MIGOGORO ya ardhi imeendelea kuzikumba jamii nyingi katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kusababisha migogoro.
Jamii inatumia muda mwingi kutatua migogoro hiyo badala ya kufanya shughuli za maendeleo.
Hali
hiyo inatokana na ukweli kwamba, ardhi ndio tegemeo kubwa kwa jamii za
wakulima na wafugaji ambao ndio sehemu kubwa ya Watanzania.
Ardhi
ndio mtaji pekee ambao Watanzania wengi waishio vijijini wanaitegemea
kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kuweza kuwapatia chakula na kipato.
Licha
ya kuwepo kwa mamlaka zinazohusika na usimamizi pamoja na ugawaji wa
ardhi, migogoro hiyo imeendelea kuwa sehemu ya maisha kwa jamii nyingi.
Kama
sheria za usimamizi na umiliki wa ardhi zipo, kitu gani kinasababisha
migogoro ambayo inagharimu maisha na mali za Watanzania wasio na hatia?
Sisi
tunasema kuwa, sheria za ardhi zinatoa haki ya kutumia ardhi na si
kuimiliki hivyo inatosha kumhakikishia mtu kuwa, kitu chochote ambacho
atakiendeleza katika ardhi husika, kitalindwa kwa maslahi yake si lazima
kumwambia ardhi hiyo ni yako ili aiendeleze.
Migogoro ya
ardhi husababishwa na mambo mbalimbali ambayo baadhi yake ni upungufu
katika sheria za ardhi, mamlaka zinazohusika na ugawaji wa viwanja
kugawa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja na fidia ndogo.
Licha
ya kufanyika marekebisho katika sheria za kusimamia matumizi ya ardhi,
bado migogoro hiyo imeendelea kuchukua nafasi miongoni mwa jamii nyingi
za Kitanzania.
Upo umuhimu mkubwa wa kushirikisha jamii katika
kufanya maamuzi yanayohusu matumizi ya ardhi. Kama wananchi
watashirikishwa, migogoro mingi iliyopo vijiji itapungua.
Ipo
tabia ya baadhi ya Halmashauri za vijiji, kupitisha taarifa feki
inayoamua matumizi ya ardhi ya kijiji bila ridhaa ya wananchi.
Serikali
nayo inachangia migogoro hii pale inaposhindwa kulipa fidia kwa
wananchi baada ya kutwaa ardhi kwa ajili ya kufanikisha miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Umefika wakati wa wananchi kuelimishwa
juu ya sheria mbalimbali za ardhi ili watambue haki na wajibu wao katika
suala zima la umiliki na matumizi ya yake.
|
Posted: 15 Apr 2012 11:41 PM PDT
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma, bado inakabiliwa na tatizo la mimba katika shule mbalimbali za msingi na sekondari. Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Bi. Betty Mkwasa, aliyasema hayo juzi wakati
akizungumza na wadau wa elimu na kujadili changamoto zinazowakabili
wanafunzi.
Alisema tatizo la mimba na utoro kwa wanafunzi limekuwa sugu na kuwaomba wadau hao, waone umuhimu wa kulitafutia ufumbuzi.
Bi.
Mkwasa alisema tatizo hilo linatokana na changamoto mbalimbali za
baadhi ya wanafunzi wa sekondari kutembea umbali mrefu, kukosekana kwa
hosteli na zile zilizopo nyingi hazitambuliki 'bubu' na hazina ulinzi
kwa watoto hao.
Aliongeza kuwa, wanafunzi wengi wa kike wanaosoma
sekondari wamepanga mitaani ambapo nyumba wanazoishi si salama kwa
maisha yao jambo linalosababisha baadhi ya wasichana kuingia kirahisi
katika vishawishi.
“Halmashauri hii pia inakabiliwa na tatizo
kubwa la utoro kwa wanafunzi shuleni hivyo kusababisha wale wanaofaulu
shule ya msingi kwenda sekondari, kutoripoti shuleni na hawafuatiliwi.
“Kutokana
na hali hii, nawaagiza Watendaji wa Kata na Vijiji, kuhakikisha
mnawafuatilia wanafunzi watoro na kuwachukulia hatua wazazi au walezi wa
wao,” alisema Bi. Mkwasa na kusisitiza kuwa, suala la miundombinu
katika shule mbalimbali za msingi na sekondari hairidhishi.
Alisema
halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu, matundu
ya vyoo kwa shule mbalimbali na thamani za shule hivyo aliwaomba wadau
hao kutafuta ufumbuzi.
|
Posted: 15 Apr 2012 11:38 PM PDT
Meneja
Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu (katikati), akionesha
nambari ya Mshindi wa Droo kubwa ya mwezi ya kumpata mshindi wa
promosheni ya M-PESA, ambapo mkazi wa Kitangiri mkoani Mwanza, Bw.
Revocatus Mkama, alishinda na kupata sh. milioni 10. Kushoto ni Mkaguzi
wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Maggid na Mtaalamu wa
huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom, Bi. Reenu Verma. (Na Mpigapicha
Wetu) Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam KA M P U N I y a Ma w a s i l i a n o y a Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya M-Pesa hadi asilimia 20 kwa mteja anapotoa fedha kwa wakala yeyote wa huduma hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Bw. Rene Meza alisema gharama hizo zimepunguzwa rasmi kuanzia leo kwa wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na hudu ma ya Vodacom M-Pesa. "Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi M-Pesa ilivyokua huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu," alisema Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama mpya za kutoa fedha. Alisema upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya kampuni ya kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia sh. 50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya siku 90 iitwayo 'Tuma na Ushinde' ambapo sh. milioni 480 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni. Alisema jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na wanajiwezesha kupitia huduma ya M-Pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye M-Pesa ili kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya kila siku ya wateja
|
Posted: 15 Apr 2012 11:32 PM PDT
Na Mwandishi Wetu MBUNGE
wa Kawe Bi. Halima Mdee (CHADEMA) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Bi.
Ester Bulaya (CCM) wameamua kujitokeza kumsaidia msanii Elizabeth
Michael ‘Lulu’ anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa mwigizaji marehemu Steven
Kanumba. Wabunge hao juzi waliamua kwenda kumuona Lulu na kwa sasa wameamua kuendesha kampeni ya kuchangisha fedha za malazi kwa ajili ya familia yake. Bi. Mdee kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Twitter alisema Lulu anahitaji mwanasheria makini wa kuweza kumnasua kwenye kesi hiyo akiwemo Mwanasaikolojia wa kuzungumza naye ili aweze kuwa vizuri kiakili. Mbunge huyo wa Jimbo la Kawe aliandika katika ukurasa huo kuwa “Leo (mwishoni mwa wiki) mimi na Mheshimiwa Bulaya tulikwenda kumuona Lulu Oysterbay Polisi. ‘She really needs our support’ ( kwa kweli anahitaji msaada wetu). Kwanza ‘she is only 17’ (kwanza huyu ni binti wa miaka 17 tu). “Pili anahitaji sana psychological support (msaada wa kisaikolojia). Nawaomba watu wenye taaluma hiyo wasisite kwenda kumuona. Wasiliana na 0714282527 Steve Nyerere. Tatu anahitaji wanasheria makini wa kumsaidia na kwa yeyote ambaye yuko tayari naomba awasiliane nami 0759 569823 (Halima Mdee). Nne, at that tender age (kwa umri huo Lulu) ndio alikuwa anategemewa na familia yake. Now (sasa) yuko ndani matatizo yamezidi kuwa makubwa. “Kwa yeyote anayeguswa, naomba atume chochote kwenye namba hii 0754 878890 ni namba ya M-Pesa ya mama yake tumsaidie huyu mtoto!...”Again (tena).. namba ya M-PESA kwa wanaotaka kumsaidia Binti yetu Lulu ni +255754878890. Ni namba ya mama yake,” aliongeza Bi.Mdee.
|
Posted: 15 Apr 2012 11:29 PM PDT
Na Mwandishi Maalum, Ikulu
Zanzibar SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kulinda
uhuru wa dini zote lakini haitavumilia vitendo vyovyote vya uvunjaji wa
sheria vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa jina la dini huku ikisisitiza
uadilifu kwa viongozi wa dini. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo -jana katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya kumweka wakfu Askofu wa 10 wa Dayosisi ya Zanzibar Michael Henry Hafidh. Alisema, ustawi wa dini mbalimbali Zanzibar unahusika na Sera ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya uhuru wa kuachia kanisa kuendesha seminari zao na makongamano yao bila ya kuingiliwa. Alieleza kuwa, kwa kiasi kikubwa shughuli hizo za kidini zimekuwa zikiendeshwa kwa amani ambapo kwa bahati mbaya pamoja na hayo kumekuwepo nyakati ambapo kutofahamiana kumejitokeza katika baadhi ya akongamano. "Serikali imeweka utaratibu maalum wa utoaji ruhusa wa makongamano hayo, taratibu hizo ni pamoja na utunzaji wa amani nakutobughu dhiana kidini‚ tuelewe sote kwamba viongozi wa dini ni walimu na walezi wa jamii na anadhamana kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu," alisema Dkt.Shein. Aidha, alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kufanya kila linalowezekana kulinda haki za Watanzania katika kufuata dini na kuabudu dini waitakayo na kuishi bila ya kubaguliwa kutokana na sababu ya dini, kabila au rangi. Alisema, hakuna budi wananchi wote kwa pamoja kujivunia na kuiendeleza hali ya amani na utulivu iliyopo hapa nchini ambapo ziko nchi mbalimbali wamekuwa wakikosa hali hiyo kwa sababu ya migogoro inayotokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kidini, kisiasa na kikabila, Pamoja na hayo Dkt. Shein alisema kuwa licha ya kuwa Tanzania haina dini ya serikali kama ilivyokuwa ikisisitizwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wa amamu zilizofuata lakini Watanzania wengi ni wafuasi na waumini wa dini zenye madhehebu tofauti. Kutokana na hilo Dkt. Shein alisisitiza jukumu la kulinda heshima baina wananchi na usalama wa nchi linategemea sana mafunzo yanayofundishwa na yanayohutubiwa na viongozi katika nyumba za ibada. Pia, alisisitiza viongozi wa dini mbalimbali wana wajibu wa kuhakikisha sehemu za ibada zinatumika kwa ibada tu bila ya kuingiza mambo mengine na kutoa mwito kwa Jumuiya zote za kidini na wananchi kuendelea kuheshimiana na kuishi bila ya kubaguana. "Sote tuwe na lengo moja la kuiletea maendeleo nchi yetu kwa manufaa ya watu wake wote,” alisema Rais. Pia Dkt. Shein aliwaeleza waumini hao kuwa mambo yao waliyomueleza ameyasikia na atayafanyia kazi.
|
Posted: 15 Apr 2012 11:27 PM PDT
Na Pamela Mollel, Manyara SHUGHULI za uchimbaji wa madini katika Kitalu D eneo la Mererani wilayani S ima n j i r o Mk o a wa Manyara umesimamishwa kwa muda na Ofisi ya Madini Kanda ya Kaskazini baada ya kuibuka kutoelewana kwa wamiliki wa mgodi huo. Mg o d i u l i o s imami s hwa unamilikiwa na wakazi wawili wa mkoani Arusha ambao ni Bw.Kitinda Kimaro pamoja na Anthony Ngoo ambapo ulipewa leseni ya uchimbaji yenye namba PML No.0003601 miaka iliyopita. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyolifikia gazeti hili kwa masharti ya kutokutaka majina yao yaandikwe magazetini vilidai kwamba ofisi hiyo imesimamisha kwa muda wa mwezi mmoja shughuli za uchimbaji katika mgodi kuanzia Machi 26 mwaka huu hadi Mei 3, mwaka huu. Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa lengo la kusimamishwa kwa shughuli hizo za uchimbaji katika eneo hilo, lililenga kutoa muda kwa pande mbili zinazovutana kutafuta suluhu ya namna ya kufanya kazi kwa maelewano. Hata hivyo, Majira ilifanikiwa kupata nakala ya barua ya kusimamisha shughuli za uchimbaji katika mgodi huo yenye Kumb.Na DA 74|503|VOL II|160 ya Machi 26 mwaka huu iliyoandikwa na kusainiwa na Ofisa Madini Mkazi wa Mererani mkoani Manyara Injinia L .P Mayala. Katika barua hiyo ambayo nakala imepelekwa moja kwa moja kwa Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Mkuu wa Kituo cha Polisi Machimboni pamoja na kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi na Usalama ilitaka pande mbili kuwasilisha mapendekezo wa kufanya kazi kwa maelewano mnamo Aprili 3, mwaka huu. Ha t a h i v y o , g a z e t i h i l i lilipowasiliana na Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Bw.Benjamin Mchwapaka alikiri ofisi yake kusimamisha kwa muda shughuli za uchimbaji katika mgodi huo huku akisema kuwa wanasubiri maagizo waliyoyatoa kwa pande zote mbili yatekelezwe hadi pale watakapokutana tena. Alisema kwamba, pande mbili zinazovutana katika mgodi huo endapo zisipoweza kukubaliana ofisi yake itachukua maamuzi magumu kwa kuzingatia maslahi ya pande zote huku akikataa kuzungumzia maamuzi yatakayochukuliwa.
|
Posted: 15 Apr 2012 11:21 PM PDT
Kiungo
wa Manchester United, Michael Carrick (kushoto) akichuana na
mshambuliaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor katika mechi ya Ligi Kuu
ya Uingereza iliyochezwa jana Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester.
(AFP)
|
Posted: 15 Apr 2012 11:18 PM PDT
Na Elizabeth Mayemba VINARA
wa Ligi Kuu Simba, jana waliendeleza ubabe katika mechi za ligi hiyo
baada ya kuinyuka Maafande wa Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao la Simba lilifungwa dakika ya 80 kupitia kwa Patrick Mafisango ambaye alipokea pasi ya Haruna Moshi 'Boban'.
Kwa
ushindi huo Simba imeendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na
pointi 53, ikifuatiwa na Azam FC ambayo imefikisha pointi 50.
Simba
ilianza kwa kishindo mechi hiyo, ambapo dakika ya saba Salum Machaku
akwa na kipa wa Ruvu alishindwa kuiandikia bao timu yake baada ya
kuchelewa kupiga shuti na kuwahiwa.
Dakika ya saba Simba ilikosa
bao lingine kupitia kwa mshambuliaji wake Gervas Kago ambaye kabla ya
kupasiwa Boban Na Victor Costa 'Nyumba' waligongeana na vyema lakini,
Kago akashindwa kutumbukiza mpira kimiani.
Baada ya kosa kosa
hizo, Ruvu Shooting ilizinduka dakika ya 18 Mohamed Kijuso akiwa na kipa
Juma Kaseja alishindwa kutumbukiza kimiani baada ya kuwahiwa na Costa.
Kipindi
cha pili Ruvu Shooting walionekana kuimarika na dakika 48, Abdallah
Juma ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Kijuso alishindwa kufunga akiwa
na wavu huku kipa Kaseja akiwa ametoka golini.
Katika kipindi hicho Simba iliwatoa Kago na Machaku na kuwaingiza Uhuru Selemani na Edward Christopher.
Dakika
ya 78 Mafisango alikosa bao la wazi baada ya kupasiwa pasi murua na
Uhuru Selemani, lakini hata hivyo badala ya kufunga akapaisha mpira juu.
|
No comments:
Post a Comment