Usiku
wa kuamkia tarehe 1 Januari 2012, Jumuiya ya Watanzania, maafisa wa
Ubalozi pamoja na waalikwa kutoka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
pamoja na Balozi wa Malawi na Balozi wa Ethiopia nchini Zimbabwe
walihudhuria hafla ya kukaribisha mwaka mpya.
Waziri Dk Mwinyihaji Makame akutana na wabunge wa Afrika Mashariki
Waziri wa nchi
Ofisi ya Rais na menyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji
Makame,alipokuwa kaizungumza na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
ya Mashariki,walipofika ofisini kwake Ikulu Mjini Zanzibar jana,Wabunge
hao walisisitiza juu ya wananchi kupewa elimu ya kutosha kuhusu
Jumuiya hiyo na shuhuli zake kwa wajumbe,(kutoka Kulia) Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi
Uhaibuni,Khamis Ali,Mbunge Dk Said Kharib Bilal na Mbunge Bi Septuu
Mohamed.
(02/1/2012)
(Picha na Ramadhan Othman Ikulu).
MATUMLA AMGALAGAZA CHEKA KWA POINTI
Mohamed Matumla Kushoto na Cosmas Cheka wakioneshana uwezo wa kutupa Masumbwi jana huko mkoani Morogoro
Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akikingiana ngumi na Rais
Wa PST Emanuel Mlundwa kabla ya kuanza kwa mpambano jana
kutoka kushoto ni Rashid Matumla,Mohamedi Matumla,Mbwana Matumla na Mkwanda Matumla (picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com)
FAMILIA TANO ZAWAKAMBIA MORANI, ZAOGOPA KUTEMBEZWA MITAANI UCHI
Familia tano zenye
watoto zaidi ya ishirini zimelazimika kukimbia makazi yao ya kudumu kwa
kipindi cha wiki tano sasa kwa kuhofia kutembezwa uchi na kupigwa na
vijana wa kabila la kimasai”Morani”mara baaada ya kufanya ibada sanjari
na kufanya tohara kwa njia za kisasa zaidi
Familia
hizo zimelazamika kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao pamoja na maisha
ya watoto wao ambapo kundi kubwa la vijana wa kimasai wanawatafuta kwa
makosa ya kuharibu na kuvunja mila zao kwa njia ya Sala pamoja na
Kufanya tohara Mahospitalini.
Hayo
yametokea katika eneo la Oljoro Mkoani hapa ambapo kwa muda wa wiki
tano familia hizo zimelazimika kukimbia makazi yao kwa kuhofia
kutembezwa mitaani Uchi, pamoja na kupigwa kipigo kikali.
Akiongea
na WAANDISHI WA HABARI mmoja wa wanafamilia waliolazimika kukimbia
nyumba zao kwa hofu ya kutembezwa mitaani Uchi Bw Korduni Wilson,
alisema kuwa Morani hao wamekuwa wakifanya vibaya sana kwa kuwa mila
wanazozitaka zina madhara sana.
Bw
Korduni alieleza kuwa wameamua kufikia uamuzi huo wa kukimbia nyumba
zao kwa kuwa wao tayari wameshajua na kufahamu madhara ya kufanya tohara
kwa njia ya kienyeji sanjari na kuabudu mila ambazo Morani hao
wanazitaka.
“kati
ya hizi familia tano nyinginezo hazijakimbia kwa kuwa wamefanya tohara
kwa watoto wao bali Morani hao wamekuwa wakidai kuwa wanaharibiwa mambo
ya Kimila hasa pale wanaposali kwa maana hiyo wanakataa hata makanisa
kwa kuhofia Matambiko, na Mila”aliongeza Bw Korduni.
Pia
aliongeza kuwa mara baada ya Morani hao kuona kuwa Kanisa linakubali na
kusisitiza waumini wake kufanya Tohara kwa njia ya kisasa sanjari na
kukataa Mila ambazo zina madhara kwa Mtanzania Morani hao waliktaa amri
hiyo na kuvunja Kanisa la T.A.G oljoro hali ambayo ilisababisha hasara kubwa sana.
Katika hatua nyingine Msimamizi na Muangalizi wa
makanisa ya T.A.G mkoani hapa Bw Simion Vomo alisema kuwa wao kama
kanisa hawataweza kuwasikiliza Morani hao kwa kuwa madai yao hayana
Msingi Kisheria
Aliongeza
kuwa Kanisa litalazimika kuchukua hatua kali na za kisheria,kwa kuwa
Morani hao wanasababisha amani ndani ya miji na Maboma ya wananchi
kukosekana hali ambayo kama haitaweza kuchukuliwa tahadhari basi itazaa
matatizo makubwa sana katika jamii.
Awali Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoa wa Arusha Bw. Akili Mpwapwa alisema kuwa bado polisi wanaendelea
na Upelelezi,hivyo familia hizo tano ambazo zimelazimika kukimbia makazi
yao kwa kuwahofia Morani hao, wanatakiwa kutoa Taarifa ili Sheria
ichukue mkondo wake kwa kuwa wanachokifanya Morani hao ni Makosa.(Na:Shaaban Mpalule)
Shule ya kufundishia mpira yapata msaada wa vifaa vya michezo.
Na Gladness mushi , Arusha.
SHULE ya kufundisha mpira wa miguu ijulikanayo kama Future Stars
Academy iliyopo jijini hapa imenufaika na msaada wa vifaa vya michezo
vyenye thamani ya shs, 4.5 milion.
Msaada huo umetolewa na wafadhili kutoka chama cha mpira cha vijana
jimbo la Florida Marekani ikiwa ni njia mojawapo ya kuchangia swala
zima la michezo kwa shule hiyo.
Akizungumzia kuhusiana na shule hiyo , Mkurugenzi wake, Alfred Itaeli
alisema kuwa, lengo la shule hiyo ni kufundisha michezo kwa wanafunzi
waliopo mashuleni ambapo wanafunzi zaidi ya 152 kutoka shule mbali
mbali za mkoa wa Arusha wanafundishwa michezo katika shule hiyo.
Alisema kuwa, shule hiyo iliazishwa kwa lengo la kuinua vipaji vya
michezo kwa wanafunzi ambapo hadi sasa wana jumla ya timu sita kuanzia
umri wa miaka 11 hadi 17 .
Itaeli alisema kuwa, shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009 likiwa na lengo
la kuwaweka wanafunzi pamoja ambapo wanajifunza mpira wa miguu .
Ambapo mwaka jana wanafunzi hao wamefanikiwa kushiriki mchezo wa
kikombe cha ligi ya Afrika Mashariki ambapo mchezo huo ulifanyikia
Nairobi na ilizishirikisha jumla ya timu 94 ambapo timu hiyo ya Future
stars Academy ilifanikiwa kushinda nusu fainali ambapo lengo lao ni
kuchukua kombe .
‘pamoja na kuwa sisi tunajitahidi sana kuleta maendeleo ya michezo
katika jamii yetu kwa ujumla bado changamoto ni nyingi sana
zinazotukabili ,hivyo tunaomba watu binafsi na mashirika wajitokeze
kwa wingi kuchangia vifaa mbalimbali vya michezo kwani hivi bado
havitoshelezi ikilinganishwa na kuwa uhitaji ni mkubwa sana’alisema
Itaeli.
Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni apmoja na ukosefu wa viwanja
vya michezo na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza vijana hao
kwani michezo imeweza kwa kiasi kikubwa sana kuwaondoa katika
changamoto mbalimbali zikiwemo za kuondokana na makundi yasiyofaa(Na :Mwandishi Wetu)
MDAU WA WWW.ELIMUBORA.COM AMALIZA KOZI YA WEB DESIGN
Evance ambae anaratibu website ya www.elimubora.com
akiwa anapokea cheti baada ya kuhitimu kozi fupi nchini India.
Amewataka watanzania hususan wadau wa masuala ya IT kufuatilia udhamini
mbalimbali wa kozi fupi utolewao na chuo hicho kwa taarifa zaidi ingia
katika libeneke lake la www.elimubora.com
RAIS JAKAYA AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAWILI NA NAIBU KATIBU MKUU MMOJA IKULU DAR LEO
Rais Jakaya Kikwete aklimwapisha Mh Eliakim C. Maswi kuwa Katibu Mkuu
wizara ya Nishati na Madini katika hafla iliyofanyika Iukulu leo jijini
Dar es salaam.
(PICHA ZOTE NA IKULU)
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimpongeza na kumkabidhi
zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliackim Chacha, baada ya
kuapishwa leo Ikulu Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Paul, Katibu Mkuu
Ikulu, Peter Alanambula Ilomo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Eliackim Chacha, kabla ya kuapishwa wakati Makamu akiingia
katika Ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya
kuapishwa kwa makatibu hao walipokuwa wakisubiri kuapishwa rasmi
kushika nafasi hizo Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati
na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, Katibu Mkuu wa
wizara hiyo aliyeapishwa leo Januari 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa
Katibu huyo.
Rais
Dk. Jakaya Kikwete wa pili wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha
ya pamoja na Makamu wa rais Dk. Gharib Bilal wa pili kutoka kushoto na
makatibu walioapishwa leo kutoka kulia ni Mh Peter Ilomo Katibu Mkuu Ikulu, Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi,Balozi Ombeni Sefue katibu mkuu kiongozi na mwisho kushoto ni Mh Eliakim C. Maswi Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini
(Mwandishi Wetu).
UWF yatoa msada kwa familia iliothirika na mafuriko huko kigogo mji mpya
Mwenyekiti wa UWF
- Unity Of Women Friends,Mwate Madinda akikabidhi kiasi cha fedha
taslim kwa familia ya Mzee Shaaban Mkana,ambao walithirika na mafuriko
huko Kigogo mji mpya,jijini Dar,pamoja na kukabidhi kiasi cha fedha pia
UWF walitoa msaada wa vifaa, chakula na vitu mbalimbali,mwishoni mwa
wiki,Kushoto kwa Mwenyekiti ni Mwenyekiti wa mradi wa SOMKI (somesha
mtoto wa kike),Maryam Shamo pamoja na mwanachama wa UWF,Bi.Galina Ajmy.
UWF
- Unity Of Women Friends wakijumuika na marafiki wa karibu na
kukabidhi misaada ya vifaa, chakula na fedha taslim kwa familia ya mzee
Shaaban Mkana ambao waliathirika na mafuriko huko Kigogo mji
mpya,mwishoni mwa wiki.
Kikundi
cha UWF kimejikita katika kuwakomboa watoto wa kike wasio na uwezo
katika kupata elimu kupitia mradi wao wa SOMESHA MTOTO WA KIKE (SOMKI),
pia wamejiwekea utamadumuni wa kutembelea vituo mbali mbali kama
hospitali, vituo vya kulelea watoto n.k. kuwafariji wakati wa sikukuu
mbali mbali.Ukitaka kuona kazi mbalimbali zilizowahi kufanywa na UWF,(Mwandishi Wetu)
No comments:
Post a Comment