Zaidi
ya wanafunzi 750 katika shule saba za wilaya ya Singida zitapokea
msaada wa madawati yaliyotolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya
Hassan Maajar Trust na Shirika La Nyumba La Taifa
Jumla
ya madawati 264 yanatolewa na wabia hao kupunguza tatizo sugu la upungu
wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao,
imefanyika katika Shule ya Msingi ya Munisa, iliyoko Halmashauri ya
Singida.
Bwana
Shariff Maajar, kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust
akishirikiana na Bwana Nehemiah Mchechu kwa niaba ya Shirika La Nyumba
La Taifa, walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr.
Parseko V Kone.
“Napenda
kutoa shukurani za dhati kwa Wakfu wa Hassan Maajar na Shirika La
Nyumba La Taifa kwa msaada hu mkubwa utakaochangia kuboresha elimu
Singida’, alisema Dr. Kone.
Wanafunzi
mkoani Singida, hususan, walioko vijijini wanakabiliwa na changamoto
kubwa la kwanza likuwa mazingira ya kusomea, hivyo tunafarijika kuona
wabia wanotusaidia kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wetu. Hii
inakuza viwango na kuhimiza matokeo bora”, aliongeza.
Chini
wa mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For
Every Child) mkoa wa Singida wa pili kati ya mitano itakayonufaika kwa
msaada inyaotelewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha
zilizopatikana na michango iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa
Desemba 2011. Garama za madawati haya ni Tsh 22,500,000, kati ya hizo
Shirika La Nyumba La Taifa limetoa jumla ya Tsh 10,000,000.
“Tunataka
kuhakikisha kuwa kampeni ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia watoto
wengi iwezekenavyo na kujenga maisha bora kwa watoto hao”, alisema Zena
Tenga, Mkurugenzi Mtendaji. “Tunashukuru Shirika La Nyumba La Taifa kwa
kuunga mkono juhudi zetu. Tutaendelea kuhamasisha ushirikiano na wote
wenye nia ya kuona lengo la Hassan Maajar Trust la kuhakikisha watoto
wetu wakiondoka sakafuni na kukaa kwenye madawati lina timia”,aliongeza.
“Tunafurahi
kuona kwamba mchango wa shirika letu sasa uko katika hali ya madawati
ambapo watoto watakaa na watafurahia masomo ‘, alisema Bw. Mchechu,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Nyumba La Taifa. , “ Shirika la Nyumba
La Taifa lilishirikiana vema na Taasisi ya Hassan Maajar Trust kuchangia
fursa hii adimu kwa wanafunzi na maendeleo ya elimu kwa ujumla”,
aliongeza.
No comments:
Post a Comment