Mkurugenzi
 Mkuu Mwandamizi wa  shirika la Millenium Challenge Account  Tanzania 
Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw.  Bernard Mchomvu akimkabidhi zawadi ya 
Khanga yenye nembo ya shirika hilo kwa  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia 
Stella Manyanya walipoonana ofisini kwa Mkuu wa  Mkoa wa Ruvuma Said 
Thabit Mwambungu (kulia) jana kujadili miradi ya barabara  
inayodhaminiwa na shirika la Millenium Challenge Cooperation (MCC) 
kupitia  Tanzania Millenium Challenge Account (MCA-T Dsm). (Pichana 
Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Shirika hilo linafadhili ujenzi wa
 barabara kuu za  lami zinazojengwa Mkoani Rukwa zenye jumla ya Km. 224 
kwa miradi ya  Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, na Laela-Sumbawanga. Kwa 
mujibu wa Bwana Mchomvu  miradi hiyo yote pamoja na changamoto zote 
kuzingatiwa itakuwa imekamilika  ifikapo mwezi June 2013 na barabara 
zote zitakuwa zimekabidhiwa kabla ya mwezi  wa nane 2013.
Kwa upande  wa Ruvuma shirika hilo
 linafadhili ujenzi wa barabara itokayo mjini Songea  kuelekea Wilaya ya
 Mbinga ambapo ujenzi huo unaendelea na unategemewa kukamilika  mwakani.
Hata hivo  Mkurugenzi huyo 
aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wanaoutoa  
kuwaeleimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa miradi hiyo na ulinzi wa 
vifaa vya  ujenzi kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi wa 
vifaa vya ujenzi  vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya wananchi na 
wafanyakazi wasiokuwa  waaminifu.
Kwa upande  wake Mkuu wa Mkoa wa 
Rukwa Injinia Stella Manyanya allishukuru shirika hilo kwa  jitihada zao
 za kuchangia maendeleo nchini. Aliwashukuru pia kwa hatua za hivi  
karibuni walizochukua kujenga daraja la Laela ambalo ni kiunganishi 
muhimu kwa  wananchi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku 
hususani kuwaunganisha na  kituo cha afya cha Laela.
Picha
 ya pamoja kati Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, Injinia 
Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa  Rukwa, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa 
Ruvuma Tarimo na wawakilishi wa Jumuiya ya  Millenium Challenge 
Cooperation (MCC) Bw. Carl Fickenscher Mkurugenzi  Mkazi nchini 
(kushoto) na Bw. Bernard Mchomvu Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa  shirika 
la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T  Dsm).

No comments:
Post a Comment