TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 26, 2013

MASHAUZI CLASSIC KUIZINDUA NAWINA RESORT MBAGALA KUU

Bendi ya Mashauzi Classic chini ya I sha Mashauzi imeandaa Uzinduzi Rasmi wa Ukumbi wa Nawina Resort Mbagala kuu baada ya Matengenezo kutokana na ajali ya moto iliyotokea mwanzoni
mwa mwaka huu.
akizungumzia Uzinduzi huo mkurugenzi wa Nawina Resort Marry Komba, amesema kwamba Matayarisho yamekamilika na Tayari Isha Mashauzi na Kundi lake wamekamilisha taratibu zote kuhusiana na Onyesho hilo la Uzinduzi siku ya jumamosi tarehe 29 mwezi huu.
"Kikubwa ninamshukuru Mungu kwa kuwezesha kukamilika kwa Ukumbi huu wa Nawina Resort, kama unavyojulikana ukumbi huu na wakazi wengi wa Mbagala Kuu, ndiyo pekee uliokuwa ukiwapatia burudani mbalimbali wakazi wa maeneo haya a Vitongoji vyake vyote, kwa hiyo nawaomba wakazi wa mbagala Kuu waendelee kuunga mkono juhudi hizi ambazo ni kiburudisho kwao, nachukua fulsa hii kuwakaribisha sana siku ya Ufunguzi ili waweze kufika kushuhudia Nawina Mpya chini ya Mashauzi Classic" alisema Marry Komba
Awali kabla ukumbi wa Nawina Resort aujaungua Moto, ulikuwa ni kati ya Miimili ya Burudani iliyokuwa ikiwapa raha wakazi mbalimbali wa Mbagala, ikiwa ni pamoja na Miziki ya Kizazi kipya, Miziki ya Bendi, Taarabu na hata vikundi vya Sanaa kutoka kwa wasanii mbalimbali hapa nchini.
kwa Upande wake Isha Ramadhani maaufu kama Isha Mashauzi amesema kwamba wamejipanga kufanya Onyesho kali na la kusisimua ambapo wakazi wa Mbagala Kuu na Vitongoji vyake wafike ili waweze kufurahia Burudani kutoka katika kundi lake," Nimejipanga vizuri kuhakikisha wakazi na wapenzi wangu tunafanya kitu kipya na siku hiyo nitawapa pia vitu vipya kwa kuwa ni siku ya Ufunguzi wa Ukumbi Mpya, maana hivi sasa Nawina ni mpya kwa hiyo tutaingia na nyimbo zingine mpya ambazo ni burudani ya kupendeza" alisema Isha Mashauzi
katika onyesho hilo ambalo linatarajia kuanza majira ya saa mbili za Usiku , kiingilia  kimewekwa cha kuridhisha ili kuwafanya wakazi wote wa mbagala kufika ili kupata burudani wakiwa nafamilia zao kwa shilingi 5000 tu.
Kuhusiana na Ulnzi wa mali za wote watakaofika, Usalama wa vyombo vya Usafiri , mkurugenzi wa Nawina Resort  Marr Komba alisema kuwa ulinzi ni wa kutosha kwa wote watakaofika siku hiyo.

No comments:

Post a Comment