TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 18, 2015

Vijiji viwili kupata maji mwishoni mwa wiki hii

2
WAKAZI wa vijiji viwili vya Nyagasense na Rung’abure vilivyoko kwenye wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wamehakikishiwa kuanza kupata maji ifikapo mwishoni mwa wiki hii kufuatia wakandarasi wanaojenga miradi ya maji ya vijiji hivyo kuahidi kufikisha maji katika kipindi hicho. Akitoa ahadi kwa Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Nyagasense, Mhandisi wa mradi wa maji wa kijiji hicho John Mapande amesema maji yataanza kutoka siku tatu kuanzia leo. Mhandisi Mapande alitoa ahadi hiyo wakati Waziri Prof. Maghembe akizungumzia matumaini ya kukamilika kwa mradi huo wa maji ambapo aliwaomba wananchi wa kijiji hicho kukaa mkao wa kunywa maji. “Ninawomba sana mkae mkao wa kunywa maji kwa sababu nimeona kwa macho yangu na nimeridhika, vinginevyo nisingeweka jiwe la msingi, hivyo katika kipindi kifupi maji yatafika huku mitaani” alisema Waziri Prof. Maghembe Baada ya kutoa matumaini hayo, Waziri Prof. Maghembe alimuita mkandarasi wa mradi huo na kumsihi kukamilisha mradi huo na kwamba fedha zake zilizobaki atalipwa, na mazungumzo yao yailikuwa hivi: Waziri: Mkandarasi uko wapi? Mkandarasi: Niko hapa mheshimiwa Waziri. Waziri: Sasa wewe ukamilishe mradi wangu, ile miezi sita ikiisha fedha zako zitakazokuwa zimebaki tutakulipa, kwa hiyo we maliza mradi haraka wiki ijayo mimi ninywe maji hapa kabla sijakwenda Dar es Salaam. Mkandarasi: Nitajitahidi Mhe Waziri kukamilisha. Waziri: Jitahidi, maana kazi iliyobaki ni kidogo sana kukamilisha huu mradi Mkandarasi: Ni kazi ya siku mbili au siku tatu maji yatakuwa yameshatoka Waziri: Eeh sasa kazi ya siku mbili tatu mimi nitakuwa Mara hapa, nataka nikienda Mugumu nisimame hapa ninywe maji. Kwa upande wa mradi wa Maji wa kijiji cha Rung’abure, Waziri Prof. Maghembe alimuagiza mkandar akafunge jenereta na kupeleka pampu na kuifunga ili maji yaanze kusukumwa kuanzia leo. Waziri Prof. Maghembe alichukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wananchi kuzuia malori yanayopeleka jenereta na pampu kwenye eneo la mradi, kupita kwenye eneo lao, lakini Serikali ya kijiji ilimuhakikishia Waziri kwamba wananchi hao wameruhusu gari ipite. Waziri: bwana mkadarasi yuko wapi Mkandarasi: Nipo hapa mheshimiwa Waziri: Nimemuagiza huyu mkandarasi kesho alete jenereta ifungwe kwenye nyumba ya genereta na alete pampu pale ifungwe ili maji yaanze kusukumwa kesho (leo). Kwa hiyo muangalie atafunga kesho labda jioni atakuwa amekamilisha, lakini hata kama hakukamilisha Alhamisi atakamilisha, Alihamisi akikamilishwa bado nitakuwa mkao wa Mara. Kwa hiyo siku ya Alhamisi kwa uhakikka wataanza kusukuma maji, nimeona kazi nyingi hazijakamilika, lakini hiyo ikamilishwe kesho na Alhamisi ili sasa wakati wanaendelea na kazi nyingine mnaendelea kunywa maji. Baada ya kuzungumza hayo, wananchi walipiga vigelegele na makofi kuonesha kufurahishwa na hatua hiyo. Wakizungumza kufurahishwa na matumaini hayo ya kupata maji, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nyagasense wamesema wamefurahi kupata ujio wa Waziri na hatimaye kuahidiwa kupata maji. “Kwa kweli tumefurahi sana kupata ujio wa Waziri wa Maji na tumeridhika na ahadi ya kupata maji wiki hii kwa sababu tumekosa maji kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunapata shida ya kuyapata” alisema mkazi wa kijiji hicho Christina Machota. Mradi wa Maji wa kijiji cha Nyagasense unaotekelezwa chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira, unatumia chanzo cha kisima kirefu chenye uwezo wa kutoa maji lita 6000 kwa saa na utakapo kamilika utahudmia watu 5,530 na mifugo 2620. Mradi huo una jumla ya kilometa 19.54 za mtandao wa mabomba ya maji na vituo 20 vya kuchote maji na birika 2 za kunyweshea mifugo. Akiwasilisha taarifa ya mradi wa maji wa Rung’abure, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Serengeti Marwa Mulaza, alisema una chanzo cha maji mtiririko na hutoa lita 10,000 kwa saa na ulianza kutekelezwa Oktoba mwaka2013. Alisema mradi huo utakapokamilika utahudumia watu 3, 457 na mifugo na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Aprili mwaka huu 2015.

No comments:

Post a Comment