Na Georgina Misama-Maelezo
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani
amewataka watumishi wa Umma kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kukuza
uchumi wa nchi.
Waziri
Kombani amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusu
majukumu ya watumishi wa Umma katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa
miaka mitano.
Alisema ubora au udhaifu wa utendaji wa serikali yoyote unahusishwa na ubora wa watumishi wa Umma.
“Uchumi
hauwezi kukua bila watumishi wa umma kufanya kazi vizuri, katika kukuza
uchumi tunategemea,kukua kwa uchumi pia kunategemea watumishi wa umma,”
alisema Waziri Kombani.
Waziri
Kombani alisema kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara,
Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo, ingawa inakabiliwa na
changamoto mbali mbali.
Pamoja
na changamoto hizo, Waziri Kombani amesema Serikali imekuwa ikifanya
juhudi mbali mbali ikiwemo, kupitia na kutafakari jinsi ya kufikia
malengo ya maendeleo yake kwa haraka zaidi
Alisema
changomoto zilizopo katika utumishi huo ni kuwa huduma zinawafikia
wananchi kwa polepole, zisizo na ubora mfano kumekuwa na ongezeko la
idadi ya wanafunzi wanaondikishwa katika shule ya msingi na sekondari,
lakini kuna tatizo la ubora wa elimu.
“Tunapo
sema uchumi wa nchi inatakiwa kumwangalia mtu wa ngazi za chini. Hivyo
mkutano huu utakuwa unajadili changamoto zilizopo na nini kifanyike,”
alisema.
Aidha aliongeza kuwa wakati mwingine wananchi wanalalamikia kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
Hata
hivyo Waziri Kombani ametoa wito kwa viongozi kutafuta majibu ya
changamoto zilizopo, ikiwemo ongozeko la idadi ya watu, matumizi ya
rasilimali na matumizi bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA).
Mkutano
huo wa siku mbili, unawashirikisha manaibu makatibu wakuu kutoka
wizara mbalimbali, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa Halmashauri,
wakuu wa taasisi za elimu ya juu , sekta binafsi na wadau wa maendeleo
kutoka ndani na nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment