Mahmoud Ahmad Arusha
Mbunge
wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema ameachiwa huru kwa dhamana na
mahakama ya hakimu mkazi baada ya kusota rumande kwenye kituo kikuu cha
polisi kwa siku tatu kwa kosa la kuchochea vurugu chuoni uhasibu huku
baada ya kutoka akiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kumzomea
mkuu wa mkoa.
Lema
alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa Tatu na robo asubuhi akiwa
chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa mbele ya hakimu Devotha Msele
na ndipo mwendesha mashtaka Eliang’enyi Njiro alisimama kuanza kumsomewa
mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani
aliyoyafanya kwenye eneo la chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha.
Baada
ya kutoka mahakamani hapo alielekea kwenye ofisi za chama hicho na
kuzungumza na waandishi wa habari huku akitoa malalamiko na kuwataka
wanachama na wapenzi wa chadema kumzomea mkuu wa mkoa iwe
kanisani,mskitini,au kwenye sherehe mbali mbali,
“Nawatakeni
kumzomea huyo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo na kuwa nia ya kumshtaki ipo
pale pale ndugu zangu Makamanda wenzangu huyu jamaa awe msikitini
kanisani kote tumzome hiyo itakuwa ndiyo salamu yetu kwake”alisema Lema
Katika
hali nyingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi tangu nje ya mahakama
hadi ndani ya mahakama hiyo kiasi utulivu katika mahakama hiyo
ulionekana na shughuli kuendelea bila bughaa.
Hali
kwenye mitaa mbali mbali ya viunga vya jiji la Arusha ilionekana
kuendelea na mishughuliko ya kila siku kama kawaida kuliko ilivyokuwa
ikionekana huko mwanzo kwenye kesi zilizokuwa zikimkabili mbunge huyo
kwa wakazi wa jiji hili kuacha shughuli zao na kuelekea mahakamani
kufuatilia kesi ya mbunge huyo.
No comments:
Post a Comment