TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 16, 2015

Mkutano Mkuu wa TASWA umepangwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro

imagesKAMATI YA Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana Dar es Salaam jana na kujadili masuala mbalimbali.     
A; MAFUNZO
Kikao kilikubaliana watafutwe wataalamu wa kuendesha mafunzo kwa kada mbalimbali za waandishi wa habari za michezo nchini ili kuongeza ufanisi katika namna ya kuripoti habari za michezo michezo mbalimbali.
Kundi la kwanza litakuwa la waandishi chipukizi ambao wapo chini ya miaka mitano katika taaluma, ambapo mafunzo yao yatafanyika Machi 25 mwaka huu Dar es Salaam yakishirikisha waandishi wa habari chipukizi 30 na wa kada ya kati 10.
Tayari TASWA imepata mdhamini wa mafunzo hayo na kinachofanyika hivi sasa ni uteuzi wa washiriki, ambapo wahariri wa habari za michezo watahusishwa kupendekeza washiriki kutoka katika vyombo vyao.
Wakufunzi wa semina hiyo watakuwa waandishi wa habari wakongwe, walimu wa uandishi wa habari na wataalamu wa michezo mbalimbali nchini. Jumatano Machi 18 TASWA itatangaza mdhamini wa mafunzo ya Dar es Salaam pamoja na majina ya washiriki.
 Awamu ya pili pia itafanyika Dar es Salaamwaandamizi ikihusisha waandishi wa habari za michezo wa kada ya kati 30 na waandishi wa habari waandamizi 10 na itafanyika mwanzoni mwa Mei mwaka huu.
Awamu ya tatu itahusisha waandishi wa habari za michezo waandamizi na wahariri wa habari za michezo na jumla yao itakuwa 40 na  itafanyika mkoani Mtwara Mei 29, 30 na 31 mwaka huu. TASWA ipo hatua za mwisho za mazungumzo na wadhamini wa mafunzo hayo ya Mtwara.
     B; MKUTANO MKUU
Mkutano Mkuu wa TASWA umepangwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine utajadili Rasimu ya Katiba mpya ya chama hicho.
 
Kamati ya Utendaji ya TASWA imeteua kamati maalum ya kushughulikia katiba hiyo, ambapo hivi sasa Katibu Mkuu anawasiliana na wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo na baada ya wote kupewa barua na kukubali uteuzi atatangaza majina hayo.
 
C: Kamati ya Faraja
 
Kikao kilikubaliana kuwa iundwe Kamati ya Faraja kwa ajili ya kuwafariji wanachama wake kutokana na matukio mbalimbali yanayowakuta ikiwemo ugonjwa.
Uamuzi huo umechukuliwa kwa nia ya kuhakikisha waandishi wa habari za michezo wanakuwa wamoja kwa shida na raha kwa vile wamekuwa kama ndugu.
Kwa kuanzia TASWA inawaomba wadau wote kushirikiana na kamati hiyo ambayo jukumu lake la kwanza itakuwa kumsaidia mwandishi mkongwe nchini, Masoud Sanani, ambaye waandishi wengi kwa namna mbalimbali wamepita mikononi mwake.
Sanan hivi sasa ni mgonjwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na yupo kwao Zanzibar, ambapo juzi niliwasiliana naye na amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku.
Kutokana na hali hiyo TASWA kwa kushirikiana na kamati hiyo imepanga kwenda kumjulia hali Jumapili Machi 22 mwaka huu.Tunaomba wadau waipe ushirikiano kamati yetu.
Walioteuliwa katika kamati hiyo na nafasi zao kwenye mabano ni Angela Msangi (Mwenyekiti), Majuto Omary (Katibu), Zena Chande (Mhazini),  Asha Kigundula, Isakwisa Mwaifuge  na Elias Kambili (Wajumbe).
 
D;MEDIA DAY
Maandalizi kuhusiana na bonanza kwa wanahabari yanaendelea na matumaini ni kuwa litafanyika Aprili 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam kama ilivyopangwa.
 
E;MSIBA WA KOCHA MARSH
TASWA imepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyepata kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Sylivestre Marsh, hivyo inatoa pole kwa familia na wanamichezo wote hapa nchini katika kuomboleza kifo cha kocha huyo.
 Marsh atakumbukwa na waandishi wa habari za michezo kutokana na ukaribu wake na alikuwa na ushirikiano wa kutosha pale alipoombwa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment