TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 1, 2013

Manispaa ya Kinondoni kuongeza kasi ya utatuzi wa migogoro ya ardhi


 
MANISPAA ya Kinondoni  imeahidi  kuongeza nguvu katika kushughulikia masula ya migogoro ya ardhi , huku pia ikiwataka wananchi kutoa ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya watu wote wanaokwenda kinyume na utaratibu uliopo.Akizungumza na jiji Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus Fwema alisisitiza kuwa katika  kukabiliana na migogoro hiyo, uongozi wa manispaa umekuwa ukichukua hatua za haraka kuhakikisha  viongozi na watendaji wanaojihusisha na migogoro na kashfa za ardhi wanachukuliwa hatua mara moja.
Alisema katika kuishughulikia migogoro hiyo, manispaa imekuwa ikiendelea kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kamati ya migogoro ya ardhi iliyoundwa kwa maelekezo ya Rais, hatua aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa imeweza kuleta mafanikio. 
“Hadi sasa migogoro iliyokuwepo imeshughulikiwa kwa asimilia 95 na kupatiwa ufumbuzi, kwa sasa migogoro iliyopo ni ile inayotokana na uvamizi wa ardhi unaofanywa na makundi ya watu kinyjme na sheria ambayo manispaa kwa kushirikiana na Serikali kuu imeendelea kuipatia ufumbuzi” alisema Fwema. 
Aidha alisema kumekuwa na mawazo potofu ya baadhi ya watu kwamba  manispaa hiyo imekuwa ikifanya upendeleo kwa wakubwa wakati wa uuzaji wa viwanja vyake, madai aliyosema kuwa si ya kweli na zaidi yamelenga kuichafua manispaa hiyo. 
“Madai haya si ya kweli ikizingatiwa kuwa katika kipindi kinachokaribia miaka 10 manispaa ya Kinondoni haijawahi kupima viwanja na kuviuza kwa wananchi kutokana na changamoto mbalimbali hasa zinazohusiana na utwaaji wa ardhi na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kugharamia fidia na upimaji” alisema Fwema.
Alisema manispaa kwa muda mrefu imekuwa ikihangaika kutafuta fedha za kupimia viwanja kutoka sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha na madhumuni ni kuvipima viwanja hivyo ili kukabiliana na ongezeko la ujenzi holela katika maeneo yasiyopangwa.
Kuhusu utoaji wa vibali vya ujenzi na kushughulikia maombi ya kubadili matumizi ya ardhi, Fwema alisema manispaa hiyo kwa kutumia wataalam wake, kabla ya kutoa vibali hivyo wameweka utaratibu wa kuhakikisha maombi yaliyotolewa, hayakinzani na matumizi yaliyopo na yaliyoidhinishwa katika mpango wa matumizi ya ardhi.

No comments:

Post a Comment