Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas (kushoto) kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura akikabidhi sehemu ya msaada kwa baadhi ya watoto kutoka Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede kilichopo Buguruni Malapa cha jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa leo na Kampuni ya TTCL kwa ajili ya Siku Kuu ya Mwaka Mpya 2016.
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, December 31, 2015
WANANCHI WATAKIWA KUCHANGIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI
SERIKALI imesema kuwa haina mpango wakujenga nyumba za kuwapa Wananchi bure kutokana na gharama ambazo Serikali inagharamia katika ujenzi nyumba hizo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula (Pichani)wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).
Angeline amesema kuwa shirika la nyumba la Taifa linajenga nyumba kwaajili ya kuuzwa pamoja na kupangisha na si kuwapa wanchi bure.
Amesema kuwa gharama ya kujenga nyumba hizo inakuja katika maandalizi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu kama Barabara, Maji pamoja na Umeme.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC), Nehemia Mchechu amesema shirika hilo tayari limejenga nyumba za kutosha katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.Pia amesema katika nyumba za mikoani shirika hilo limeuza nyumba hizo kwa 40% hadi 50% huku akisisitiza zaidi kuendelea na Kampeni ya (Nyumba yangu, Maisha yangu) ili wananchi wawezi kumudu gharama za nyumba hizo.
Waziri akuta ‘ofisi nzima’ wako likizo
By Raymond Kaminyoge, MwananchiDar es Salaam. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amefanya ziara ya kushtukiza Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kukuta zaidi ya nusu ya watendaji wake wako likizo.Naibu Waziri huyo aliwasili ofisini hapo jana saa 8.30 mchana na kupokewa na mtunza kumbukumbu, Bahati Kassim ambaye ni mtumishi pekee
WADAU WA UJENZI WATAKIWA KULITUMIA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI ILI KUEPUKA MIGOGORO.
Na: Jovina Bujulu - MAELEZO.
Wadau wa Ujenzi wameshauriwa kutumia huduma za kitalaam zinazotolewa na Baraza la Taifa la Ujenzi ili kuepuka migogoro inayojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi nchini.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu ya baraza hilo katika utatuzi wa migogoro inayotokea katika maeneo mbalimbali.
Mhandisi Chamuriho amesema kuwa migogoro ya miradi ya ujenzi inayojitokeza mara kwa mara baina ya wadau husika hutokana na kukosekana kwa ushirikiano baina yao.
" Wadau wanatakiwa kushirikiana kulingana na makubaliano yao ili mradi husika ukamilike" Alisema na kuongeza kuwa tofauti kati ya wadau wa miradi ya ujenzi hujitokeza kutokana na ukubwa na ugumu wake.
Aidha, Dkt. Chamuriho amesema kwamba migogoro ya ujenzi isiposuluhishwa mapema hugharimu pesa nyingi, muda wa wadau na fursa za matokeo ya miradi inayojengwa.
"Ninajua njia mahususi ya utatuzi wa migogoro inayoajitokeza nchini ni kutumia mahakama ambayo mashauri yake huchukua muda mrefu, ili kuokoa muda huu, utatuzi mbadala katika ujenzi ni kulitumia Baraza la Ujenzi" alisisitiza Mhandisi Dkt. Chamuriho.
Akitaja majukumu mengine ya Baraza hilo amesema kuwa ni kutoa huduma za ushauri , usuluhisi wa migogoro, mafunzo, ukaguzi wa kiufundi, utafiti na kutoa machapisho ya kiufundi.
Alisema kuwa Baraza la Taifa la Ujenzi lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge na 20 ya mwaka 1976 na kuanza kutekeleza majukumu yake.
Wednesday, December 30, 2015
KAMPUNI ZA SIMU ZILIZOSHINDWA KUWALINDA WATEJA WAKE KITEKNOLOJIA ZACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA NA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA).
Subscribe to:
Posts (Atom)