juu kusini, wananjombe hawa wamejizatiti katika kilimo cha chai, mahindi, viazi mviringo na misitu ya mbao.
4. Miundombinu: kwa sehemu kubwa wananjombe wamejitahidi sana kutengeneza barabara za ndani na wanaamini ni kwa barabara nzuri wataweza kufaidika na fursa zitokanazo na migodi ya machimbo ya chuma na mkaa wa mawe ya Mchuchuma na Liganga
Kilimo cha chai Njombe
Ujenzi wa zahanati
Ujenzi wa kituo cha Afya

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein jana amefanya uteuzi wa nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee Rais amewateuwa Sheikh Saleh Omar Kabhi kuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar,Sheikh Khamis Haji Khamis kuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar ambapo Sheikh Hassan Othman Ngwali kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar.
Aidha Dk Shein amemteuwa Muumin Khamis Kombo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Zanzibar,Khalifa Hassan Choum kuwa Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Zanzibar, Abdulrahman Mwinyi Jumbe kuwa Mshauri wa Rais Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi .Pia Mwinyi Jumbe ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu wa Zanzibar.
Vile vile Rais amewateuwa Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa kuwa Mshauri wake katika mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji. Ramia aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Sweden na India pia alikamata nafasi mbali mbali za Uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Burhani Saadati Haji ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makaazi. Kabla ya Uteuzi huo Burhani aliwahi kuwa Waziri wa Kilimo pia Waziri wa Ardhi,Maji na Nishati.Pia Dk Shein amemteuwa Issa Ahmed Othman kuwa Mshauri wa Rais Utalii. Issa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza juzi

Pichani Juu na Chini Mgeni rasmi Hoyce Temu akiwapa risala wahitimu wa kidato cha IV katika shule ya Cambridge. Hoyce aliwasihi wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanafanya mitihani yao kwa utulivu na kujiamini sambamba na kuwasisitiza kuchagua masomo yenye masoko katika ajira na kujiendeleza binafsi. Aidha aliwaomba wazazi na walezi kuwasaidia vijana hao katika safari yao ya Maisha na kuwataka kuwa wavumilivu wakati wote ili waweze kufikia mafanikio.
Mwanafunzi Monica Mwaipopo akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Hoyce Temu cha kufanya vizuri katika taaluma na Vilabu Shuleni hapo.
Wahitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Cambridge wakiingia rasmi katika sherehe za mahafali yao kwa wimbo maalum. Sherehe hizo zilifanyika Shuleni hapo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali pamoja na ndugu na jamaa.
JAPO NI KIDOGO TUNAKUOMBA UZIWASILISHE KWA SESILIA, ndivyo anavyosema Meneja wa Shule ya Sekondari Cambridge Bi. Laura Mataita wakati akimakabidhi mgeni rasmi na Mwendeshaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Bi. Hoyce Temu.
Umati wa wageni waalikwa, walezi na wazazi waliohudhuria mahafali hayo ya kumi na moja shuleni hapo.
Meneja wa Shule ya Sekondari Cambridge Bi. Laura Mataita akihamisha uchangiaji wa fedha za Mtoto Sesilia Edward ambaye anasumbuliwa na maradhi ya moyo anayetarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu. Mtoto Sesilia aligundulika kufuatia kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Channeli Ten na kuendeshwa na Hoyce Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule hiyo.
 

Hatimaye lile shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Mara katika maswala ya utalii, litafanyika Ijumaa ya tarehe 07/10/2011, katika ukumbi wa Bwalo la Magereza mjini Musoma, ambapo takriban warembo 15 watapanda jukwaa moja kuchuana kumpata muakilishi wa mkoa katika mashindano yan Miss Tourism Lake Zone yatakayofanyika baadae mwezi december. Kampuni ya Stoppers Entertainment inayoandaa mashindano hayo, imejipanga kuyapa hadhi mashindano hayo ambapo warembo mbali na kupita jukwaani, watashiriki katika shughuli za kijamii, kuimba na kucheza ngoma za makabila ya mkoa wa Mara. Hata hivyo waandaji wamewaomba wadhamini kuendelea kujitokeza kudhamini shindano hilo, kutokana na kugusa utalii, utamaduni na uchumi wa nchi yetu, yote kwa minaajili ya kuitangaza Tanzania. Shindano la Miss Tourism Mara 2011, litasindikizwa na burudani kutoka kwa Ditto na Linah wote kutoka jumba la vipaji THT. Pia burudani za ngoma za asili zitakuwepo.

Na Mwandishi wetu
TIMU ya Leaders Club imeisambaratisha timu ya Bongo Movie bao 1-0 katika mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club jana.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kutokana na wachezaji wote kuonyesha viwango vya hali ya juu.
Leaders Club ikiongozwa na Doyi Moke, Adam Sapi, Christopher Semi, Baraka, Makoye, Juma Pinto, Idd Janguo, Abdul Tall, Michael, Kibwana Matephone na Charles Nyarusi walitawala mchezo huo ambao ulivuta mashabiki wengi kutoka kona mbali mbali za jiji.
Bongo Movie iliongozwa na Jacob Steve, (JB), Masoud Bitebo, Steven Nyerere na Vincent Kigosi ‘Ray’ ilishindwa kumudu kasi ya timu ya Leaders.
Baada ya kosa kosa nyingi, Leaders Club ilipachika bao la ushindi kupitia kwa Juma Tall kufutia ushirikiano mzuri na Adam Sapi na Juma Pinto.
Bao hilo liliwachangaya zaidi Bongo Movie ambao walipoteza ‘network’ uwanjani na kuanza kumvamia mwamuzi kila wakati wanapocheza faulo.
Tofauti na mchezo wa soka, mchezo huo ulionekana kuwa wa upande mmoja zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa Leaders Club.
Baada ya mchezo, timu ya Bongo Movie iliondoka mapema uwanjani hapo tofauti na awali kwani mara kadhaa huwa wanadumu uwanjani hapo kwa vinywaji na vitafunwa vingine.

AFISA Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Elias Msese akitoa maelezo kuhusiana na miradi ya nyumba inayoendeshwa na shirika hilo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Mazingira Abdulkarim Shah, katika viwanja vya Mashujaa vya Mnazi Mmoja kabla ya kufunga maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi jana. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Suzan Omari. (Na Magreth Kinabo - Maelezo ).

Na mwandishi wetu
WANAFUNZI wametakiwa kusoma kwa bidii ili kupata ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kumudu ushindani katika soko la ajira katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).
Pia, wameaswa kuacha kuiga tabia na tamaduni za kigeni ambazo mwisho wake zinaweza kuwaingiza kwenye vitendo vya kihuni ikiwemo uvutaji bangi.
Wito huo umetolewa jana na Meneja Utawala na Utumishi wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Lucas Kisasa, wakati akizungumzia kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Sekondari ya Actas, iliyopo Mbezi, Dar es Salaam.
Alisema kuwa soko la ajira kwa nchi wanachama wa EAC limekuwa na changamoto kubwa na kwamba, wanafunzi hasa vijana hawana budi kusoma kwa bidii ili kutoa upinzani kwa wenzao.
“Hakuna muda wa kupoteza kwa sasa, mnapaswa kusoma kwa bidii na maarifa ili kuweza kumudu upinzani katika soko la ajira. Hakikisheni mnafany vizuri kwenye masomo ili muweze kupata nafasi na kutumia fursa za ajira kwenye soko la jumuia yetu,” alisema Kisasa.
Pia, Kisasa alikemea tabia za baadhi ya vijana kuiga tamaduni za kigeni, ambazo zinakwenda kinyume na maadili ya Mtanzania.
Alisema kuwa uigaji huo umekuwa na madhara makubwa kwa vijana kutokana na wengi kujikuta wameangukia kwenye matendo ya kuhuni ikiwemo uvutaji wa bangi, ukahaba hivyo hawana budi kuwa makini.
Katika mahafali hayo ambayo ni ya tatu tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, Kisasa alikabidhi vyeti kwa wahitimu 264 kati yao wasichana wakiwa 147 na 117 ni wavulana.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na wazazi, walezi, wageni mbalimbali na majirani wanaozunguka shuleni hapo na wanafunzi, ambapo yalifana vilivyo kwa kupambwa na burudani za kila aina.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimshukuru Mbunge wa Rorya, Lameck Airo kwa kutoa mchango wa zaidi ya shilingi milioni 530 kwa shughuli mblaimbali za maendeleokwenye jimbo lake wakati alipozungumza na wananchi kwenye shamba la umwagiliaji la mpunga la Irienyi wilayni Roraya akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Septemba 22, 2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa umwagiliaji wa kilimo cha mpunga katika kijiji cha Irienyi wilayani Rorya akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Septemba 22,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WIZARA YA Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kwa makini ili kuhakikisha kuwa maeneo yote ya wazi yanarudishwa kwa wananchi ambapo matumizi yake yatakuwa kwa manufaa ya watanzania wote.
Aidha wizara hiyo imesema kuwa itatoa muda maalum kwa watu wote walivamia maeneo hayo kuondoka wenyewe na utakapokwisha muda uliopangwa itakuja kubomoa hivyo hakutakuwa na msamaha.(hakuna cha msalie mtume).
Kauli hiyo ilitolewa (leo) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah, wakati akifunga maonesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya wizara hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa, Mnazimmoja, jijini Dares Salaam.
Shah alitoa kauli hiyo ikiwa ni matazamio ya miaka 50 ijayo ya wizara hiyo huku akisema maeneo hayo yamepangwa kwa faida ya wananchi wote.
“Napenda kusisitiza kwamba taaluma ya upangaji miji inahitajika kutiliwa maanani na serikali haitakubali mipango hiyo kubadilishwa matumizi kiholela. Natoa rai hii kwa jamii kushirikiana na serikali kulinda maeneo ya wazi yaliyoko katika maeneo yao,” alisema Shah.
Aliwataka watendaji husika hasa wa halimashauri kutobalidilisha matumizi ya ardhi .
Aliongeza kuwa wizara hiyo imeandaa mikakati ya kuwa na mipango shahidi ya uendelezaji miji itakayokidhi mahitaji ya idadi kubwa zaidi ya watu watakaoishi mijini.
Pia kuwa na mipango itakayowezesha ujenzi wa miji nadhifu, ya kisasa na endelevu,kuzijengea uwezo halimashauri kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa miji na kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi kwa kila eneo la makazi nchini.
“ Wizara imedhamiria kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi nchini kwa matumizi mbalimbali pamoja na kupunguza gharama za upimaji, ambapo nchi itakuwa imejenga kituo cha kupokea na kusambaza picha za saltillite, vituo vingi zaidi cha upimaji vitajengwa,” alisema.
Makamu Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa wizara hiyo itaanza kutunza kumbukumbu za upimaji na ramani kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ambapo sasa inatumika mikoa 15 baadae itakuwa mikoa yote hadi wilayani kulingana na uwezo wa bajeti.
Alisema ili kuwawezesha wananchi kutumia ardhi kama mtaji wizara itahakikisha kuwa mashamba ya wananchi vijijini kote nchini yanabainishwa yanapimwa na wamiliki wake wanapewa hatimiliki za kimila.
Alisema kwa upande wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) limejipanga kujenga nyumba 150,000 katika kipindi cha miaka 50 ijayo na kujenga nyumba kwa ubia kwa kuwashirikisha wawekezaji wengine.

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe na maofisa wengine leo wakati
akiondoka New York kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya Marekani ambapo alihudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa na wa Diapora jijini New York na Virginia, Washington DC.
Picha na Ikulu
Rais Jakaya Kikwete akiagana na Mbunge wa Bukombe Profesa Kahigi huku Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii wa Zanzibar Mh Juma Duni Haji akiangalia leo wakati
akiondoka New York kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya Marekani ambapo alihudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa na wa Diapora jijini New York na Virginia, Washington DC.

IMBA YASHINDA 1-0 DHIDI YA MTIBWA SUGAR YA MANUNGU

Mshambuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akishangilia huku akiwa amembeba mchezaji mwenzake Amri Kiemba, mara baada ya kufunga goli dhidi ya timu ya Mtibwa Sugar ambao mpaka mpira unakwisha hawakupata goli, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo mpira umekwisha na Simba wameshinda goli 1-0. Ulikuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote kwani wamekuwa wakishabuliana na kukosa magoli mara nyingi pande zote huku magolikipa wakijitahidi kuzuia mipira ya hatari. Simba wamepata penati dakika za nyongeza hata hivyo beki wa timu hiyo Victor Costa amekosa penati hiyo baada ya golikipa wa timu ya Mtibwa Sugar Dida kupangua mpira huo.
KIjana Mpondela ambaye amevaa skafu nyekundu katikati akishangilia kwa nguvu na mashabiki wenzake wakati timu ya simba ilipopata goli la kuongoza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezaji Emmanuel Okwi wa Simba akikokota mpira mbele ya mabeki wa timu ya Mtibwa Sugar kabla ya kufunga goli katika mpambano huo.
Mchezaji wa Simba Gervas Kago akiongoza wenzake wakati wachezaji hao walipokuwa wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha Timu ya Mtibwa Sugar katika picha ya pamoja.
Kikosi cha Timu ya Simba katika picha ya pamoja.

Sunday, September 25, 2011

BONANZA LA UJIRANI MWEMA STAKISHARI LEO

Timu ambazo tayari zimefika ni pamoja na Kitunda na Ulongoni ambazo mchezo unaendelea, Mbagala ambayo itaingia uwanjani muda mfupi kucheza na timu ya Makangalawe kabla ya Timu za Tabata dhidi ya Vituka kuinmgia kupepetana, mchezo mwingine ambao unatazamiwa kuwa mkali kutokana na Timu Mwenyeji ambao ni Staki shari kuikaribisha Timu ya Wadhamini Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kUPITIA KINYWAJI CHAKE CHA KILIMANJARO.

Michezo Mingine itakayofuatia ni kati ya Timu za Kunduchi, Charambe, Bandari, Kigamboni, Skopioni, na Vingunguti 

Kwamujibu wa Waandaji wa Mashindano hayo Meneja Emmanuel Urembo amesema kuwa Kila Timu imepangwa kucheza mchezo mmoja kutokana na kubanwa na Ratiba ya mashindano na Mshindi wa Kila mchezo atapatiwa zawadi kutoka kwa wadhamini wa michezo hiyo

Lengo kubwa la mashindano ni kuimarisha wachezaji wa zamani, kuimarisha na kukuza vipaji vya wanamichezo kupitia wachezaji hao ambao kutokana na kutambua Soka ni chachu ya kupatikana kwa wachezaji ikiwa ni sehemu ya Burudani kutokana namajukumu ya kila siku.

Mchezo uliopo Dimbani kwa sasa Timu ya Ulongoni Inaongoza kwa Mabao 3-0 ambayo yamepachikwa kipindi cha kwanza na bado mpira Unaendelea isipokuwa mchezo ni mzuri na timu zote zinashambuliana kwa zamu.









Saturday, September 24, 2011

Rais wa Zambia akubali kushindwa

Rais wa Zambia Rupiah Banda amekubali kushindwa kwake na kiongozi wa upinzani Michael Sata.
Bw Sata, aliyegombea urais mara nne, alitangazwa kuwa mshindi usiku baada ya kupata asilimia 43 ya kura zote.
"Watu wa Zambia wamezungumza na lazima sote tusikilize," Bw Banda aliwaambia waandishi wa habari, huku akifuta machozi baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Chama chake cha Movement for Multiparty Democracy kimeongoza Zambia kwa miaka 20.
"Nikizungumza kwa nafsi yangu na chama changu, tunakubali matokeo. Sisi ni chama cha kidemokrasia na hakuna namna nyingine yeyote ile," Bw Banda alisema.
Siku ya Alhamis, kulikuwa na ghasia eneo la kaskazini lenye migodi zilizofanywa na wanaounga mkono upinzani wakiwa hawana subra na matokeo ya Jumanne.
Matokeo hayo yalitangazwa huku majimbo saba yakiwa bado kura zao kuhesabiwa, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema Bw Banda hatoweza kumfikia Bw Sata.
Mwandishi wa BBC Louise Redvers kwenye mji mkuu, Lusaka, alisema kuhusu tangazo hilo, wasiwasi uliogubika matokeo hayo ulisababisha makelele huku wafuasi wa Patriotic Front wakishangilia ushindi wao.
Maelfu ya watu walifurika nje ya geti lenye ulinzi mkali wakipiga ngoma, wakipiga honi na kupeperusha bendera.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Rais Mstaafu wa Zambia,Mh. Ruphia Banda kwenye ofisi za Mahakama Kuu ya Zambia wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Michael Sata zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia.
(Picha na Amour Nassor VPO).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,John Tendwa kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata mjini Lusaka jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mama Asha Bilal (kulia) na Rais mstaafu wa Zambia Ruphia Banda, wakimsikiliza Rais mpya wa Zambia Michael Sata alipokuwa akijitambulisha kwa viongozi wakuu wa Nchi mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
katikati ni Mama Asha Bilal.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) na mkewe Mama Asha Bilal (wa pili kushoto), Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa (kushoto) na Rais wa kwanza wa Zambia,Dkt. Keneth Kaunda wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana kwenye sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilala akisalimiana na Rais wa Malawi,Bingu wa Mutharika walipokutana kwenye Ofisi za Mahakama Kuu mjini Lusaka Zambia jana wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata