Mkurugenzi
  wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto) akijadili jambo na  
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas  
Wambura mara tu kabla ya makabidhiano rasmi ya jengo la nymba  
atakayokuwa anatumia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
iliyoko eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo. 
Muonekano
  wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo litakuwa makazi ya Spika  
yeyote atakayeliongoza Bunge la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009 
 na limegharimu takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba 
rasmi  ya Spika wa Bunge Dodoma
   Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction Company
  ( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban Mwatawala (kulia) 
akitoa  maelezo ya ujumla kabla ya kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya 
Bunge  katika jengo hili. Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha Bw.
  Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na Teknolojia ya Mawasiliano wa
  Bunge Bw. Siegfied Kuwite, na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John
  Joel.
Bw. Siegfried Kuwite akitia saini makabidhiano hayo kwa niaba ya Katibu wa Bunge ambaye ndiye Mshitiri (client) wa jengo.
 Bwana Mwatawala akimkabidhi  Msanifu
  Majengo M. F. M Msangi (kulia) anyewakilisha Wakala wa Majengo ya  
Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa Mradi huu.
Picha zote na Prosper Minja-Bunge
No comments:
Post a Comment