Maafisa Ubalozi wa Tanzania
nchini Japani, Jilly Maleko na Francis Mossongo wakijiandaa tayari kwa
matembezi ya hisani yenye lengo la kuhamasisha juhudi za kufufua uchumi
na utalii wa jiji la Yokohama.
Maandalizi yakiendelea
Watanzania
wanaoishi nchini Japani wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wengine
kutoka mataifa ya Afrika katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa
matembelezi hayo.
Watanzani wakipeperusha bendera ya Tanzania katika Matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na jiji la Yokohama
Matembezi yamekolea, Mwenyekiti wa watanzania wanaoishi nchini Japani Radhid Njenga (mwenye kanzu) naye alikuwemo.
Noboru
Ninomiya (mwenye picha ya tingatinga) mwenyeji wetu katika matembezi
haya akiwa sambamba na Francis Mossongo, Afisa Ubalozi.
Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani,
wamewaongoza watanzania wanaoishi hapa kushiriki katika matembezi ya
hisani ya mji wa Yokohama, ikiwa ni moja ya hatua za kukuza urafiki kati
ya jijini hilo na Tanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na
hata mataifa ya Afrika kushiriki rasmi kwenye matembezi hayo ambayo
yamekuwa yakifanyika kila mwaka. Mwaka huu, Tanzania kutokana na
historia yake ya kupenda, kusimamia na kutetea amani, umoja na
mshikamano duniani.
Aidha katika siku za usoni, mji wa
Yokohama una mpango wa kuanzisha uhusiano (Sistercity Friendship) na
moja ya miji ya Tanzania, uhusiano ambao utajumuisha kupanda miti aina
ya Cherry blossom katika mji utakaochaguliwa Tanzania.
Matembezi
hayo yalianzishwa mwaka 1953 kwa lengo la kuhamasisha jitihada za
kufufua uchumi na utalii wa mji wa Yokohama kufuatia uharibifu
uliotokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
No comments:
Post a Comment